Tunaposema Sera za CCM zimeshindwa hatutanii, mfano hai huu..

Tunaposema Sera za CCM zimeshindwa hatutanii, mfano hai huu..

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
301102_518863438129478_1120496333_n.jpg
Wapo baadhi yetu ambao wanaamini kuwa "sera za CCM ni nzuri ila zimekosa watekelezaji tu". Wapo wanaoamini kuwa sera hizi ni nzuri sana vitabuni ila hazijapata watu wazuri kuweza kuzifanyia kazi. Wengine wamefikia kuamini kuwa uzuri wa sera hizi unasababisha hata nchi jirani kuzi"copy" na kuzi"paste" kwenye mipango yao. Wale wenye kuamini hivi hatimaye huamini kuwa siku moja CCM itaweza kupata watu wazuri wa kuzitekeleza sera zake - hadi hivi sasa inaonekana watu hao hawapo. Miaka hamsini ya kutawala ati hawajapatikana watu wakuzitekeleza sera hizi vizuri.

Sisi wengine tunasema siyo tu wamekosa watu wa kuzitekeleza bali hata wakipata watu wazuri kiasi gani sera hizo hazitekelezeki. Hazitekelezeki kwa sababu ni sera mbovu zilizoandikwa kwa maneno mazuri. Kwa watu wanaopenda maneno matamu ni rahisi sana kuhadaika na sera hizo.

Mfano mzuri ni hili la Kenya kutuwekea ngumu mabasi yetu ya kubeba watalii (tour buses) kutumia viwanja vyao kwa ajili ya watu wetu kubeba watalii na kuja nao Bongo. Ukiangalia kwa haraka haraka utaona kuwa ni matokeo ya kushindwa kwa sera mbalimbali; kuanzia ya usafiri, uchukuzi, uchumi n.k Sasa watu wengine wanapolalamikia Kenya na kuona kama Wakenya hawaoneshi kujali udugu na ujirani mwema wanasahau kuwa ukipanda mbigili usitegemee kuvuna mpunga! Tunavuna tulichopanda.

Inawezekana vipi katika mipango yetu yote na matumizi yote ya hela kwa miaka hamsini na ushee bado tunategemea huruma na hisani ya majirani zetu kufanikisha mojawapo ya kinachoitwa ni sekta muhimu sana? Hivi kwa muda wote huo watawala wetu walioshindwa wamekuwa wakinufaika kwa sababu ya huruma ya Kenya? Hivi wamesahau kabisa historia? Cha jirani siyo chako; hata kama kakuazima.

Kwamba kisa ni masuala ya sheria ya miaka 30 iliyopita ambayo inaonekana kushindwa kwenda na wakati au mahitaji nalo linathibitisha tu kushindwa kwa viongozi wetu. Hivi hatuwezi kufikiri mbali hadi itokee migogoro? Inawezekana kweli watawala wetu wanaendeshwa na matukio na siyo maono yenye kueleweka? Wengine wanasema na sisi tulipize kisasi; sawa lakini mwisho wake ni nini? Inaonekana kwenye utalii sisi ndio tuko kwenye huruma ya Wakenya.

Angalia kwenye sekta nyingine vile vile utaona tatizo hili la kushindwa kwa sera zao liko wazi japo hatujapata watu wenye kulionesha hili bayana. Miye nimedokeza kitu ambacho kiko dhahiri. Cha kushangaza na kusikitisha kuwa wapo baadhi yetu bado wanafikiria kuwapa tena watu wale wale miaka mingine mitano ya kujaribu sera zile zile ambazo zimethibitika kushindwa huko nyuma ati kwa vile watakuwa na sura tofauti. Kwani tatizo letu sisi sura? Ni sera.

Kama kuna mtu anasema wana sera nzuri; naombeni hata mfano mmoja wa maana wa uzuri wa sera zao.
 
