japo mliomba msaada wa kampuni Bora ya mawakili Ili muweze kusaidiwa kupata haki zenu. Kwa faida ya jukwaa ndaelezea utaratibu wa mashauri ya kazi ikiwa ninyi ni watumishi wa umma au kwa wale wa taasisi binafsi
Kwa watumishi waumma yapo mabadiliko ya Sheria kutokana na maamuzi ya kesi kadhaa tangu mwaka 2017 kuja mbele kuhusu sehemu sahihi ya mtumishi kupeleka malalamiko yake.
ikiwa umeshawasilisha malalamiko yako kwa mkuu wa idara yako na hayakutendewa kazi. Basi unanafasi ya kuwasilisha malalamiko yako katika tume ya utumishi wa umma kwa HATUA zaidi, ikiwa Tume itashindwa basi unanafasi ya kuyapeleka kwa rais (katibu mkuu) ambapo yeye kwa vyombo vya utatuzi wa migogoro kwa watumishi wa umma ndio mwisho.
ikiwa hujaridhika basi utaenda mahakamani kuomba mapitio ya mahakama kuhusu maamuzi hayo. JUDICIAL REVIEW) Ikishindikana hapo utakuwa huna namna tena.
WATUMISHI TAASISI BINAFSI
Wao wanapaswa kupeleka migogoro yao CMA ndani ya siku 30 tangu kuanza kwa mgogoro husika.
hii kwasasa nikwajili ya watumishi wa taasisi binafsi.
Ahsante sana ,nina omba kueleza japo kwa ufupi.Sisi kesi yetu niya usajili.Tulienda kusoma vyuo vya nje ya nchi tukiwa na sifa zote za kusoma chuo kikuu(Wote tulikuwa na NO OBJECTION CERTIFICATE KUTOKA TCU) .Tulienda kusoma kwa vyuo tofauti tofauti na kwa miaka tofauti tofauti .Lakini pia tumeganyika kuna ambao walienda kusoma wakitokea kazini na wale walikuwa wakitoka shuleni moja kwa moja(Fresh from school).
Kesi yetu inazaidi ya miaka 10.Kwa maana wahitimu wa kwanza walikuwa mwaka 2011.
Tulisoma udaktari wote kwa vyuo vinavyo tambulika na TCU na TCU ikatupatia idhibati ya kutambua shahada zetu.
Baraza la madaktari Tanganyika (MCT ) lilikataa kutupatia mtihani ,lilikataa kutupatia kibali cha kufanya mazoezi kwa vitendo(Internship),Ikakataa kutusajili kama madaktari kamili ,Sababu ikawa ni moja tumesema shahada hiyo kwa miaka 4 badala ya miaka 5.
Tulijieleza kwa vielelezo kuwa tumesoma vyote ambavyo anapaswa kusoma daktari ,tumesoma miaka 4 yenye jumla ya mihula 12 kwa maana ya mihula mitatu kila mwaka (Trimesters).
Daktari aliyesoma miaka 5 ana jumla ya semester 10 kwa maana ya kila mwaka kuwa na mihula 2.
Tuliandika barua ikiwa na vielelezo vya curriculum yetu na curriculum ya vyuo vyote vya hapa nchni.
Tumeandika barua zaidi ya tatu ,Waziri wa afya anajua,Katibu mkuu wizara ya Afya,Mganga mkuu wa serikali anajua na msajili (MCT) anajua.
Tumefika wizarani ,tumefanya kikao na Katibu mkuu wa wizara ya afya ,Katibu akasema hilo swala nilakitaaluma tumuone Mganga mkuu wa serikali(Ambaye kwa sasa ameshaondolewa kwenye nafasi hiyo ) Mganga mkuu alitusikiliza akatutaka tukafanye kikao na msajili.Tukarudi kwa msajili tukafanya kikao cha pamoja akakili kubwa haoni tofauti.Lakini atawasilisha kwenye kikao cha Baraza.
Katika barua zote walitujibu barua moja ,wakiwa wanatutaka tuwe na subira wakati wakiendelea na majadiliano
TULIWAOMBA YAFUATAYO
1.Watupime kwa mtihani
2.Watuoneshe ni wapi kuna madhaifu kwenye training yetu ,nasi tutayafanyia kazi.(Kama nikurudi shule kwenye sehemu zenye madhaifu tuko tayari)
AJABU
1.Hataki kutupatia mtihani iliwaone udhaifu wetu
2.Hawataki kusema kuna madhaifu wapi
3.Wiki hii wameamua kutusajili kama madaktari wasaidizi (Cheo ambacho kilishafutwa).Na hata hivyo training yetu inaruhitaji kumgusa mgonjwa mara baada ya kufanya Internship lakini Daktari msaidizi (AMO) hahitaji Internship kwa maana yeye ni PRACTICAL TRAINING BASED ,Sisi wameamua kutupatia kibali cha kufanya upasuaji na kutibu wagonjwa bila kupitia Internship kitu ambacho ni hatari kwa afya za Watanzania.
3.Kati yetu kuna walionda kufanya Internship nje ya nchi lakini wamekataa kuwasajili kama madaktari
4.Kati yetu tunao madaktari bingwa wanne,mmoja amemaliza MMED (Radiology ) Alexandria University ,Mwingine anasoma Pretoria University Masters of medicine in internal medicine (MMED ),Mwingine yupo Adidas Ababa University Mmed (Gynaecology and Obstetrics)
Waha wote hawawezi kusajiliwa kama madaktari bingwa ikiwa usajili wa awali umeshindikana
TUNAOMBA MSAADA WA KISHERIA TAYARI TUNA 4M mkononi