Tunavuna aibu – Wapinzani

Tunavuna aibu – Wapinzani

MImi sasa naaamini vyama vya upinzani vinatumiwa tu kama geresha na chama tawala.
Utakuta vyama havina nguvu wadau wakiomba viungane ili viwe na nguvu kama wasahili wasemavyo umoja ni nguvu utengano ni udhaifu wao wanakuwa hawataki.Wanang'ang'ania kujitenga lengo la upinzani si kushindana kwa hoja na chama tawala sasa iweje wakatae kuungana wakati vyama vyao havina nguvu?Upinzani upo kwa masrahi yanani?
 
MImi sasa naaamini vyama vya upinzani vinatumiwa tu kama geresha na chama tawala.
Utakuta vyama havina nguvu wadau wakiomba viungane ili viwe na nguvu kama wasahili wasemavyo umoja ni nguvu utengano ni udhaifu wao wanakuwa hawataki.Wanang'ang'ania kujitenga lengo la upinzani si kushindana kwa hoja na chama tawala sasa iweje wakatae kuungana wakati vyama vyao havina nguvu?Upinzani upo kwa masrahi yanani?

wewe kwa mawazo yako havina nguvu kwa sababu havijaungana? mimi nakataa kabisa ngoja nikupe mfano mrahisi tu si tuna vyama 13 vya siasa? kati ya hivyo toa CCM, chadema na CUF halafu uviunganishe vilivyobaki chausta, nccr na nk . Kwa hesabu yako wewe hivyo vyama vilivyoungana vitakuwa na nguvu kuvizidi hivi vingine. Najua jibu lako litakuwa hapana hivyo umekili kuwa kuwa na nguvu siyo kuungana bali ni kwa chama kuwa na
(i) itikadi,
(ii) strategy
(iii) na dhamira ya kisiasa

chama chochote hakitaweza kuwa na nguvu kwa kuungana tu nakuomba ufute hicho akilini kwako na kwa kifupi ni kwamba kuunganisha vyama ni kuvifanya dhaifu kwani inabidi mucopromise hivyo vitu vitatu hapo juu. Al Gore alijua kabisa kuwa Nader alikuwa anachukua kura zake kwenye toss up state na angemsababishia kukosa majimbo mengine. kwa akili zako wewe ungetaka aende kwa Nader na kuungana naye na kutengeneza chama kipya. kwa taarifa yako hakufanya hivyo ni bora ukose urahisi kuliko kuungana na mtu mnaye pingana kiitikadi

Ross Perot alipata 19% ya kula za uchaguzi wa marekani mwaka 1988 na kusababisha clintoni awe rais. G W Bush alijua effect ya RP lakini hakuwa na sababu ya kucompromise na kwenda kuunga na chama cha RP ingawa wote walikuwa ni watu wa mlengo wa kulia na hii ndiyo demokrasi sasa nyie mnataka nini jamani. History imejihakikishia kuwa ni somo zuri sana kwani linatufundisha mambo yaliyopita na yaliyopo ili kuweza kupanga mambo yajayo. lakini nyie wenzetu mnataka kukurupuka tu na kuunganisha vyama vya siasa kna kuisahau history mna ugonjwa gani?
 
Mkuu Shalom nashukuru kwa maelezo yako.
Nacho taka kusema hapa refence yako imebase katika nchi iliyo piga hatua kimaendeleo kwa kila kitu naweza kusema yenye demokrasia ya kweli ukasahau kuwa Tanzania ni nchi changa sana katika demokrasia.
Jaribu angalia nchi kama Kenya wapinzani waliungana wakaung'oa utawala wa KANU katika harakati za ukombozi nchi za kimaskini kama zetu hizi siku zote umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu na 'kidole kimoja hakivunji chawa'.
Upinzani wasinge ungana wasingeweza kuchukua nchi hapo Nairobi.
Kinacho tuangusha sisi ni uroho wa madaraka wakiungana mara utasikia Mrema anataka agombee urais kwa mfano au Lipumba.
Mkuu elewa kuwa nchi zetu hizi ni maskini kwa kila kitu ndo maana tunasisitiza UMOJA kwa kila kitu nina uhakika baadae tutafika tu.
 
Mkuu Shalom nashukuru kwa maelezo yako.
Nacho taka kusema hapa refence yako imebase katika nchi iliyo piga hatua kimaendeleo kwa kila kitu naweza kusema yenye demokrasia ya kweli ukasahau kuwa Tanzania ni nchi changa sana katika demokrasia.
Jaribu angalia nchi kama Kenya wapinzani waliungana wakaung'oa utawala wa KANU katika harakati za ukombozi nchi za kimaskini kama zetu hizi siku zote umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu na 'kidole kimoja hakivunji chawa'.
Upinzani wasinge ungana wasingeweza kuchukua nchi hapo Nairobi.
Kinacho tuangusha sisi ni uroho wa madaraka wakiungana mara utasikia Mrema anataka agombee urais kwa mfano au Lipumba.
Mkuu elewa kuwa nchi zetu hizi ni maskini kwa kila kitu ndo maana tunasisitiza UMOJA kwa kila kitu nina uhakika baadae tutafika tu.
 