Sera za ccm ni mbovu haswa lakini ukizizikiliza kupitia viongozi wao utaona kama NZURI! Mathalani, wengi tunajua ubovu na madudu ya ESCROW na kwamba ni wazi sera ya WIZARA ya NISHATI NA MADINI ni mbovu lakini alipopewa nafasi ya kulifafanua jambo hili, WAZIRI Muhongo alitumia maneno matamu hadi kufanya wananchi wengine kuanza kutetea eti Muhongo ni kiongozi bota!
 
Mkuu Mwanakijiji, wakati mwingine ukiangalia Rasilimali kuanzia watu,madini ardhi ya kutosha tena yenye rutuba inayopaswa kustawisha mazao yoyote yale ya Chakula then uoanishe na nchi hapa ilipo unashangaa, kwakweli, huwezi pata jibu kama kweli wewe ni mtu makini mwenye uelewa wa kutosha.

Nchi hii imezungukwa na takribani nchi nane zinazotegemea bandari yetu kwa namna moja ama nyingine, badala ya kukaa na kubuni mbinu mikakati itakayowezesha kuchangamkia fursa hii adimu kabisa sisi tunaangalia upenyo wa kuweza kupiga dili na kupata choochote kwaajili ya matumbo, tubaangalia ya leo huku tukidai ya kesho yatanishughulikia yenyewe...!!!

Some time unajikuta kumkufuru Mungu kwa kutupendelea yote haya na KUTUNYIMA AKILI.

Kwa nchi yetu kuanzia ukubwa,population,rasimali ilikuwa si nchi ya kuchimbwa mkwara na Nchi kama Kenya, Kama tungekuwa na watu wanaofikiri sawasawa na kitenda kwa hofu ya kizazi kijacho hakika tusingekuwa hapa tulipo, Inasikitisha sana, leo hii nchi kama Rwanda inashirika lake makini kabisa la usafiri wa amga lenye Ndege za kutosha huku sisi tuking'ng'ana na kale kale ka ndege Chakavu huku tukikodi hata visivyokodiwa (Vilivyokataliwa na wenetu huko)

Kwa kweli inasikitisha inatia uchungu, nchi hii bila Watanzania kuonyesha hadharani kwamba tumechoka na hawa wapiga dili (ccm) Titapigwa bao mpaka na nchi kama Sidan kusini iliyotoka juzi tu hapa kwenye vita vya wenyeqe kwa wenyewe. Unakuja uchaguzi hapa baadaye hawa walioshindwa wataonyesha wameshinda tena iwe kweli ama kimagumashi laiki watatutawala tena na kuendeleza yale yale business as usually....!!! Sijui tunataka aje nani kutuonyeaha kwa vitendo kwamba hawa jamaa wameahindwa kusogeza mbele gurudumu la Maendeleo kwa Taifa letu.

Inauma sana.

BACK TANGANYIKA
 
Mkuu nakuna maono yoyote wala.mipango yoyote kwenye serikali hii ya kikwete.

Madharani mpaka sasa hatujui tarehe wala siku ya Uchaguzi mkuu.
Wala hakuna dalili zaidi ya maneno matupu.

Kwa hili wenzetu wamarekani. Uchaguzi mkuu ni mwakani siku ya Jumanne tareh 08 Nov 2016.

Kila raia anajui siku na tarehe. Mwaka mmoja zaid. Wameenda mbali mpaka tarehe ya kuapishwa na kushika madaraka rasmi vyote vimeshapangwa mpaka sasa.

Tanzania uchaguzi ni mwaka huu 2015. Mpka sasa tunaambiwa ni October bila kujua tarehe wala siku.

Achilia mipango hiyo. Mpaka sasa wagombea hawajulikani kwa Umma. Ten kwa maCCM ukitangaza unapigwa na ban.

Hapo tutawezaje kupanga mipango ya Taifa miaka 5 ama kumi kama matukio muhimu tu hakuna vision?
 
