Tunaposikia ya Makamba na Zitto kutaka kubinafsisha TANESCO, tukumbuke yaliyofanyika TTCL

Tunaposikia ya Makamba na Zitto kutaka kubinafsisha TANESCO, tukumbuke yaliyofanyika TTCL

Kuna mashirika ya Serikali kutokana na wajibu wake ni kama idara za Serikali. Yanatakiwa yagharamikiwe na hazina kuu. Yanafanywa mashirika ili kuweza kudhibiti matumizi na kwamba iwepo tija.

Ukitaka kugeuza TANESCO liwe la kibiashara moja kwa moja kwanza utapata muwekezaji gani? Lazima awe wa nje na atakua na nguvu gani ya kisiasa nchini? Yeye atataka faida tu na umeme ndio roho ya uchumi wa nchi.

Sisi tunamlenga nani kuhusu maendeleo? Raia wa kawaida au wawekezaji kutoka nje? Lazima umeme utakua bei mbaya kwa raia wapiga kura na ndio mfarakano utaanzia hapo.

Hii mambo ya kubinafsisha sijui asili mia 20 TANESCO ni ile ile habari ya kubinafsisha TTCL. Wajanja wakawagawia wahindi hisa za TTCL kwa bei ya bure wakati Serikali ishawekeza mabilioni. Kisha wajanja kushirikiana na wahindi wakakwapua celltel kampuni ya TTCL ya simu za mikononi.

Ikawa wahindi wameshika jikoni TTCL wakikamua hela za umma kwa ruzuku za Serikali eti ni wabia wa TTCL. Magufuli akaja kuwafukuza wahindi na kuirejesha kampuni yake ya mkononi kwa kuhakikisha serikali inapewa hisa stahiki.

Sio kila anayejidai ana uthubutu ana uwezo au nia nzuri. Mashirika kama TANESCO au TTCL sio ya kuwekwa sokoni kama njuku.

Wanaoweza kuyaendesha kwa kufikia malengo yake kwa nchi kama Tanzania hakuna. Ni watanzania gani utawashawishi kuwekeza tanesco?

Hivi unaweza mshawishi mtu awekeze kwa gereza. Gereza linaweza kua mradi wa kibiashara? ..sina hakika wala sijaona. Lakini si lazima magereza yawepo? Kuna mambo lazima yawe jukumu la serikali. Ndio maana kuna kodi.

Tukikubaliana na uhuni huu wa january na zitto akijidai mpendekezaji wa hoja tunaona yale ya TTCL na ule mradi wa umeme wa makaa kule Songwe mbeya uhuni ule wa simon group kuhusu uda na kwingine.

La kufanyika ni uongozi imara wa kisiasa usiyokua na mchezo kudhibiti mashirika makubwa ya umma kuhakikisha hakuna ubadhirifu na inakwepo tija.
Rugemalira si yupo?
 
Chochote kilichobinafsishwa Kwa ufasaha kinafanya vizuri sana!!!...NBC,NMB,CRDB unajua kwanini umeme unaleta shida kila siku?.. Shirika hili la Tanesco halina mshindani ndio maana hata ufanisi ni sifuri!!!..Unajiuliza kwanini Taasisi kama hii ambayo ina vyuo vyake inashindwa kuwa na weledi kwenye kuhudumia wananchi?!!.. Tanesco lazima wabinafsishe tukitaka twende mbele lakini kama tutaendeleza huu utumbo hakika siku nchi itakua kiza yote na hakuna wakusema!!
Tatizo la Tanesco ni kuwa linaendeshwa kisiasa zaidi. Fikiria gharama za kuunganisha umeme za Tzs 27,000 kwenye kibanda chenye kuwasha bulb moja au mbili. Hizo gharama zitarudi baada ya karne ngapi?
 
Tatizo ni monopoly ya TANESCO hawana mshindani na uwajibikaji zero wanaishi na kuiba kwa ruzuku za serikali, waruhusu sekta binafsi zifanye biashara ya umeme sio uzalishe na uwauzie TANESCO kwa bei wanayotaka wao, turuhusu uzalishaji na usambazaji kwa sekta binafsi na serikali kama inatka kusaidia iwape ruzuku wananchi wanaotumia huduma
 
Hivi kwanini tusiruhusu mashirika huru ya umeme kuanzishwa ili kuondokana na tatizo la umeme nchini?
maana kiukweli TANESCO ni wamezidiwa ile mbaya.
Mkuu Tanesco haijazidiwa, ila Serikali ndo wamezidiwa,tena uhai wa kama aslimia 10 wa tanesco nimeona ndani ya 5yrs.
Ukiwa nashida walikuwa wanawahi sana lakini hili shirika utapeli wa wafanyakazi na rushwa,maana ukifuata utaratibu kujakupata umeme urasota sana. Serikali waje na mpango kabambe wakuliwezesha shirika,
Kumbuka tanesco wanatoa huduma na siyo beneficially oriented,ndo maana linapewa ruzuku na serikali.
 
