Tunashukuru lakini si haki: Kuitwa kwenye usaili kwa majina ya nyongeza na tume ya ajira

Tunashukuru lakini si haki: Kuitwa kwenye usaili kwa majina ya nyongeza na tume ya ajira

Wewe ni fala, sisi tulikuwa tunaenda kwenye interviews kwa ghafla. Unaweza kukurupushwa kwa Interview toka Lindi huko interview kesho saa 4 unapanda gari unatembea usiku kwa usiku.

Unapanda hata gari za ndizi mradi ufike kwenye panel mkoa mwengine zaidi ya kilometre 650.

We umepewa siku tatu. Halafu nikwambie tu kutoboa ni bahati. Kama huna hata ukipewa taarifa miezi miwili nyuma hutoboiii
Tunazungumzia logic ya kuweka uwanja sawa kwa wasailiwa wote na si vinginevyo. Jadili kama kwa mazingira haya uwanja uko sawa kwa wote? Je ni haki uwanja usiwe sawa kwa wasailiwa wote? Hiyo ndiyo hoja iliyopo kwenye uzi huu. Ukitaka kuongea vingine ni sawa lakini vifungulie uzi mwingine!!
 
Mbona unaanza kulalamika mapema siku tatu kujiandaa kwa kada yako bado ni nyingi piga msuli kama unaenda kwenye mtihani wa taifa yaani ni mchana na usiku na tusikuone humu hadi baada ya usaili
Kwa taarifa yako mimi si kijana, wala si miongoni wa waombaji wa ajira. Ila mimi ni mtanzania mzalendo ninayependa haki. Ni mmoja wa wazee wastaafu waliolitumikia Taifa hili kwa rekodi iliyotukuka!!
 
Kijana wa hovyo sana wewe!! Na hustahili kupata kazi hii, una upumbavu mkubwa sana!! Kuna maandalizi gani unahitaji kufanya kwa jambo usilojua utaulizwa nini na vipi?? Je ndio kusema kama wote mngefaahamishwa siku tatu kabla wote msingefaulu??

Utafika kwenye usahili na malalamiko haya kichwani na utafeli!! Ukisikia kutojiamini ni hii.
Utakaa unavuja mijasho na kutoa hewa chafu na suti yako ya mchongo. Kisha utarudi nyumbani na hutawasikia tena wakiwasiliana na wewe.

Ungekuwa na maana zaidi kama ungesema siku 3 hazikutoshi kusafiri kwenda eneo la usahili. Sio habari ya maandalizi ya written interview ya kitu ambacho hujaambiwa ni nini ujiandae kuandika.
Interview za PSRS ni simple jmn, huez amn interview zangu za mwnzo nlikua nasoma sana ila sikufika oral,
Ikabidi nibalike nikaacha kujisomea, me nikawa nasafir tu Cha msng nigike eneo la tukio, nlifaulu sana na kubahatika kuingia hadi oral saiz nasubir placement tu😂😂.

Cha msing fika eneo la tukio na acha papara, siku tatu zinakutosha kabisa.
 
Kwa taarifa yako mimi si kijana, wala si miongoni wa waombaji wa ajira. Ila mimi ni mtanzania mzalendo ninayependa haki. Ni mmoja wa wazee wastaafu waliolitumikia Taifa hili kwa rekodi iliyotukuka!!
Vyovyote vile Uwe mzee au kijana chamsingi ni tumia siku zilizobaki ujiandae kwa usaili
 
Vyovyote vile Uwe mzee au kijana chamsingi ni tumia siku zilizobaki ujiandae kwa usaili
Zungumzia hoja usizungumzie mtu!! Wala sijasema nahusika na huo usaili. Hoja ni kuwa uwanja hauko sawa kwa wasailiwa wote, zungumzia hoja hiyo!! Simple mind discusses people but greater mind discusses issues!
 
Muda huu ungeutumia kujiandaa Ili kufanya atleast uwanja uwe sawa
 
Inatakiwa uanze kusoma punde tu baada ya ku apply mana UTUMISHI ukitimiza masharti yao lazma uitwe sasa ukikaa usubiri majina yatoke ndio usome kwanza huweza kusoma.

Siku saba utasoma nn na hujui wapi wanatoa ukichukulia contents zipo nyng...

Kufaulu hz written ni zali tu 80% na 20% ni huko kujisomea...
 
