Tuna tatizo kubwa la kimkakati linaloanzia kwenye Taifa mpaka hizi ngazi za chini kiuongozi, huwezi kuamini kuna watu ni viongozi miaka rudi nenda na bado ukifika uchaguzi wanachaguliwa tena ili hali hakuna walichofanya muda wao wa uongozi,.
Ili tuweze kusonga mbele tunatakiwa kuwa na shule za michezo kuanzia primary na kuendelea hapo tunaweza kupiga hatua. Yaani kwasasa viongozi wapo ofisini wakisubiri mtu ajitume mwenyewe afanye mazoezi aonekene na wadau kisha wao ndio wanaenda kumdandia na kumpeleka kwenye mashindano.