Serikali kwendelea kuhodhi shirika hili ni kupoteza mapato na kushindwa kufika malengo yetu kama Nchi!!..unajua Shirika hili Lina madeni yasiyoweza kulipika?!!..Hebu Angali vyanzo vyetu vya umeme lakini bado tunanunua Kwa watu binafsi!!..
Vyanzo ni srikali anawajibika siyo shirika,ndo maana wanajenga vyanzo.
 
kmbwembwe TANESCO lazima ibinafsishwe ili kuongeza ufanisi na sio lazima gharama za umeme zipande sababu ya ubinafsishwaji.

Hivi sasa Tanesco inapoteza mapato mengi sana kwa sababu kadha wa kadha ambazo zinazuilika na ufanisi wake ni almost sifuri. Tanesco wanaona kawaida sababu serikali bails them out everytime, ubinafsishaji utaongeza uwajibikaji.

Aidha kuna magereza ya biashara tembea ujionee au jisomee online. US ina magereza kibao tu for profit.
 
Huku Marekani uzalishaji na usambazaji wa umeme unafanywa na makampuni binafsi...

Serikali haina kampuni hata moja

Serikali yaani FBI na CIA wanasimamia sheria,hakuna economic crime inapita bila kua detected na watu kufungwa inavyotakiwa

Tatizo mnaacha kazi zenu hasa za CIA na FBI mmegeukia kazi zisizo zenu za kufanya "biashara"....

Yaani unaacha kazi yako,unavamia kazi usioijua ya "biashara"..lazima ufeli na kupigwa tako kama inavyotakiwa!
Mkuu kwa katiba hii na sheria hizi tukibinafisisha sijui usimamizi utakuwa je. Maana upigaji bongo ni mwingi sana.
 
kumbuka dunia inapokwenda inaenda wapi......lau tungebaki na ttcl yetu je izi smartphone tungekuwa nazo leo hii
Wa kwetu let me tell you mitambo ya buzz na celtel(celnet) ilinunuliwa na ttcl na sera za kijinga za ubinafsishaji mitambo hiyo wakapewa mobitel na celtel.Kwa hiyo hata bila kuuza tanesco we can do it.Kinachotakiwa ni akili kubwa
 
kmbwembwe TANESCO lazima ibinafsishwe ili kuongeza ufanisi na sio lazima gharama za umeme zipande sababu ya ubinafsishwaji.

Hivi sasa Tanesco inapoteza mapato mengi sana kwa sababu kadha wa kadha ambazo zinazuilika na ufanisi wake ni almost sifuri. Tanesco wanaona kawaida sababu serikali bails them out everytime, ubinafsishaji utaongeza uwajibikaji.

Aidha kuna magereza ya biashara tembea ujionee au jisomee online. US ina magereza kibao tu for profit.
Lakn serikali na mashirika mengine ya umma ndo wadaiwa sugu wa mabilioni ya bill za umeme. Lakini wasiwasi mkubwa ni ukiritimba wa kubinafisisha maana kuna kuwini au kuumia kwa katiba na sheria hizi zilizopo, maana watu wanamifano ya huko nyuma ndani ya tanesco.
Na viongozi wa serikali ndo wanalazimisha shirika kuingia mikataba mibovu kwa masirahi ya wanasiasa.
 
I hear your concerns.

Mashirika kama CRDB, NBC yalifufuka sababu ya ubinafsishwaji.

Serikali na hayo mashirika mengine hawalipi sababu wanaiona Tanesco kama mwenzao, washika dau hawawezi vumilia huu upuuzi kama likibinafsishwa.

Tanesco inapoteza karibu 16% ya umeme wote inaozalisha, hii haikubaliki hata kidogo ila wao wanaona kawaida. Ndo maana tunasema ubinafsishwaji utaongeza ufanisi.

Kuingia mikataba mibovu is a different story ila kwanza tukubaliane kwamba inabidi Tanesco ibinafsishwe.
 
Zito ni starter kwenye gari hivyo ujue katumwa kuwasha gari engine ikopokea yeye hana kazi tena fikiria ikipelekwa mswada bungeni wa kuuza his za tannesco utafanyaje kwenye bunge hili ndiyo maana tunataka katiba mpya,wananch tukichagua viongozi wapewe uongozi wasifanyiwe fitina naserikali kuwaapisha waliopendwa na rais.
Du. Wewe noma. Umepamtia kweli kweli huyu jamaa. Ni starter ya gari kweli kweli. Ametumwa kuanzisha.
 
