Tunashukuru kwa Ushindi wa Goli 3 kwa 0, ila tungeacha Upuuzi, Utoto na kutokuwa Makini tungeshinda hata Goli 8 za uhakika

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Japo ni mwana Simba SC lia lia ila kwanini nawapenda Yanga SC ( hasa Kiuchezaji ) ni kwamba Wachezaji wao hata kama wameshinda lakini muda Wote wa Mchezo wanakuwa very committed kutaka Ushindi zaidi na Wanahamasishana muda wote na Umakini ukiwa ni wa hali ya juu na kamwe hawabweteki tofauti na ilivyo kwa Simba SC yangu.

Simba SC nawaonya msije Kuthubutu Kucheza mpira ule mbovu ( japo tumeshinda Goli 3 jana dhidi ya Timu ya Mkoani Kwangu Mara ) ya Biashara United FC tukicheza na Yanga SC hii iliyokamilika kwa Kuna uwezekano wa hata tukapigwa Goli Kumi ( 10 ) huku 'Mtetemaji' Fiston Kalala Mayele 'akitetema' peke yake mara Saba ( 7 )

Yaani Uwanja mzuri wa Mkapa tunacheza vibaya vile je, tukienda tena Viwanja vibovu vya huko Mikoani itakuwaje? Sijafurahishwa na Ushindi wa Goli zile Tatu ( 3 ) za Jana kwani Uwezo wa Kuwafunga hata Goli 8 ulikuwepo kama Wachezaji wetu wa Simba SC wangejitambua na kuwa makini.
 
Hata mimi nimeshangaa, half time nimeacha 3-0 sijaangalia tena kurudi baada ya mpira kwisha naona bado 3-0 ile ile, game kama ile ya jana ndio nzuri kujenga confidence ya wachezaji, piga mtu zakutosha kama akilegea mbele yako.
 
Simba wana match nyingi na muhimu sana hawahitaji kutumia nguvu nyingiiii huku wakijua kazi imeisha... utopolo lazima watumie migivu wakati wote kwa sabbu na wana cha kupoteza akili yao yote ipo NBC tu..
 
Japo ni mwana Simba SC lia lia ila kwanini nawapenda Yanga SC ( hasa Kiuchezaji ) ni kwamba Wachezaji wao hata kama wameshinda lakini muda Wote wa Mchezo wanakuwa very committed kutaka Ushindi zaidi na Wanahamasishana muda wote na Umakini ukiwa ni wa hali ya juu na kamwe hawabweteki tofauti na ilivyo kwa Simba SC yangu.

Simba SC nawaonya msije Kuthubutu Kucheza mpira ule mbovu ( japo tumeshinda Goli 3 jana dhidi ya Timu ya Mkoani Kwangu Mara ) ya Biashara United FC tukicheza na Yanga SC hii iliyokamilika kwa Kuna uwezekano wa hata tukapigwa Goli Kumi ( 10 ) huku 'Mtetemaji' Fiston Kalala Mayele 'akitetema' peke yake mara Saba ( 7 )

Yaani Uwanja mzuri wa Mkapa tunacheza vibaya vile je, tukienda tena Viwanja vibovu vya huko Mikoani itakuwaje? Sijafurahishwa na Ushindi wa Goli zile Tatu ( 3 ) za Jana kwani Uwezo wa Kuwafunga hata Goli 8 ulikuwepo kama Wachezaji wetu wa Simba SC wangejitambua na kuwa makini.
Ni kweli kabisa Mkuu, ila kikubwa tumechukua point tatu.

Simba Nguvu Moja
 
Hao akina Mayele waliifunga ngapi biashara hapo kwa Mkapa?
 
Back
Top Bottom