Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 790
- 1,316
Hakuna ubishi, wito wa Mh. Makamu wa Rais, Balozi, Dr. Emmanuel Nchimbi, wa kuwahimiza watanzania kupigania katiba mpya, umepata mwitikio na hamasa kubwa kutoka kwa watanzania wote.
Kwa kuzingatia maoni mbalimbali yaliyotolewa, ni wazi kuwa tupo tunaomuona Dr. Nchimbi kama kiongozi wa mfano, aliyetoa kauli sahihi kwa wakati sahihi; Na wengine wanaomuona kama ni mkakati wa CCM na serikali kuwazubaisha wapinzani, wanaharakati na wananchi kwa ujumla.
Binafsi sikubaliani na mashaka ya hili kundi la pili kutokana na ukweli kwamba linapuuza tabia na haiba ya Dr. Nchimbi ya muda mrefu ya kusimamia anachokiamini hata kama wenzake ndani ya chama hawakitaki.
Mifano ni mingi, kwa uchache nitawakumbusha kuwa Dr. Nchimbi akiwa mjumbe wa kamati kuu, aliwahi kujitenga na uamuzi wa kamati kuu, kuwaengua Lowasa na wenzake kugombea uraisi. Bila woga alieleza kuwa Rais Kikwete alienda kwenye kikao na majina yake mfukoni bila kujali nani anakubalika kwa wananchi.
Mfano wa pili ni msimamo wake dhidi ya upinzani akiwa katibu mkuu wa CCM. Dr. Nchimbi ndiye kiongozi wa juu wa CCM aliyejitokeza si mara moja au mara mbili kukemea kauli tata za makada wa CCM zenye mwelekeo wa kuvunja haki za kiraia za wapinzani. Alipiga marufuku wimbo wa Toti unaosema, "wapinzani tuwachanechane tuwatupe" na alikemea kauli za vijana wetu wa UVCCM zenye mwelekeo wa kuwadhuru wapinzani.
Hata hivyo, zipo hoja nzito ambazo wito wa makamu wa Rais unaziibua nazo ni zile ziliyoibuliwa na Askofu Bagonza pamoja na Sugu, mbunge wa zamani wa Mbeya mjini. Hoja hizo ni; watanzania wanatakiwa wapambane na nani kupata katiba mpya? Kama wanatakiwa wapambane na serikali, wapambane kwa namna gani ikiwa harakati yoyote wanayoianzisha wanashtakiwa kwa uhaini, ugaidi na uchochezi?
Ni wazi kuwa mijadala yetu itatusaidia kupata majibu ya hizi sintofahamu mbili zilizoachwa