Sera za ccm ni mbovu haswa lakini ukizizikiliza kupitia viongozi wao utaona kama NZURI! Mathalani, wengi tunajua ubovu na madudu ya ESCROW na kwamba ni wazi sera ya WIZARA ya NISHATI NA MADINI ni mbovu lakini alipopewa nafasi ya kulifafanua jambo hili, WAZIRI Muhongo alitumia maneno matamu hadi kufanya wananchi wengine kuanza kutetea eti Muhongo ni kiongozi bota!

Naam! Mfano mwingine hai huo.. na wapo wanaoamini kuwa watu wale wale wakija 2015 wataweza kutatua tatizo la nishati!
 
Mkuu nakuna maono yoyote wala.mipango yoyote kwenye serikali hii ya kikwete.

Madharani mpaka sasa hatujui tarehe wala siku ya Uchaguzi mkuu.
Wala hakuna dalili zaidi ya maneno matupu.

Kwa hili wenzetu wamarekani. Uchaguzi mkuu ni mwakani siku ya Jumanne tareh 08 Nov 2016.

Kila raia anajui siku na tarehe. Mwaka mmoja zaid. Wameenda mbali mpaka tarehe ya kuapishwa na kushika madaraka rasmi vyote vimeshapangwa mpaka sasa.

Tanzania uchaguzi ni mwaka huu 2015. Mpka sasa tunaambiwa ni October bila kujua tarehe wala siku.

Achilia mipango hiyo. Mpaka sasa wagombea hawajulikani kwa Umma. Ten kwa maCCM ukitangaza unapigwa na ban.

Hapo tutawezaje kupanga mipango ya Taifa miaka 5 ama kumi kama matukio muhimu tu hakuna vision?

Mifano mizuri; lakini si unaona hata watu makini wanavyotumia muda kuwapa legitimacy na relevance wanaotangaza nia ndani ya CCM kana kwamba tumeshakubali Rais ajaye lazima atoke CCM?
 
Hivi kuna mtalii mwenye akili timamu atakuja kwenye Airport ya namna hii?

Mwanakijiji inaelekea wewe bado unaishi kwenye dimbwi la alinacha

Tatizo unaanzisha thread ku target CCM

Dawa ungelenga wahusika kwa majina kuanzia FOREIGN, MALIASILI NA UTALIII, AFRCA MASHARIKI, IKULU

hapo ndio huwa wanashtuka na kupanic

Ukitaja CCM none of those clowns cares...mbaya zaidi ungetegemea waziri KIVULI wa utalii angeiita press conference na kikipaka Mmavi mmavi lakini wapi ..... kilichobaki ni hii hii JF ya SIRIKALI...(siku wakiwa na mood wanaondoa kabisa na threads zinawalenga)

Last edited by a moderator:
Mkuu Mwanakijiji, wakati mwingine ukiangalia Rasilimali kuanzia watu,madini ardhi ya kutosha tena yenye rutuba inayopaswa kustawisha mazao yoyote yale ya Chakula then uoanishe na nchi hapa ilipo unashangaa, kwakweli, huwezi pata jibu kama kweli wewe ni mtu makini mwenye uelewa wa kutosha.

Labda hili linaelezea ni kwanini JK alisema hajui kwanini Tanzania ni maskini. Labda jibu ni sera zao zisizotekelezeka ndio kiini cha matatizo yetu.
 
Hivi kuna mtalii mwenye akili timamu atakuja kwenye Airport ya namna hii?

Mwanakijiji inaelekea wewe bado unaishi kwenye dimbwi la alinacha

Tatizo unaanzisha thread ku target CCM

Binafsi naamini tatizo la msingi liko huku kwenye CCM; siyo suala la taasisi au watendaji. Ni chama. Zamani tulisema "chama chashika hatamu" sasa hivi hata hivyo "chama kimeshika tama". Hakitoi uongozi ambao ungeweza kuonekana kwenye hizi taasisi mbalimbali. Matokeo yake taasisi na idara zinajiendea alimradi zinakwenda...
 
sera za CCM siyo tu ni mbovu bali ni hatarishi kwa amani, usalama, utulivu na uchumi wa watanzania... CCM imefeli ktik kila nyanja... niambieni eneo moja ambayo ccm imefanikiwa..
 
