Tunaposikia ya Makamba na Zitto kutaka kubinafsisha TANESCO, tukumbuke yaliyofanyika TTCL

Tunaposikia ya Makamba na Zitto kutaka kubinafsisha TANESCO, tukumbuke yaliyofanyika TTCL

Kuna mashirika ya serikali kutokana na wajibu wake ni kama idara za serikali. Yanatakiwa yagharamikiwe na hazina kuu. Yanafanywa mashirika ili kuweza kudhibiti matumizi na kwamba iwepo tija.
Ukitaka kugeuza tanesco liwe la kibiashara moja kwa moja kwanza utapata muwekezaji gani? Lazima awe wa nje na atakua na nguvu gani ya kisiasa nchini? Yeye atataka faida tu na umeme ndio roho ya uchumi wa nchi. Sisi
Ni kawaida ya kila jamii kuwa na mtu anayesukumiwa mambo ya hovyo hovyo kuyasema au kuyafanya.Januari alikuwa akibeba boksi Amerika wakati Netgroup solution ya Afrika kusini ilipochukuwa TANESCO. Tatizo la mtu kama Januari ni la kielimu. Huwezi hata kujua ana digrii au diploma ya kitu gani. Huyo Zitto, yeye ni mpiga dili. Hapo wapo akina riziwani, na familia ya kikwete, tayari wamejiandaa kupiga dili, Zitto anaunga mkono.
 
Du kazi kweli kweli, haya mawazo ya kijamaa ndio yanayoturudisha nyuma. Mashirika mengi ya umma yalikufa haya kama TANESCO yameendelea kuwepo kwasababu tu yanapatiwa ruzuku serikalini ambayo ni kodi za wananchi tunalipia uzembe wote na wizi wote katika shirika hili. Dawa ya haya yote ni kilivunja shirika hili kuwa katika sehemu 3 au mbili generation and trasmission na distribution and collection of revenue. Yabinafsishwe kwa uwazi na kuzingatia sheria yunaweza kutafuta uzoefu kwenye mataifa mengine. Na kuweka vigezo vitakavyolinda maslahi ya Taifa kwa uwazi na kwa faida ya walaji. Generation ndio vital watupe ememe usio na kutetereka na penalt incase of default. mfano gas/ nuclear could be the cheapest source of power, sisi tumekimbilia water generation. Kurudi kwenye mashirika ya umma ni ngumu kumeza.
Kuna sehemu umesema uongo, umeme wa gas sio cheapest hata kidogo kulinganisha na umeme wa maji.
Mengine unaweza kuwa sawa
 
Chochote kilichobinafsishwa Kwa ufasaha kinafanya vizuri sana!!!...NBC,NMB,CRDB unajua kwanini umeme unaleta shida kila siku?.. Shirika hili la Tanesco halina mshindani ndio maana hata ufanisi ni sifuri!!!..Unajiuliza kwanini Taasisi kama hii ambayo ina vyuo vyake inashindwa kuwa na weledi kwenye kuhudumia wananchi?!!.. Tanesco lazima wabinafsishe tukitaka twende mbele lakini kama tutaendeleza huu utumbo hakika siku nchi itakua kiza yote na hakuna wakusema!!
Ok umesema shirika libinafsishwe na pawepo ushindani. Hebu ona hali itakayojitokeza kwenye usambazaji. Kila shirika na miundombinu yake. Hiyo dublication ya njia za umeme mijini na vijijini si itakua wastage? Kwa hiyo usambazaji kwanza lazima liwe shirika moja. Kama sio nchi zima iwe kwa kila eneo? Kuzalisha umeme tumefanya majaribio kubinafsisha. Kilichojitokeza ni mikataba ya ovyo ya kufilisi tanesco ambayo kwa hali halisi ndio wanunuzi ili wasambaze maana ndio wenye miundombinu. Magufuli akawafyeka wazalishaji wa mikataba mibaya ya kinyonyaji.
 
Ok umesema shirika libinafsishwe na pawepo ushindani. Hebu ona hali itakayojitokeza kwenye usambazaji. Kila shirika na miundombinu yake. Hiyo dublication ya njia za umeme mijini na vijijini si itakua wastage? Kwa hiyo usambazaji kwanza lazima liwe shirika moja. Kama sio nchi zima iwe kwa kila eneo? Kuzalisha umeme tumefanya majaribio kubinafsisha. Kilichojitokeza ni mikataba ya ovyo ya kufilisi tanesco ambayo kwa hali halisi ndio wanunuzi ila wasambaze maana ndio wenye miundombinu. Magufuli akawafyeka wazalishaji wa mikataba mibaya ya kinyonyaji.
Serikali kwendelea kuhodhi shirika hili ni kupoteza mapato na kushindwa kufika malengo yetu kama Nchi!!..unajua Shirika hili Lina madeni yasiyoweza kulipika?!!..Hebu Angali vyanzo vyetu vya umeme lakini bado tunanunua Kwa watu binafsi!!..
 
Du kazi kweli kweli, haya mawazo ya kijamaa ndio yanayoturudisha nyuma. Mashirika mengi ya umma yalikufa haya kama TANESCO yameendelea kuwepo kwasababu tu yanapatiwa ruzuku serikalini ambayo ni kodi za wananchi tunalipia uzembe wote na wizi wote katika shirika hili. Dawa ya haya yote ni kilivunja shirika hili kuwa katika sehemu 3 au mbili generation and trasmission na distribution and collection of revenue. Yabinafsishwe kwa uwazi na kuzingatia sheria yunaweza kutafuta uzoefu kwenye mataifa mengine. Na kuweka vigezo vitakavyolinda maslahi ya Taifa kwa uwazi na kwa faida ya walaji. Generation ndio vital watupe ememe usio na kutetereka na penalt incase of default. mfano gas/ nuclear could be the cheapest source of power, sisi tumekimbilia water generation. Kurudi kwenye mashirika ya umma ni ngumu kumeza.
Sio tunarudi nyuma. Tuliwahi binafsisha tanesco lini? Nilichosema kuna mashirika hayabinafsishiki. Kwanza huwezi kupata mtu wa kuyanunua kwa thamani yake halisi. Pili ni vigumu kama kupita tundu la sindano kupata muwekezaji atakayewekeza kwa malengo sera na mpango wa taifa. Sisi sera yetu ni kuleta maendeleo kwa umma wa wananchi.
 
