Tunataka Rais na Tanzania ya kufunga mkanda na kuuma meno

Tulikuwa na rais wa namba hiyo, mkamuua, basi tuendelee hivohivo
Unajua Tanzania, Afrika inahitaji kiongozi mtenda haki anayependa demokrasia, haki, uhuru, amani na utulivu kwa wote.

Haki, Amani, utulivu, demokrasia ni nini?
Tumekuwa brainwashed kufikiri haki ni kuongea chochote, haki za kisiasa tu.

Lakini haki za msingi za binadamu za kwanza kabisa ni za kiuchumi, kupata chakula, elimu, maji, makazi, umeme, afya, ajira, miundombinu kusikilizwa kwenye kwenye ofisi za umma.

Haki ya msingi ni kuhakikisha pato Taifa linatumika kwa maslahi ya Watanzania wengi.

Haki ya kiuchumi siku zote inatangulia haki zingine zote za kisiasa. Ukipata elimu, chakula, maji, nyumba, kipato utatambua haki zako zingine zote. Bila hivyo vitu vya msingi, hata huna habari za haki za kuhutubia, katiba mpya, tume huru.

Hizi haki za msingi zikiwepo zinaleta amani, utulivu baadaye haki za kisiasa na haki nyingine zote.

Ukipata haki za kiuchumi, haki zingine zote za kisiasa, kidemokrasia zitafuata.

Ndio maana watu kama JPM, Ibrahim Traore, Xi Jimping, Faye wanapendwa.
 
Watakwambia tunafunga mkanda, halafu kiuhalisia watakaofunga mkanda ni wananchi wakubwa watabaki kusosomola tu.

Tanzania , Afrika inahitaji kiongozi mzalendo, mwenye uthubutu, anayejiamini, mwenye malengo, vision, mission, seriousness, mtendaji, anayewajibika yeye mwenyewe na kuwawajibisha walio chini yake wote.

Ndio maana JPM,Traore, Diomaye Faye wanapendwa Afrika nzima.

Xi Jinping China anapendwa China, UAE, Qatar, Saudi kumetulia sababu viongozi wao wana akili timamu wamewapa Wananchi wao haki za msingi za kiuchumi kwanza.

Wakiziondoa hizo haki. Ufisadi ukitamalaki kama Tanzania pesa zote zinaenda kwa familia chache, 1% wananchi wao wangeanza mapinduzi.
 
Tupate katiba mpya kwanza hiyo ndio itakuwa nguzo ya kufika huko , kwa katiba hii inaweza kuleta dikteta mwingine mwendawazimu kwa mara ya 3 mfululilizo.
Mbona Nyerere alitumia katiba hiihii na tunamsifia Kila siku? Mbona Magufuli alitumia hiihii kujenga reli, flyovers, madaraja na kutumbua watu?. Labda tufunge safari kwenda Kenya tukapate uzoefu wao kuhusu faida walnazopata kwa kuwa na katiba mpya n tume huru ya uchaguzi ili tupate nguvu za kudai katiba mpya.
 
Mbona Nyerere alitumia katiba hiihii na tunamsifia Kila siku?
Unamsifia wewe na nani?

Binafsi mimi simsifu yeye ndio chanzo cha yote haya, 1965 alifuta vyama vingi ili abaki mwenyewe hadi anaastaafu ameshiri uchaguzi wa vyama vingi mara moja tu kwa miaka 24 ya uongozi wake.
Mbona Magufuli alitumia hiihii kujenga reli, flyovers, madaraja na kutumbua watu?.
Magufuli alitoa pesa zake kujenga hayo madaraja?

Kutumbua watu gani,? Vyeti feki viko kila idara je alitimua vyeti feki kila idara unayoijua?

Mkoloni alijenga reli, madaraja, hospital ,shule je ilimaanisha alikuwa mzuri,?

Babu zetu na bibi zetu wangapi wamekufa katika shughuli hizo za ujenzi wa hiyo miundombinu bila ujira na uvunjifu wa haki za binadamu ikiwemo usafirishaji haramu wa binadamu?
Labda tufunge safari kwenda Kenya tukapate uzoefu wao kuhusu faida walnazopata kwa kuwa na katiba mpya n tume huru ya uchaguzi ili tupate nguvu za kudai katiba mpya.
Faida zipo mojawapo kubwa tu ni katiba ndio sheria mama na rais hayupo ya katiba.

Tanzania katiba sio sheria mama , inategemea rais kaamkaje siku hiyo.
 
Bana ehee...!! Wabongo hawamtaki huyo raisi unayemtaka wewe.

