Huyu anachagua wa kuwajibu
Biashara haiko hivyo
Anyway sehemu zipo nyingi
Usikasirike kama hajakujibu, am sure atakua hajaiona meseji,
Meseji zinatiririka nyingi sana za kuuliza vitu tofauti, kuwa na subira, akiiona atajibu tu,
Mleta thread ana nia nzuri ya kufanya biashara, Big up, ila ni vema pia ushauri mzuri anaopewa akauchkua tu na kuufanyia kazi,
Biashara matangazo, na unatakiwa kujiongeza pia, mfano umeona kuna mtu kakushauri kuhusu kuweka pic na bei yake, huu ni ushauri mzuri, hupotezi chochote kwa kubandika bei Chini yake, hii itakusaidia kupunguza maswali yasiyo ya lazima.
Af usilazimishe watu wakupigie, wee ukipata chance ingia jf fatilia meseji, jibu kwa ufasaha, mfano mtu akiuliza TV aina flani bandika pic yake na nyinginezo +bei zake na other alternative, na huduma ya kufikishiwa alipo!!! HUPOTEZI KITU KUPOST TU HUMU! it's your business, and it's you utaevutia watu
Ushauri tu