Nchi ya watu zaidi ya millioni 60 kwa nini tuwe na shirika moja umeme huduma ambayo ni muhimu sana katika maisha na uchumi wa nchi, serikali kwa ruzuku zake na TANESCO hawana uwezo wa kuhudumia nchi nzima, tuache sekta binafsi iingie ifanye kazi ya uzalishaji na usambazaji, cha muhimu tuweke utaratibu mzuri tuu tupate umeme na wao wapate faida zao, tuache ujinga
 
Acha roho hii ya kipumbavu namna hii

Weka sheria,zisimamie kwa roho moja,ndio kazi yako

Then privatize kila kitu kwa watu binafsi wawe wa ndani au wa nje,privatize!

Wewe simamia sheria kama FBI au CIA

Ndio kazi yako,mengine ya biashara waachie watu binafsi

Na hii roho ya kipumbavu ya kupenda vitu vya bure au vilivyopoozwa kwa kodi za serikali ni upumbavu na umasikini mwingine wa kujidanganya

Kila kitu unalipiwa ndio maana unatawaliwa kidikteta na kua treated kama hayawani na serikali maana huna utu na sense of kujitegemea na ku-think and do for yourself...Kila kitu unategemea huruma ya wanasiasa serikalini,na wananchi wote mnakua treated kama watoto msiojua lolote
Kuna nchi nyingi tu serikali zinamiliki makampuni na mashirika na yanafanya vizuri. Tanzania kubinafsisha shirika kama Tanesco siyo wazo zuri. Libaki kuwa serikalini.
 
Chochote kilichobinafsishwa Kwa ufasaha kinafanya vizuri sana!!!...NBC,NMB,CRDB unajua kwanini umeme unaleta shida kila siku?.. Shirika hili la Tanesco halina mshindani ndio maana hata ufanisi ni sifuri!!!..Unajiuliza kwanini Taasisi kama hii ambayo ina vyuo vyake inashindwa kuwa na weledi kwenye kuhudumia wananchi?!!.. Tanesco lazima wabinafsishe tukitaka twende mbele lakini kama tutaendeleza huu utumbo hakika siku nchi itakua kiza yote na hakuna wakusema!!
Hii ni monopoly marketing.

Supplier anahodhi vyanzo vyote vya uzalishaji wa nishati, tukiruhusu ubinafsishaji umeme utakuwa bei juu sana.

Hakuna mbia atakayeuza umeme wa bei nafuu kuliko Tanesco.

Muhimu ni kuboresha shirika,kuziba mianya inayopwaya.
 
Nchi ya watu zaidi ya millioni 60 kwa nini tuwe na shirika moja umeme huduma ambayo ni muhimu sana katika maisha na uchumi wa nchi, serikali kwa ruzuku zake na TANESCO hawana uwezo wa kuhudumia nchi nzima, tuache sekta binafsi iingie ifanye kazi ya uzalishaji na usambazaji, cha muhimu tuweke utaratibu mzuri tuu tupate umeme na wao wapate faida zao, tuache ujinga
Pengine mwenye kufikiria kubinafsisha shirika kama Tanesco ndiye anatakiwa aache ujinga. Najua kama kawaida ya wabongo kutotafakari na kuangalia mambo kwa kina ndiyo utamaduni wetu.
 
Hii ni monopoly marketing.

Supplier anahodhi vyanzo vyote vya uzalishaji wa nishati, tukiruhusu ubinafsishaji umeme utakuwa bei juu sana.

Hakuna mbia atakayeuza umeme wa bei nafuu kuliko Tanesco.

Muhimu ni kuboresha shirika,kuziba mianya inayopwaya.
Sasa mbona Tanesco anauziwa Umeme au mimi sielewi?...kama Tanesco anauziwa umeme alafu anauza kwetu!!!..Alafu unasema hawa watu binafsi watatuuzia bei juu!!!..Hebu tafakari kidogo nadhani hujui hata shirika letu linauziwa umeme na kutuuzia sisi
 
Hii ni monopoly marketing.

Supplier anahodhi vyanzo vyote vya uzalishaji wa nishati, tukiruhusu ubinafsishaji umeme utakuwa bei juu sana.

Hakuna mbia atakayeuza umeme wa bei nafuu kuliko Tanesco.

Muhimu ni kuboresha shirika,kuziba mianya inayopwaya.
Hebu Fikiria kama tusinge binafsisha TBL au TCC hata hizi NBC,NMB na CRDB unadhani tungekua wapi?!!...Najua mnaogopa kupoteza ajira nyingi ambazo mlikua mnapata bila vigezo lakini tukitaka Tanesco ijiendeshe Kwa ufanisi na kupata Faida Partner ni muhimu
 
Back
Top Bottom