Wapo baadhi yetu ambao wanaamini kuwa "sera za CCM ni nzuri ila zimekosa watekelezaji tu". Wapo wanaoamini kuwa sera hizi ni nzuri sana vitabuni ila hazijapata watu wazuri kuweza kuzifanyia kazi. Wengine wamefikia kuamini kuwa uzuri wa sera hizi unasababisha hata nchi jirani kuzi"copy" na kuzi"paste" kwenye mipango yao. Wale wenye kuamini hivi hatimaye huamini kuwa siku moja CCM itaweza kupata watu wazuri wa kuzitekeleza sera zake - hadi hivi sasa inaonekana watu hao hawapo. Miaka hamsini ya kutawala ati hawajapatikana watu wakuzitekeleza sera hizi vizuri.![]()
Sisi wengine tunasema siyo tu wamekosa watu wa kuzitekeleza bali hata wakipata watu wazuri kiasi gani sera hizo hazitekelezeki. Hazitekelezeki kwa sababu ni sera mbovu zilizoandikwa kwa maneno mazuri. Kwa watu wanaopenda maneno matamu ni rahisi sana kuhadaika na sera hizo.
Mfano mzuri ni hili la Kenya kutuwekea ngumu mabasi yetu ya kubeba watalii (tour buses) kutumia viwanja vyao kwa ajili ya watu wetu kubeba watalii na kuja nao Bongo. Ukiangalia kwa haraka haraka utaona kuwa ni matokeo ya kushindwa kwa sera mbalimbali; kuanzia ya usafiri, uchukuzi, uchumi n.k Sasa watu wengine wanapolalamikia Kenya na kuona kama Wakenya hawaoneshi kujali udugu na ujirani mwema wanasahau kuwa ukipanda mbigili usitegemee kuvuna mpunga! Tunavuna tulichopanda.
Inawezekana vipi katika mipango yetu yote na matumizi yote ya hela kwa miaka hamsini na ushee bado tunategemea huruma na hisani ya majirani zetu kufanikisha mojawapo ya kinachoitwa ni sekta muhimu sana? Hivi kwa muda wote huo watawala wetu walioshindwa wamekuwa wakinufaika kwa sababu ya huruma ya Kenya? Hivi wamesahau kabisa historia? Cha jirani siyo chako; hata kama kakuazima.
Kwamba kisa ni masuala ya sheria ya miaka 30 iliyopita ambayo inaonekana kushindwa kwenda na wakati au mahitaji nalo linathibitisha tu kushindwa kwa viongozi wetu. Hivi hatuwezi kufikiri mbali hadi itokee migogoro? Inawezekana kweli watawala wetu wanaendeshwa na matukio na siyo maono yenye kueleweka? Wengine wanasema na sisi tulipize kisasi; sawa lakini mwisho wake ni nini? Inaonekana kwenye utalii sisi ndio tuko kwenye huruma ya Wakenya.
Angalia kwenye sekta nyingine vile vile utaona tatizo hili la kushindwa kwa sera zao liko wazi japo hatujapata watu wenye kulionesha hili bayana. Miye nimedokeza kitu ambacho kiko dhahiri. Cha kushangaza na kusikitisha kuwa wapo baadhi yetu bado wanafikiria kuwapa tena watu wale wale miaka mingine mitano ya kujaribu sera zile zile ambazo zimethibitika kushindwa huko nyuma ati kwa vile watakuwa na sura tofauti. Kwani tatizo letu sisi sura? Ni sera.
Kama kuna mtu anasema wana sera nzuri; naombeni hata mfano mmoja wa maana wa uzuri wa sera zao.
mwanakijiji sema neno lolote kwenye mada hii ukizingatia kipindi hiki cha uchaguzi.
Last edited by a moderator: