Lookmalasin
JF-Expert Member
- Jan 7, 2017
- 2,233
- 3,144
Unajua Tanzania, Afrika inahitaji kiongozi mtenda haki anayependa demokrasia, haki, uhuru, amani na utulivu kwa wote.Tulikuwa na rais wa namba hiyo, mkamuua, basi tuendelee hivohivo
Haki, Amani, utulivu, demokrasia ni nini?
Tumekuwa brainwashed kufikiri haki ni kuongea chochote, haki za kisiasa tu.
Lakini haki za msingi za binadamu za kwanza kabisa ni za kiuchumi, kupata chakula, elimu, maji, makazi, umeme, afya, ajira, miundombinu kusikilizwa kwenye kwenye ofisi za umma.
Haki ya msingi ni kuhakikisha pato Taifa linatumika kwa maslahi ya Watanzania wengi.
Haki ya kiuchumi siku zote inatangulia haki zingine zote za kisiasa. Ukipata elimu, chakula, maji, nyumba, kipato utatambua haki zako zingine zote. Bila hivyo vitu vya msingi, hata huna habari za haki za kuhutubia, katiba mpya, tume huru.
Hizi haki za msingi zikiwepo zinaleta amani, utulivu baadaye haki za kisiasa na haki nyingine zote.
Ukipata haki za kiuchumi, haki zingine zote za kisiasa, kidemokrasia zitafuata.
Ndio maana watu kama JPM, Ibrahim Traore, Xi Jimping, Faye wanapendwa.