Wewe una dream za kumpata kiongozi aina ya Traore, kiongozi mzalendo na anayefocus kwenye self-reliance ambaye hataki kabisa utumwa unaombatana na misaada.

Sasa wabongo wanataka kiongozi ambaye atamwaga pesa za bwerere kwenye miradi na asifuatilie chochote kuhusiana na pesa hizo, na mara nyingi pesa za kumwaga mwaga tu ambazo hazina uchungu huwa ni pesa za wafadhili/misaada.

Na ndio maana kila mtumishi sasa hivi kauli yake ni moja tu "mama mitano tena"... kwa sababu watu wanagawana tu mihela ya wafadhili.

Wewe unafikiri kwanin namba E inakimbia sana na asilimia kubwa wanaoagiza kununua magari ni watumishi? Halafu leo hii eti uje uwaletee magufuli mwingine? Kama hawata kuroga basi watakuua.
 
Kwenye zile report anazosomaga Mwigulu nchemba akiwa anawasilisha bajeti ya wizara ya fedha, pale anaposema 100b zimeenda kwenye miradi ya maendeleo halafu 900b zimeenda kwenye matumizi ya kawaida, basi hayo matumizi ya kawaida ndio kama hayo sasa i.e kununua magari ya washawasha,kuwalipa police posho hili wavunje watu miguu kwenye maandamano,kuhonga meshekh na machawa hili waendelee na mapambio,kulipana posho za vikao kwenye kamati ya ulinzi na usalama kila kata,kila wilaya na kila mkoa... na mengine meengi.

This country is rotten to the core.
 
Hapa hapa Tanzania au Mbinguni
 
Rais Muuaji kwa kisingizio cha maendeleo huku akijiwekea utajiri mwingi kwa familia yake na wanaomlinda? Huyo hatumtaki
 
Kaka sifa ya kwa kwanza ya kiongozi wa kweli wa wananchi ni kuchukiwa na kuwindwa kuawa na nchi za Magharibi. Ukiona kiongozi wenu ni rafiki mkubwa wa nchi za Magharibi ujue hapo hakuna kiongozi madhubuti.

Unapoona mtu anataka kuwa kiongozi lakini anawasema vizuri viongozi wa Magharibi, anapata usaidizi wa Magharibi, familia yake Iko nchi za Magharibi, anapata misaada kutoka nchi za Magharibi hasa zile za ufaransa, uingereza, ubelgiji, Italy, na Marekanani kumchagua huyo mnafanyakazi ya Bure kabisa, hamna kitu.

Misaada kutoka nchi hizi sio misaada bali ni mali zinazoibiwa kwenu na afrika.
 
Anachokutana nacho Ibrahim Traore kule Burkina Faso ndio uhalisia wa viongozi wote wa Afrika walichostahili kufanyiwa na nchi za Magharibi. Akina Gaddafi, Sankara, Lumumba, Nkrumah, Magufuli, Nyerere, nk walikutana nacho pale walipotaka kufanya mambo yenye mafufaa kwa watu wao. Watu wanadhani kuwa Nyerere aling'atuka kwa hiari yake tu, hapana bali mabeberu walimfikisha Kona mbaya sana ya vikwazo.

Binafsi ninawatazama Lissu na Lema kisha nacheka tu. Eti wanataka kuikomboa Tanzania na WA Tanzania lakini wanaishi Ulaya.
 
Nchi hii haitaendelea kamwe kama watu wachache tu ndio wanaofanyakazi na kulipa Kodi. Haitaendelea kama hatusimamii rasilimali zetu; ardhi, madini, wanyama, samaki, bandari, na misitu yetu. Hatutaendelea kama hatutakuwa na sheria na adhabu Kali sana kwa wasiofanyakazi, wakwepa kodi na wezi wa mali ya umma.

Kutegemea misaada ni ujinga unaoumiza vizazi vijavyo hata kama Leo inaonekana ni shuluhisho la matatizo yetu.

Maisha magumu na maisha mazuri yaonekane kuazia Ikulu hadi kitongojini.
 
Ukiona Ibrahim Traore anaandamwa hivi na viongozi wa Afrika wako kimya inaana kuwa hata wao huko kwao hali sio nzuri, wamekabwa na mabeberu na kuimba wimbo wao. Hii ni kuonyesha kuwa adui yetu halisi ni nchi za Magharibi; France, UK, Belgium, Italy, USA na German na Spain kidogo sana. Watamuua tu ili iwe fundisho kwa wengine. Lazima tuungane kupambana na maadui Hawa badala ya watu kutuamimisha kwamba adui yetu no 1 ni Katiba na tume ya uchaguzi. Tuambiane ukweli ili tupone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…