Plot4Sale Tunauza Nyumba, Mashamba na Viwanja sehemu mbalimbali

Hii nyumba Bw Dalali tangu Mwaka Jana mwezi wa 11 ,haijauzika tatizo Nini,umeongeza Cha juu Sana ,au Ni mambo ya mfuko hayajakaw sawa
Ni kweli ila saivi itauzika tu maana tumeshaanza kupata wateja tunaongea nao.hamna cha juu ndg yangu tunauza bei ya mwenye nyumba na mwisho wa siku muuzaji na mteja watakutana na kuongea wenyewe..me changu hapo ni commission tena kwa kujadiriana kwa pande zote tatu.
 
Mungu atusaidie sana ndg yangu
 
Na hata hiyo nyumba ya mil 700 itakua sio ya kawaida ni ikulu ndogo.
Nyumba nyingi za ghorofa nzuri unazoona ni around 350m, Sasa fikiria hiyo ya mil 700
Na pia ninazo mkuu nauza mpaka 150m maeneo mengine lakn
 
Wenye hela hawawazi, ila sisi wakina pangu pakavu tia mchuzi, hiyo B 1.7 ishaangukia kwenye mahesabu mengine.. Hiyo point saba tu napata bonge la kiwanja kibada na kujenga mjengo zaidi ya huo, halafu B 1...🤣
Jumba kali la 300M ukiongezea 100M ni landscape za maana na garden pamoja na makeke mengine mzee yani panakuwa kama kiji mansion cha aina yake. Uwanja wa kutosha pool, basketball court, Recreations za kutosha
 
Kuna kitu huwa sielewi kwa hawa watu wanajiita madalali, hivi kweli nyumba hiyo ni billion 1.7? Hebu tuwe wa kweli, karne hii unanunua nyumba kama hiyo 1.7 B wakati unaweza jenga nyumba nzuri zaidi ya hiyo kwa million 500 tu
 
Naijua hii nyumba tena hapo imepigwa rangi mkono mmoja ilikuwa kama gofu. Mzee aliyekuwa anakaa hapo alikuwa na mvi nyeupe kichwa kizima na hana mtoto. Nadhani alishadanja mwaka jana au juzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…