Mwanakijiji, Kikwete alikuwa na dhamira njema ya kuweka misingi imara ya kulipeleka taifa mbele, akaona aanze na kuandika katiba mpya kabisa, alichagua team makini ya akina warioba baregu salim. badae akaunda bunge la katiba lililojumuisha kila uwakilishi.

Alihakikisha watu makini wanapewa kutengeneza kanuni zitakazoongoza uendeshaji wa bunge la katiba, kazi hiyo akapewa mzee wetu Tundu Lissu, cha kushangaza akatunga kanuni mbovu na za hovyo kiasi kwamba hata yeye mwenyewe akashindwa kuzitumia, na baada ya kuona hilo basi akae kupambana angalau tuokoe chochote akabeba virago akatimua akabaki kununua viandishi vya habari vya kipuuzi na kumwandika kila gazeti.

Tunaweza inyoshea vidole ccm, tuseme ukweli miaka yote report ya CAG ilikuwa haiendi bungeni JK akaamuru ipelekwe bungeni na ijadiliwe kwa uwazi na wahusika wawajibike, badala yake tunageuza report zile kuwa sehemu ya kupigia fitina, sote tunajua biashara ya iptl ilikuwa ya nani lakini tukamshupalia muhongo kipumbavu tu, haya tunaondoa muhongo tunamweka simbachawene halafu tunajiona washindi "hovyo kabisa"

Nashindwa kuelewa tunamwondoa balozi kagasheki tunaweka nyalandu hivi kichwani zinatutosha kweli? haya mambo hayaendi na hatuna mtu wa kutukwamua gharasha tumelamba wenyewe tunafungwa sasa, inakuwaje?
 
Binafsi naamini tatizo la msingi liko huku kwenye CCM; siyo suala la taasisi au watendaji. Ni chama. Zamani tulisema "chama chashika hatamu" sasa hivi hata hivyo "chama kimeshika tama". Hakitoi uongozi ambao ungeweza kuonekana kwenye hizi taasisi mbalimbali. Matokeo yake taasisi na idara zinajiendea alimradi zinakwenda...

Chama tawala kina sera mbovu kwasababu huwa hazitokani na tafiti bali hutokana na matakwa ya walio madarakani. Mfano sera ya Elimu..shule za kata hazikufanyiwa utafiti wowote ndo maana ukikutana na mhitimu wa shule ya kata na mhitimu wa primary hakuna tofauti. Utaambiwa elimu bure wakati in reality kuna michango kibao. Sera ya kilimo nayo hakuna utafiti. Kilimo kwanza hakijaleta manufaa yeyote kwa wananchi. Mfano kumkopesha mwananchi power tiller alipe kwa instalments ni sawa lakini kutokana na ni bidhaa fake anaenufaika cyo mkulima bali ni mfanyabiashara. Ukija sera ya afya bure kwa wazee, ni uongo mtupu hakuna mzee anayetibiwa bure.
 
Mwanakijiji, Kikwete alikuwa na dhamira njema ya kuweka misingi imara ya kulipeleka taifa mbele, akaona aanze na kuandika katiba mpya kabisa, alichagua team makini ya akina warioba baregu salim. badae akaunda bunge la katiba lililojumuisha kila uwakilishi.

