Tunashukuru lakini si haki: Kuitwa kwenye usaili kwa majina ya nyongeza na tume ya ajira

Tunazungumzia logic ya kuweka uwanja sawa kwa wasailiwa wote na si vinginevyo. Jadili kama kwa mazingira haya uwanja uko sawa kwa wote? Je ni haki uwanja usiwe sawa kwa wasailiwa wote? Hiyo ndiyo hoja iliyopo kwenye uzi huu. Ukitaka kuongea vingine ni sawa lakini vifungulie uzi mwingine!!
 
Mbona unaanza kulalamika mapema siku tatu kujiandaa kwa kada yako bado ni nyingi piga msuli kama unaenda kwenye mtihani wa taifa yaani ni mchana na usiku na tusikuone humu hadi baada ya usaili
Kwa taarifa yako mimi si kijana, wala si miongoni wa waombaji wa ajira. Ila mimi ni mtanzania mzalendo ninayependa haki. Ni mmoja wa wazee wastaafu waliolitumikia Taifa hili kwa rekodi iliyotukuka!!
 
Interview za PSRS ni simple jmn, huez amn interview zangu za mwnzo nlikua nasoma sana ila sikufika oral,
Ikabidi nibalike nikaacha kujisomea, me nikawa nasafir tu Cha msng nigike eneo la tukio, nlifaulu sana na kubahatika kuingia hadi oral saiz nasubir placement tu😂😂.

Cha msing fika eneo la tukio na acha papara, siku tatu zinakutosha kabisa.
 
Kwa taarifa yako mimi si kijana, wala si miongoni wa waombaji wa ajira. Ila mimi ni mtanzania mzalendo ninayependa haki. Ni mmoja wa wazee wastaafu waliolitumikia Taifa hili kwa rekodi iliyotukuka!!
Vyovyote vile Uwe mzee au kijana chamsingi ni tumia siku zilizobaki ujiandae kwa usaili
 
Vyovyote vile Uwe mzee au kijana chamsingi ni tumia siku zilizobaki ujiandae kwa usaili
Zungumzia hoja usizungumzie mtu!! Wala sijasema nahusika na huo usaili. Hoja ni kuwa uwanja hauko sawa kwa wasailiwa wote, zungumzia hoja hiyo!! Simple mind discusses people but greater mind discusses issues!
 
Muda huu ungeutumia kujiandaa Ili kufanya atleast uwanja uwe sawa
 
Inatakiwa uanze kusoma punde tu baada ya ku apply mana UTUMISHI ukitimiza masharti yao lazma uitwe sasa ukikaa usubiri majina yatoke ndio usome kwanza huweza kusoma.

Siku saba utasoma nn na hujui wapi wanatoa ukichukulia contents zipo nyng...

Kufaulu hz written ni zali tu 80% na 20% ni huko kujisomea...
 
Hilo Sio tatizo boss kama unajua unajua tu.Tatizo ninaloona ni ajira kuwa kidogo.yaani unasaili watu 1,000 kwa nafasi 2 za kazi .haya ni matumizi mabaya ya muda na fedha.mtu anatoka mwanza anaenda DAR anatumia fedha kugombania nafasi 2.
Watu 1000 nafasi mbili 😲
 
Kwa taarifa yako mimi si kijana, wala si miongoni wa waombaji wa ajira. Ila mimi ni mtanzania mzalendo ninayependa haki. Ni mmoja wa wazee wastaafu waliolitumikia Taifa hili kwa rekodi iliyotukuka!!
Basi mwambie kijana wako akomae kama anataka hiyo ajira
 
Kwa taarifa yako mimi si kijana, wala si miongoni wa waombaji wa ajira. Ila mimi ni mtanzania mzalendo ninayependa haki. Ni mmoja wa wazee wastaafu waliolitumikia Taifa hili kwa rekodi iliyotukuka!!
Wewe unapenda kulalamika sana, wewe si ndo yule wa Sabato wewe? Punguza malalamiko timiza wajibu wako.
 
Hivi ni tarehe 15 au 14?
 
Kama kweli wewe si kijana, ingefaa ufiche hilo hapa. Sikukutukana, nimeeleza mapungufu makubwa katika mtazamo wako na ujinga (kutofahamu) katika unachojaribu kueleza. Kuna haki gani kanyimwa mtu aliyepewa taarifa siku tatu kabla??

Nimeeleza hata ungesema nini kilichokosekana hapo (rejea muda wa safari). Na huenda hujui hata sababu hasa ya hawa kuongezwa, ni vipi basi kama ingekuwa kuna nafasi nyingine zaidi za kuajiri zimepitishwa baada ya kutolewa kwa taarifa siku nane kabla?? Ni vipi kama wameamua kuwa na usahili sasa hivi kwa nafasi zaidi katika kipindi cha mbele na wanataka kufanya usahili mara moja tu??

Narudia kusema, hauna logic katika jambo lako kwa sababu hapa unadhani haki katika taarifa ni jambo la msingi. Ukimuuliza aliyepewa siku tatu atafurahi kuwa hata ameitwa kwenye usahili. Haki za msingi ziko katika usahili - maswali sawa kwa wote, muda sawa kwa wote, bila upendeleo wa rangi, kabila, dini na kadhalika. Na kwa mtazamo wako, basi haki ingekuwa sawa kama wangeitwa wale wa siku nane TU!!

Umeshindwa kuonesha kuwa kuna undeserved advantage wamepata wale wa siku nane!! Ni wazi kuwa kuna mtu wako katika hawa wa siku tatu na kama umelalamikia hili mbele yake au kukubaliana nae - anakwenda kwenye usahili huu akiwa hana kujiamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…