Tunauza Viwanja na Mashamba Chalinze na Dar Es salaam
Chalinze Ekari moja 4 mil? Sahau mteja.. Bei iko juu mno mnooo
 
Kiwanja kipo Kibaha mlandizi chenye ukubwa miguu 25 kwa 25 umbali mpaka Morogoro road mita 600 huduma zote za kijamii zipo.
Bei milioni tano.
Kwa mawasiliano na maelezo zaidi karibuni PM
 
ENEO LINAUZWA
Eneo lenye ukubwa wa ekari ishirini linauzwa Pingo, Chalinze eneo linapakana na Chuo cha Ualimu Chalinze kwa mbele na kwa upande wa kulia ni kiwanda kipya cha vigae cha Twyford kinachojengwa hapo Pingo.Kama ambavyo baadhi watakuwa wanajua, kiwanda cha vigae kitaajiri wafanyakazi wa kudumu 6,000 achilia mbali madereva na makonda wa malori watakaokuja kupakia mizigo wanaokadiriwa kufikia 2,000 kila siku ambao watalazimika kutafuta malazi. Kwa ujumla eneo hili linategemewa kuhudumia *watu elfu kumi kila siku kwa makazi na malazi.

Pamoja na hayo, ujenzi wa bandari kavu unaoendelea eneo la Kwala Railway Station unaliongezea eneo hili matumizi mengine muhimu sana katika biashara. Mizigo yote inayoingia au kutoka bandarini ni lazima.

Ikaguliwe na maofisa wa serikali ambao kimsingi ni waajiriwa wa mamlaka ya Mji Mdogo na Wilaya mpya ya Chalinze. Eneo linatoa fursa kwa makampuni ya _usafirishaji, uwakala wa forodha_ na _uwakala wa meli_ kuweka yadi kwa ajili ya kuhifadhia, kukagulia, kupakilia na kupakulia mizigo inayoingia au kutoka bandarini yakiwemo makontena yenye shehena na matupu.

Pamoja na hayo, uwepo wa shughuli za kibandari jirani na eneo hili unavutia _uwekezaji wa nyumba za kulala wageni, maofisi_ na _sehemu za biashara._ Kwa mfano watu watano walipakia mizigo yao ndani ya kontena moja, siku ya kulitoa bandarini ni lazima wote wawepo kwa ajili ya kupokea mizigo yao. Siku ya kupokea mzigo ikaangukia Ijumaa na bahati mbaya mashine ya kupakilia mzigo ikaharibika au ikawepo sababu nyingine yoyote, basi wote watano watakuwa wageni eneo hili kwa siku 3. Watahitaji kula, kulala, kunywa na kupumzika.

Kwa ujumla eneo lote la Chalinze, Pingo linatoa fursa ya kujenga *Dar es Salaam Mpya* ya siku za usoni. Wakati wa kuwekeza ni *sasa* ambapo *ekari moja* ni TShs. *4,000,000* (milioni nne tu) na maelewano yapo. *Unapimiwa kulingana na mahitaji yako* na pia tunafanya upimaji _(surveying)_ na kulifanya eneo lako *litambulike kisheria* kwa gharama nafuu sana. Wasiliana nami pm
 
Back
Top Bottom