Kuna sehemu umesema uongo, umeme wa gas sio cheapest hata kidogo kulinganisha na umeme wa maji.
Mengine unaweza kuwa sawa
Okay kwa kiasi nakubaliana na wewe ila ukiangalia kwenye issue ya environmemtal i.e. biodiversity , siltation nk. inaweza gharama kuwa ni kubwa
 
Rais Magufuli alipoliunda upya shirika la ndege na kufanya ndege kuwa za serikali na Air Tanzania kukodi ndege hizi ili wazifanyie biashara was very fine. Je shirika hili linaloiingizia Taifa hasara linawajibishwaje? Mimi nilifikiri approach could be any bidder could bid kuendesha Air Tanzania kibiashara kwa kutumia ndege za Serikali na kuilipa serikali kodi ya kukodi ndege and kulipa kodi ya biashara wanayoifanya kwenye faida zao.

Shirika la ndege la nchi ni huduma kama umeme, hospitali, magereza nk. Huwezi kusema hospitali zinazo toza tozo za huduma za afya zibinafsishwe kwa vile gharama za matibabu wanazo toza hazitoshi kuziendesha. Hivyo hivyo kwa magereza wana miradi ya uzalishaji huwezi sema ya binafsishwe kwa vile miradi yao haitoshelezi kukidhi gharama za uendeshaji wake.

ATCL inachotakiwa ni kujiendesha kwa tija ili ikidhi faida zake mtambuka kwa Watanzania. Moja ya faida mtambuka kwenye route yake ya Dar - Dom imeokoa mno kusambaratika kwa ndoa zilizo kumbwa na changamoto ya maamuzi ya serikaki kuhamia Dodoma kwa namna yalivyo tekelezwa.
 
Sio tunarudi nyuma. Tuliwahi binafsisha tanesco lini? Nilichosema kuna mashirika hayabinafsishiki. Kwanza huwezi kupata mtu wa kuyanunua kwa thamani yake halisi. Pili ni vigumu kama kupita tundu la sindano kupata muwekezaji atakayewekeza kwa malengo sera na mpango wa taifa. Sisi sera yetu ni kuleta maendeleo kwa umma wa wananchi.
Haya ni mawazo yako pia ni mazuri kwa kiasi fulani ila shorfall ni nyingi ndio maana nilipendekeza livunjwe ili libinafsishwe, ili kupata uwekezaji wenye technolojia ya kupunguza gharama kama kwenda kweny nuclear nk. Sasa hapa tulipo je ni management tu ndio shida? Au uwekezaji pia ndio shida? Tunawaumiza wananchi tu kwa kungangania kuendesha kila kitu. Niliona kwa wenzetu wamebinasfisisha raiway system kwenye wagons na serikali kuabaki na ile infrastructure na Shirika limeenda. British Airways ni shirika la serikali ila anaeliendesha ni watu binasfi nk. La msingi ni efficiency period.
 
Hawakupitisha kirahisi, na bado yale maamuzi yao yaliwagharimu hata wao walianza kuwa na hofu na maamuzi yao ya hovyo, kwani walianikwa.
Hhakuna wanachoshindwa, watatumia hadi jeshi kupitisha wanachotaka
Unakumbuka wakati wa JK, pamoja na akina Lissu na lema kupinga sana mikataba ya gesi bado CCM waliipitisha usikuusiku kwa hati ya dharura.
 
Chochote kilichobinafsishwa Kwa ufasaha kinafanya vizuri sana!!!...NBC,NMB,CRDB unajua kwanini umeme unaleta shida kila siku?.. Shirika hili la Tanesco halina mshindani ndio maana hata ufanisi ni sifuri!!!..Unajiuliza kwanini Taasisi kama hii ambayo ina vyuo vyake inashindwa kuwa na weledi kwenye kuhudumia wananchi?!!.. Tanesco lazima wabinafsishe tukitaka twende mbele lakini kama tutaendeleza huu utumbo hakika siku nchi itakua kiza yote na hakuna wakusema!!
Ni umakini wa usimamizi tu! KAma ni ubinafsishaji wa umeme, sijui uliuona nchi gani na inafanya vizuri? KInachoruhusiwa duniani kote ni wazalishaji binfasi kuiuzia TANESCO umeme. Wazalishaji wenye akili siyo hao akina Singh na Rugemalira na IPTL yao. Tatizo kubwa la Afrika ni pale tunapokuwa na rais mwizi. Jiulize nani atasimamia raslimali zeru kama rais naye anageuka kuwa mwizi? Ndo maana unaona ushujaa wa akina Januari, wanafahamu tabia ya boss wao.
 
Nadhani hata hujui unataka kuongea nini shirika la umeme Zambia unajua linaongozwa je?..Je kule Uganda na Kenya umeona utofauti na hili la kwetu?!!..Ndio maana tunasema atafutwe Partner hapo!!..Hawa wazalendo unaosema for more than 30 years bado tuna shida ya umeme!!...
 
Nchi ya kikwete ndugu hii yeye akiamua hakuna kinachoshibdikana
 
Back
Top Bottom