Tunapoufikia ukomo

Tunapoufikia ukomo

Mbepo yamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2012
Posts
1,262
Reaction score
1,773
Ndugu wanabodi heshima yenu nyote.

Awali ya yote mimi siyo mzima kiafya ya akili mpaka muda huu. Ninajiona kabisa endapo sintafanikiwa kwenye hili basi mwaka huu hautoisha kabla sijalala umauti.

Iko hivi,.

Nilikuwa mfanyakazi wa kampuni moja ya genera supply hapa jijini Dar nikiwa kama muandaaji wa tender documents kuomba kazi zote ambazo kampuni imekuwa ikifanya. Mwaka jana mwezi wa tisa niliomba kuacha kazi kwenye hiyo kampuni kwa sababu niliamini naweza kusimama mwenyewe.

Ni kweli kwa kazi za pale niliweza kununua shamba kubwa tuu wilaya ya Chunya karibu ekari 140 na nikapambana nikazikatia hatimiliki.
Nililitegemea shamba kama mtaji wangu wa kwanza kwa sababu kuna miti ya kutosha niliyoona ni faida kuzalisha mkaa.

Kweli nilichoma mkaa kwa mara ya kwanza na kuupeleka mbeya. Kwa kuwa haikuwa ni field yangu ya ufanisi nilijikuta nimekosea ujazo kwenye mifuko na ubora wa mkaa kwa maana kwa kiasi kikubwa sikuchambua chenga na mabonge. Ukanisumbua sana sokoni na ulinikata mtaji.

Kuona hivyo nikajaribu kuunganisha nguvu kwa watu kuomba wanisaidie mtaji kwa njia ya ubia wa biashara. Nilipata stoo Dar Kijitonyama nikailipia. Nikaenda kuandaa mzigo Chunya na kuuleta.

Hapo nikaja kukutana na maluweluwe ya ajabu sana. Niliuza ule mkaa na hela haikuonekana. Yaani nauza mkaa madebe ya kutoa laki na ishirini na naikusanya hiyo hela halafu najikuta nimebaki na elfu thelathini pekee.

Nilikatika vibaya sana kuliko nilipofanyia biashara Mbeya.

Kimbembe kikawa hela ya watu. Tena wengine ni classmates wangu ambao najua wataisoma hii thread na wataijadili kwenye group.

Nilionekana tapeli na mwizi. Na mpaka leo hii hiyo ndo image waliyo nayo kwangu.

Biashara ya gunia 180 za mkaa niliambulia milioni tatu na nusu pekee. Yaani ilitoka hela ya kulipia usafiri tuu ikaisha.

Pengine kama ningekuwa nimetumbua na mke wangu au mama yangu au hata mchepuko (ambaye hata hivyo sina) ningeeleweka kirahisi. Ila nilipiga flash kabisa ile awamu.

Mwezi May mwaka huu mama mkwe wangu akanisaidia fedha ya mtaji niende Zambia nikafanye biashara ya soya na mahindi. Ukweli ni kuwa ile hela alikopa tuu na yeye tena kwenye taasisi ya fedha.

Nimeenda kule. Awali biashara ilienda sawa na mtaji ukaanza kukua. Mara likatokea tatizo kule. Passport yangu hairuhusu kufanya biashara ila nikaonekana nafanya biashara. Nilipoteza gari ya mahindi ya tani 30 kwa kosa hilo. Na ni hela ya mkopo. Tena mama mkwe.

Aisee nikahangaika sana mpka kupika kachori na kuwauzia wazambia wasozijua ili ninunue mahindi hata kwa kudunduliza.

Nikakusanya kiasi cha tani 20. Kasheshe ikawa kutoka na mzigo kule kuja nao maana nilikuwa nimeshakaa kule mpaka pass ikaexpire kwa miezi minne mbele ya muda unaoruhusiwa.

Pia biashara ya kachori ikafa maana kwa mwezi November na December watu wanapotelea mashambani.

Nimerudi nikate passport na kufanya namna niweze kwenda kukomboa huo mzigo ila Bongo nako ndo kugumu balaa.

Kasheshe ni kuwa kwenda kumuona mkwe napata ugumu kwa haya nilopitia maana naye aliposikia nimerudi tuu anataka nimuone na hela kiasi chochote ambapo kweli mimi sina.

Nimefikiria niliuze shamba hata kwa hasara ili nikamilishe huu mchakato mapema ndo solution ya mwisho kabla sijajiua.

Shamba la ekari 140 ninaliuza kwa milioni kumi na mbili pekee. Ni shamba lenye hati kabisa na kwa kweli muda wa mauzo ni sasa ili nikwamuke na huu mkwamo.
 
