Tunapozidiwa hadi na nchi zenye watu laki 3 kwenye Olympics

Tunapozidiwa hadi na nchi zenye watu laki 3 kwenye Olympics

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Wale wanaofatilia Olympics wataona kuna nchi kama Bahamas ina Wanamichezo wengi kwenye hii Olympics kuliko sisi. Cha ajabu idadi ya watu huko Bahamas ni laki tatu tu. Sisi wenye milioni 60 tunashindwaje?

Jamaica idadi ya watu milioni 3 tu kama nusu ya wakazi wa Dar. Ajabu wana wanamichezo wengi sana kutuzidi.

Hivi kweli Taifa la watu milioni 60 haya warussha tufe Tu hatuna?

Nchi kama Botswana..Qatar..zimetushinda?

Uganda , Namibia?..

Waziri wa michezo anafanya shughuli gani?
 
Muda mwingi tunautumia kwenye siasa
Fikiria saa hii watu wako Space, kesho wako hoi unategemea nini, tunaishi kwa ujanja ujanja tu, kuiba zilizopo bila kuzizalisha
 
Kwa huu mfuma wa utezi wa alpha ,gama,beta radiation unazani tutafika kweli. Fadhila
 
Michezo mashuleni ilianza kwisha pindi majizi yalipouza viwanja vya michezo

Michezo mingi tulikuwa tunacheza shuleni miaka ya 70 mpaka 80 ingawa hatukushiriki sana Olympic

Wakulaumiwa ni wabunge wanaokaa tu na kula pesa za bure na kuongea utumbo tu
Bajeti inaenda wapi?
Nani wa kumhoji maana pesa kama hizo zipo ila zinaliwa tu

Kweli Taifa kubwa hivi hata bendera yetu wenyewe tumebebewa
 
Kanuni ya uongozi inaainisha kuwa siasa ikiwa mbovu kila kitu kitakuwa kibovu,na ndo haya yanayotokea nchini kwetu
 
Kipaumbele chetu sio michezo, hyo ni ziada tu.
Fuatilia hata kwenye bajet michezo ipo ili mradi tu, haiangaliwi kama sekta muhimu kama chanzo cha hajira kwa vijana.
 
Kila mafanikio yanahitaji uwekezaji, China wana shule za kufundisha watoto michezo kuanzia miaka mitano. Waliwekeza katika hili baada ya kugundua gold medals kwenye mashindano ni tija kwa Taifa.
 
Huwezi kuwa bora kwenye kila kitu, Marekani na umwamba wake wote ule lakini football team yao sio kali kivile
 
Tuna tatizo kubwa la kimkakati linaloanzia kwenye Taifa mpaka hizi ngazi za chini kiuongozi, huwezi kuamini kuna watu ni viongozi miaka rudi nenda na bado ukifika uchaguzi wanachaguliwa tena ili hali hakuna walichofanya muda wao wa uongozi,.
Ili tuweze kusonga mbele tunatakiwa kuwa na shule za michezo kuanzia primary na kuendelea hapo tunaweza kupiga hatua. Yaani kwasasa viongozi wapo ofisini wakisubiri mtu ajitume mwenyewe afanye mazoezi aonekene na wadau kisha wao ndio wanaenda kumdandia na kumpeleka kwenye mashindano.
 
Back
Top Bottom