Mimi sioni mapinduzi ya aina yeyote ya kilimo. Kama Taifa iliweka lengo mathalani pamba kuwa mwaka 2024 Taifa litazalisha marobota 750,000 lakini cha ajabu uzalishaji 2024 hautafika hata marobota 50,000. Nenda vijijini uone wakulima wanavyolima hovyo hovyo hakuna cha maelekezo ya Maafisa ugani. Shamba ekari moja la mahindi mkulima anatoa gunia 4. Shamba ekari moja la mpunga mkulima anatoa gunia 3. Mapinduzi gani ya kilimo wanayotuambia.