Sir, Uza vyote ila usiuze ardhi yako yote kwa hasara. Na kifo sio suluhisho utakua umecheat maisha.
2Pac anasema kama usiku ni wa giza nene basi jua linakaribia kuchomoza!
Mkuu nahitaji nikakomboe mzigo Zambia ili nilipe huku kwa mkwe niwe na amani. Na kuuza kwa bei ya faida naona itakuwa ngumu kumpata mteja kwa haraka
 
Pole sana sana nashauri pita kwenye mabenki kama uko dar tafuta vijana wa kichaga watachukua hio Shamba fasta hautajuta fasta sana au omba page za celebrities kama lemutuz na wengineo weka tangazo fupi sana, au mpigie lemutuz akusaidie kupata wadau
 
Najua kuna wakinga pale makongorosi ambao wanaweza kununua ninawafahamu ila Bora utangaze mwenyewe hio biashara.
 
Pole sana sana nashauri pita kwenye mabenki kama uko dar tafuta vijana wa kichaga watachukua hio Shamba fasta hautajuta fasta sana au omba page za celebrities kama lemutuz na wengineo weka tangazo fupi sana, au mpigie lemutuz akusaidie kupata wadau
Asante mkuu. Kweli umenipa angle ambayo sikuiona. Nitalifanyia kazi kesho tuu kukikucha
 
Mkuu nahitaji nikakomboe mzigo Zambia ili nilipe huku kwa mkwe niwe na amani. Na kuuza kwa bei ya faida naona itakuwa ngumu kumpata mteja kwa haraka
Sir, You appear to be dying for having a death wish! I will make effort to prevent this but can promise nothing!

"You gotta find a way to survive coz they win when your soul die"
-2Pac
 
Sir, You appear to be dying for having a death wish! I will make effort to prevent this but can promise nothing!

"You gotta find a way to survive coz they win when your soul die"
-2Pac
Nimekosa emoji ya kushukuru mkuu. Asante sana
 
Mwanangu wewe fighter sana unahitaji coaching kidogo tu ili utoboe, lazima uwe na kinga lazima nyota inghae kwenye private life hasa upambanaji usiruhusu ngedere wakusumbue. Lazima uwe mnyama sana sana, pambana Kwanza piga hatua kidogo then uje inbox ntakupa mchongo. Game la private sio maigizo mepesi lazima uwe solid na compact kwenye game mwanzo mwisho. Dadeki ndio life
 
Mwanangu wewe fighter sana unahitaji coaching kidogo tu ili utoboe, lazima uwe na kinga lazima nyota inghae kwenye private life hasa upambanaji usiruhusu ngedere wakusumbue. Lazima uwe mnyama sana sana, pambana Kwanza piga hatua kidogo then uje inbox ntakupa mchongo. Game la private sio maigizo mepesi lazima uwe solid na compact kwenye game mwanzo mwisho. Dadeki ndio life
Kweli eenh? Wewe ni mtu wa ngapi sijui ukizungumzia suala la nyota. Ila kuhusu kujiweka sawa unanipa insight mpya. Gemu ngumu nakujia hata pm tuyajenge. Im still young with ambition
 
Ukiuza Shamba usifanye kosa ukaenda bila kujiweka sawa kwenda Zambia lazima uondoe nuksi na ujinga wote walokupa washenzi kwenye nyota yako, maana hapo tayari upo kwenye mufilisi kwenye nyota be careful, na wala sio lazima nikusaidie mimi , mi naplay role yangu kukufungua akili kama msamalia mwema
 
Ukiuza Shamba usifanye kosa ukaenda bila kujiweka sawa kwenda Zambia lazima uondoe nuksi na ujinga wote walokupa washenzi kwenye nyota yako, maana hapo tayari upo kwenye mufilisi kwenye nyota be careful, na wala sio lazima nikusaidie mimi , mi naplay role yangu kufungua akili kama msamalia

Je nuksi haiwezi kuchelewesha kuuza shamba?
 
Baharia usione nakupa ushauri na dondoo tumepitia mengi zaidi yako na wengine sasa tuna roho za kinyama hatukaribishi nzi au kupe kwenye maisha yetu. Acha uoga na hofu next year unatusua maisha
 
Wewe ni kwamba umefikia kiwango cha mwisho cha kufikiria ndio suluhisho pekee ni kujiua

Kujiua nakataa mzee baba wali ulivyo mtamu sijui tambi unaachaje vitamu hivi

Tafuta rafiki ama ndugu yako wa karibu sana muelezee ili yakutoke moyoni
inaonekana moyoni mwako kuna mengi ambayo rafiki/ndugu zako hawayajui zaidi ya kutuandikia sisi
 
Back
Top Bottom