Alihakikisha watu makini wanapewa kutengeneza kanuni zitakazoongoza uendeshaji wa bunge la katiba, kazi hiyo akapewa mzee wetu Tundu Lissu, cha kushangaza akatunga kanuni mbovu na za hovyo kiasi kwamba hata yeye mwenyewe akashindwa kuzitumia, na baada ya kuona hilo basi akae kupambana angalau tuokoe chochote akabeba virago akatimua akabaki kununua viandishi vya habari vya kipuuzi na kumwandika kila gazeti.

Tunaweza inyoshea vidole ccm, tuseme ukweli miaka yote report ya CAG ilikuwa haiendi bungeni JK akaamuru ipelekwe bungeni na ijadiliwe kwa uwazi na wahusika wawajibike, badala yake tunageuza report zile kuwa sehemu ya kupigia fitina, sote tunajua biashara ya iptl ilikuwa ya nani lakini tukamshupalia muhongo kipumbavu tu, haya tunaondoa muhongo tunamweka simbachawene halafu tunajiona washindi "hovyo kabisa"

Nashindwa kuelewa tunamwondoa balozi kagasheki tunaweka nyalandu hivi kichwani zinatutosha kweli? haya mambo hayaendi na hatuna mtu wa kutukwamua gharasha tumelamba wenyewe tunafungwa sasa, inakuwaje?

Unataka kutuaminisha kwamba kanunu za BMK zimetungwa na Tundu Lisu,wakati ukweli ni kwamba yeye alikuwa miongoni mwa wajumbe wa kamati ya kutunga kanuni, kamati ambayo wajumbe wake wengi walikuwa makada wa CCM. Hata hivyo, yeye mmoja alijitahidi alivyoweza but alishindwa kwa wingi wa wajumbe wa CCM.
 
Kila siku tunasikia wanasiasa wakisema wananchi kwa sasa wako tayari kwa mageuzi lakini swali muhimu ni mageuzi ya aina gani ambayo wananchi wako tayari na wampe nani hayo mageuzi.

Mpaka pale wananchi watakaposema potelea mbali kama Mwl. Nyerere alivyosema mwaka 1995 lakini kwa sasa tutaendelea kuona hamasa kwenye mikutano ya kisiasa. Hamasa ni tofauti na kupiga kura.

Unapoona idadi ndogo ya wananchi wanajitokeza kwenda kupiga kura ukilinganisha na idadi ya waliojiandika, hiyo huwa ni dalili elekezi ya ushindi wa chama chochote kilichoko madarakani. Ukiona idadi ya wananchi wengi wanaenda kupiga kura kulinganisha na idadi ya waliojiandisha, hiyo huwa mara nyingi ni dalili elekezi ya ushindi wa wapinzani.

Wananchi wanaweza wakawa ni tayari kwa mageuzi lakini hawajapata mbadala wa kumkabidhi nchi kama chaguzi zilivyoonyesha!.

Watanzania wanaweza kuonekana kama wajinga lakini linapofika suala la kupiga kura huwa ni werevu ndiyo maana hata wale wamejiandikisha huwa wanaamua kubaki nyumbani siku ya kupiga kura baada ya kugundua hakuna mbadala wa kuwakabidhi nchi. Zimwi likujualo...!.

Ukiona kwa mfano madudu yanayojitokeza ndani ya repoti ya CAG unaweza ukadhani nchi haina viongozi.

Ni kazi ya vyama vya upinzani kuwaambia na kuwaaminisha wananchi kile ambacho watakifanya vizuri zaidi ya CCM badala ya kuwaona wananchi ni wajinga wakati wanategemea ridhaa ya wananchi kupewa madaraka.
 
Wanachoongea ni wagombea tu na ushabiki bila kueleza sera! Afya serambovu, elimu sera mbovu, bank sera mbove hata mfumo wa uchumi wa Tanzania haueleweki!. Inachukua miaka 3 hadi 4 kupata kibali cha kiwanja wakati una signature zote na una mpaka GPS map ya kiwanja, mikopo ya biashara ni zaidi ya 18% n.k sasa kama kweli una raisi mgombea mzuri aje atoe plan tuone.
 