Hilo Sio tatizo boss kama unajua unajua tu.Tatizo ninaloona ni ajira kuwa kidogo.yaani unasaili watu 1,000 kwa nafasi 2 za kazi .haya ni matumizi mabaya ya muda na fedha.mtu anatoka mwanza anaenda DAR anatumia fedha kugombania nafasi 2.
Watu 1000 nafasi mbili 😲
 
Kwa taarifa yako mimi si kijana, wala si miongoni wa waombaji wa ajira. Ila mimi ni mtanzania mzalendo ninayependa haki. Ni mmoja wa wazee wastaafu waliolitumikia Taifa hili kwa rekodi iliyotukuka!!
Basi mwambie kijana wako akomae kama anataka hiyo ajira
 
Kwa taarifa yako mimi si kijana, wala si miongoni wa waombaji wa ajira. Ila mimi ni mtanzania mzalendo ninayependa haki. Ni mmoja wa wazee wastaafu waliolitumikia Taifa hili kwa rekodi iliyotukuka!!
Wewe unapenda kulalamika sana, wewe si ndo yule wa Sabato wewe? Punguza malalamiko timiza wajibu wako.
 
Kwa sasa imekuwa kama utaratibu. Kwa mfano ulio hai kuna baadhi ya waombaji wa ajira MDA's na LGA's walipewa taarifa ya kuitwa kwenye usajili tarehe 07/01/2023 na wengine wakaitwa kama majina ya nyongeza siku tano baadaye yaani tarehe 12/01/2023. Na wote hao watafanya usaili tarehe 15/01/2023.

Tunashukuru kwa sababu walioitwa baadaye ni kama walikuwa wamesahaulika kwa hiyo wakikumbukwa tunashukuru. Ni kama hatimaye wametendewa haki.

Lakini tunasema si haki kwa sababu hao walioitwa awali ana siku tano zaidi ya maandalizi kuliko hawa walioitwa baadaye maana tarehe ya usaili ni moja. Kwa kuwa tarehe ya usaili ni 15/01/2023 walioitwa awali wana siku nane (8) za kujiandaa na usaili wa kuandika (written interview) wakati walioitwa baadaye wana siku tatu (3) tu za kujiandaa na usaili huo.

Kwa hiyo hao waliopata muda mrefu wa maandalizi wana nafasi nzuri zaidi ya kufanya vizuri kwenye usaili kuliko waliopata muda mfupi wa maandalizi. Hapo ndipo tunasema si haki.

Kwa hiyo tunaomba sana tume ya ajira wajitahidi kutoa uwanja sawa kwa wasailiwa wote.
Hivi ni tarehe 15 au 14?
 
Pole naona umejaa matusi kwa sababu hujalelewa vizuri na wazazi wako. Si ajabu walikuwa wanakutukana na ukajifunza kwao matusi!

Ninachozungumza ni kutoa uwanja sawa kwa wote!! Tuambie kama ni haki kutokutoa uwanja sawa kwa wote!! Suala si kufaulu wote bali ni wote kucheza kwenye uwanja ulio sawa!! Kama logic hii huwezi kuielewa sina cha kukusaidia.

Kwa taarifa yako mimi si kijana, wala si miongoni wa waombaji wa ajira. Ila mimi ni mtanzania mzalendo ninayependa haki. Ni mmoja wa wazee wastaafu waliolitumikia Taifa hili kwa rekodi iliyotukuka!!
Kama kweli wewe si kijana, ingefaa ufiche hilo hapa. Sikukutukana, nimeeleza mapungufu makubwa katika mtazamo wako na ujinga (kutofahamu) katika unachojaribu kueleza. Kuna haki gani kanyimwa mtu aliyepewa taarifa siku tatu kabla??

Nimeeleza hata ungesema nini kilichokosekana hapo (rejea muda wa safari). Na huenda hujui hata sababu hasa ya hawa kuongezwa, ni vipi basi kama ingekuwa kuna nafasi nyingine zaidi za kuajiri zimepitishwa baada ya kutolewa kwa taarifa siku nane kabla?? Ni vipi kama wameamua kuwa na usahili sasa hivi kwa nafasi zaidi katika kipindi cha mbele na wanataka kufanya usahili mara moja tu??

Narudia kusema, hauna logic katika jambo lako kwa sababu hapa unadhani haki katika taarifa ni jambo la msingi. Ukimuuliza aliyepewa siku tatu atafurahi kuwa hata ameitwa kwenye usahili. Haki za msingi ziko katika usahili - maswali sawa kwa wote, muda sawa kwa wote, bila upendeleo wa rangi, kabila, dini na kadhalika. Na kwa mtazamo wako, basi haki ingekuwa sawa kama wangeitwa wale wa siku nane TU!!

Umeshindwa kuonesha kuwa kuna undeserved advantage wamepata wale wa siku nane!! Ni wazi kuwa kuna mtu wako katika hawa wa siku tatu na kama umelalamikia hili mbele yake au kukubaliana nae - anakwenda kwenye usahili huu akiwa hana kujiamini.
 
Back
Top Bottom