kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Kuna mashirika ya Serikali kutokana na wajibu wake ni kama idara za Serikali. Yanatakiwa yagharamikiwe na hazina kuu. Yanafanywa mashirika ili kuweza kudhibiti matumizi na kwamba iwepo tija.
Ukitaka kugeuza TANESCO liwe la kibiashara moja kwa moja kwanza utapata muwekezaji gani? Lazima awe wa nje na atakua na nguvu gani ya kisiasa nchini? Yeye atataka faida tu na umeme ndio roho ya uchumi wa nchi.
Sisi tunamlenga nani kuhusu maendeleo? Raia wa kawaida au wawekezaji kutoka nje? Lazima umeme utakua bei mbaya kwa raia wapiga kura na ndio mfarakano utaanzia hapo.
Hii mambo ya kubinafsisha sijui asili mia 20 TANESCO ni ile ile habari ya kubinafsisha TTCL. Wajanja wakawagawia wahindi hisa za TTCL kwa bei ya bure wakati serikali ishawekeza mabilioni. Kisha wajanja kushirikiana na wahindi wakakwapua celltel kampuni ya TTCL ya simu za mikononi.
Ikawa wahindi wameshika jikoni TTCL wakikamua hela za umma kwa ruzuku za serikali eti ni wabia wa TTCL. Magufuli akaja kuwafukuza wahindi na kuirejesha kampuni yake ya mkononi kwa kuhakikisha serikali inapewa hisa stahiki.
Sio kila anayejidai ana uthubutu ana uwezo au nia nzuri. Mashirika kama TANESCO au TTCL sio ya kuwekwa sokoni kama njuku.
Wanaoweza kuyaendesha kwa kufikia malengo yake kwa nchi kama Tanzania hakuna. Ni watanzania gani utawashawishi kuwekeza tanesco?
Hivi unaweza mshawishi mtu awekeze kwa gereza. Gereza linaweza kua mradi wa kibiashara? ..sina hakika wala sijaona. Lakini si lazima magereza yawepo? Kuna mambo lazima yawe jukumu la serikali. Ndio maana kuna kodi.
Tukikubaliana na uhuni huu wa january na zitto akijidai mpendekezaji wa hoja tunaona yale ya TTCL, TRC, na ule mradi wa umeme wa makaa kule Songwe mbeya uhuni ule wa simon group kuhusu uda na kwingine.
La kufanyika ni uongozi imara wa kisiasa usiyokua na mchezo kudhibiti mashirika makubwa ya umma kuhakikisha hakuna ubadhirifu na inakwepo tija.