Mhhhh!
HAKUNA ANAYEFANIKIWA KWA KUMSHUSHA ALIYE JUU! Huu mchezo wa kudhani ushindi unakuja kwa kunyooshea chama tawala vidole, hata sijui umetoka wapi na ni nani amedanganya kwamba hiyo ndio siri!
Wanaoendekeza siasa hizi wamesahau kabisa; la muhimu kwa wananchi ni SERA; sio bahati nasibu; na sio ujuzi wa kunyosheena vidole.
*Thread hii inazungumzia "Sera" mbovu za CCM! ...
Kweli? Zipo wapi sera "mbadala"?
Huwa ninasikiliza sana zile hotuba za "mawaziri vivulil"... Tafadhali nisaidie... ni lini umesikia waziri kivuli akitangaza sera "mbadala"? NI rahisi sana kupiga mawe kilichopo mezani! LAkini ukweli ni kwamba; hadi hapo wapinzani watakapoweka sera zao mezani? Maneno haya yote ni bure tu!
Dawa kamili ya "sera mbovu" ni kutoa sera "mbadala"; na kuhakikisha "sera hizo mbadala" zinafanyiwa kazi... kuanzia kwenye
halmashauri ambazo "wapinzani ndio watawala".
WEKENI SERA MBADALA, sera zinazoeleweka kirahisi, na tuonyesheni mfano wa mafanikio!
Leo ni February; IWAPO kwa miezi hii michache iliyobaki watu mtaendelea na siasa za kunyooshea "vidole"; na hakuna mawazo/sera mbadala... nadhani ni haki tu niseme "mjiandae kisaikolojia".
Peace!
 
Ukiona kwa mfano madudu yanayojitokeza ndani ya repoti ya CAG unaweza ukadhani nchi haina viongozi.

Ni kazi ya vyama vya upinzani kuwaambia na kuwaaminisha wananchi kile ambacho watakifanya vizuri zaidi ya CCM badala ya kuwaona wananchi ni wajinga wakati wanategemea ridhaa ya wananchi kupewa madaraka.

Ripoti ya CAG peke yake ingekuwa inatosha kuwafanya Watanzania waamue kuwaondoa watawala wao wa sasa. Tangu 2006 ripoti hiyo imekuwa ikitolewa hadharani na miye nilishaacha kuifuatilia hasa baada ya kuona kina Utouh wanarudia mambo yale yale katika mapendekezo yao miaka nenda miaka rudi huku kila wakienda kukagua wanakutana na madudu yale yale.

Hivi unajua ni mara ngapi CAG kapendekeza wabunge wasiteuliwe kuwa wajumbe wa bodi za Mashirika ya Umma? kwani wameachwa?
 
Mhhhh!
HAKUNA ANAYEFANIKIWA KWA KUMSHUSHA ALIYE JUU! Huu mchezo wa kudhani ushindi unakuja kwa kunyooshea chama tawala vidole, hata sijui umetoka wapi na ni nani amedanganya kwamba hiyo ndio siri!
Wanaoendekeza siasa hizi wamesahau kabisa; la muhimu kwa wananchi ni SERA; sio bahati nasibu; na sio ujuzi wa kunyosheena vidole.
*Thread hii inazungumzia "Sera" mbovu za CCM! ...
Kweli? Zipo wapi sera "mbadala"?
Huwa ninasikiliza sana zile hotuba za "mawaziri vivulil"... Tafadhali nisaidie... ni lini umesikia waziri kivuli akitangaza sera "mbadala"? NI rahisi sana kupiga mawe kilichopo mezani! LAkini ukweli ni kwamba; hadi hapo wapinzani watakapoweka sera zao mezani? Maneno haya yote ni bure tu!
Dawa kamili ya "sera mbovu" ni kutoa sera "mbadala"; na kuhakikisha "sera hizo mbadala" zinafanyiwa kazi... kuanzia kwenye
halmashauri ambazo "wapinzani ndio watawala".
WEKENI SERA MBADALA, sera zinazoeleweka kirahisi, na tuonyesheni mfano wa mafanikio!
Leo ni February; IWAPO kwa miezi hii michache iliyobaki watu mtaendelea na siasa za kunyooshea "vidole"; na hakuna mawazo/sera mbadala... nadhani ni haki tu niseme "mjiandae kisaikolojia".
Peace!

Kama unataka kusikiliza sera mbadala tafuta taarifa za kamati mbalimbali za bunge na mapendekezo. Nadhani kama ni kuunyoshewa kidole cyo kitu cha kusingiziwa uzii huu upo sawa kabisa. Mfano tuu wa kujiuliza; CCM ya enzi za mwalimu ukilinganisha na ya sasa utadhani ni vyama viwili tofauti!

Kuna mambo machache tuu ambayo ni ushahidi wa kushindwa kwa CCM; kitendo cha rais kutetea na kuudanganya wananchi hakuna fedha za umma kwenye escrow account, ni udhaifu wa chama ambacho yeye ni mwenyekti.

Kitendo cha serikali ya CCM kubadili baraza la mawaziri zaidi ya mara tatu ni ishara ya kushindwa kwa chama. Chama hakina utaratibu wa kuwajibishana ndo maana kila mtu aliyeko madarakani anataka apige hela akishtukiwa atahamishwa kituo cha kazi!

Sera mbovu zimekuwa ndo chanzo cha umasikini wa taifa. Mikataba ya uwekezaji ilitakiwa iwe wazi hata ikibidi iwepo tovuti ya mikataba ya serikali na wawekezaji. Mikataba kuwa siri imesababisha nchi kuendelea kuwa tegemezi na hata misaada na mikopo kwa vile ni siri inafaidisha wachache..........

..............To be continue ................
 
Mwanakijiji, Kikwete alikuwa na dhamira njema ya kuweka misingi imara ya kulipeleka taifa mbele, akaona aanze na kuandika katiba mpya kabisa, alichagua team makini ya akina warioba baregu salim. badae akaunda bunge la katiba lililojumuisha kila uwakilishi.

Alihakikisha watu makini wanapewa kutengeneza kanuni zitakazoongoza uendeshaji wa bunge la katiba, kazi hiyo akapewa mzee wetu Tundu Lissu, cha kushangaza akatunga kanuni mbovu na za hovyo kiasi kwamba hata yeye mwenyewe akashindwa kuzitumia, na baada ya kuona hilo basi akae kupambana angalau tuokoe chochote akabeba virago akatimua akabaki kununua viandishi vya habari vya kipuuzi na kumwandika kila gazeti.

Tunaweza inyoshea vidole ccm, tuseme ukweli miaka yote report ya CAG ilikuwa haiendi bungeni JK akaamuru ipelekwe bungeni na ijadiliwe kwa uwazi na wahusika wawajibike, badala yake tunageuza report zile kuwa sehemu ya kupigia fitina, sote tunajua biashara ya iptl ilikuwa ya nani lakini tukamshupalia muhongo kipumbavu tu, haya tunaondoa muhongo tunamweka simbachawene halafu tunajiona washindi "hovyo kabisa"

Nashindwa kuelewa tunamwondoa balozi kagasheki tunaweka nyalandu hivi kichwani zinatutosha kweli? haya mambo hayaendi na hatuna mtu wa kutukwamua gharasha tumelamba wenyewe tunafungwa sasa, inakuwaje?

JK alipokabidhiwa rasimu ya katiba mpya na tume ya Warioba alifanya nini?.Nani alimwondoa Kagasheki kwenye Uwaziri?Je unakiri kuwa IPTL/ESCROW ni ufisadi mwingine?Jibu hayo maswala achana na hizo blah blah zako nyingine.
 
Back
Top Bottom