Wapinzani Tanzania ni ma populist tuu.. Hakuna sera inayoeleweka.. On one has ever come up with any agenda that will work... Itachukua muda mrefu sana mpaka tupate upinzani waukweli.
 
Mkuu Shalom nashukuru kwa maelezo yako.
Nacho taka kusema hapa refence yako imebase katika nchi iliyo piga hatua kimaendeleo kwa kila kitu naweza kusema yenye demokrasia ya kweli ukasahau kuwa Tanzania ni nchi changa sana katika demokrasia.
Jaribu angalia nchi kama Kenya wapinzani waliungana wakaung'oa utawala wa KANU katika harakati za ukombozi nchi za kimaskini kama zetu hizi siku zote umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu na 'kidole kimoja hakivunji chawa'.
Upinzani wasinge ungana wasingeweza kuchukua nchi hapo Nairobi.
Kinacho tuangusha sisi ni uroho wa madaraka wakiungana mara utasikia Mrema anataka agombee urais kwa mfano au Lipumba.
Mkuu elewa kuwa nchi zetu hizi ni maskini kwa kila kitu ndo maana tunasisitiza UMOJA kwa kila kitu nina uhakika baadae tutafika tu.

Fidel80,

Inabidi tuwe makini sana na hii dhana ya nchi maskini. Kanuni huwa hazina cha umaskini wala utajiri wote tunakuwa sawa na kanuni. Mfumo wa vyama ving una kanuni zake na usipozifuata uwe nchi maskini au tahiri zinakuasili tu. Hatuwezi kusema kuwa kwa sababu sisi ni maskini basi moja+Moja ni tatu.

Mgfano wa Kenya nadhani unaonesha njisi ya kuungana bila kuwa na itikadi moja kunavyoweza kuleta madhara. watu takribani 1000 wamekuf kufuatia hiyo miungano batili. KANU haikuhusika kabisa hau hujui? na hichi ndiyo nacho kisema lengo letu ni tujenge demokrasia siyo kuiondoa CCM madarakani ingawa kuwa na demokrasia moja kwa moja inamaanisha chama cha mafisadi nje kwani hakuna anayependa ufisadi.

Umoja ni nguvu hili halina ubishi ila huwezi kuunganisha itikadi mbili tofauti bila kucompromise. Mfano Chadema ina wanachama 100 na kafu 100 ukiweza kuwaunganisha hawa unapata wanachama 200 hii ni mathematically na siyo practical kwa itikadi ukiuunganisha hivi vyama wanachama 50 wa chadema watakimbia na wanachama wa cuf 50 watakimbia kwa kutokukubari itakadi za chama kingine na unaweza kubaki na wanachama chini ya 100 mlikokuwa nao hapo mwanzo. Ila kama wote mnachukia ufisadi ni rahisi tu kushirilkiana na kuanzisha maandamano kwa wanachama wenu wote 200 kupinga na kila mtu kurudi kwenye itikadi yake anayoiona inafaa kuendeleza nchi.

Hakuna shada kwa lipumba, mbowe na wengine walioshiriki uchanguzi uliopita ambao walipata all most 20% ya kura huwenda limpumba angesimama peke yake labda angepata 11% kwa kuwa hakuna guarantee kuwa wote waliompigia kura chadema mbowe asingekuwepo wangempigia kura lipumba. Kuna watu wachache sana waliopiga kura upinzani asilimia kubwa walipigia chama, sasa huo muungano unauona wa muhimu kwa nini.

Mimi mwenyewe kura yagu ilienda kwa upinzania lakini ni chama kimoja tu nilichokuwa tayari kukipigia kama wasinge simamisha mgombea basi ningekuwa sina mtu wa kumpigia kura.
 
Wapinzani Tanzania ni ma populist tuu.. Hakuna sera inayoeleweka.. On one has ever come up with any agenda that will work... Itachukua muda mrefu sana mpaka tupate upinzani waukweli.

Kaka

wewe uko upande upi kwani kama una akili timamu na ni mtanzania ni lazima utakuwa na upande mmoja either wa chama tawala au upinzani. Na kama ni hivyo basi wewe ni ccm. na kama ni ccm hatuwezi kushangaa kwa sababu si unataka upande wako uonekane mzuri. Inahitaji courage kubwa sana kutuambia mamilioni ya watanzania tulio upande wa upinzani ni mapopulist, hizi kauri za kejeri zinazofanana na za vijisenti ipo siku zitakwisha tu.
 
Shalom,
Mkuu unazungumzia Ushabiki hapa na sioni kama unatutakia mema sisi wananchi wote.. Kama ni swala la Uanachama wa Chadema basi mimi mkuu wangu kwa taarifa yako mimi CHADEMA tena naweza kusema ni mtu pekee ambaye hana wadhifa wala nafasi ndani ya Chadema na kajitoa wazi hapa JF ukumbini..wengine wote wanajificha chini ya kivuli wanaona sijui aibu!.. au unataka nikwambie kadi yangu namba ngapi! - Mkuu huwa sina kitu cha kuficha na nikiamua kukipaka nakipaka hata kwa ndugu zangu acha Chama..

Sasa turudi kwenye mada, kwanza nilisema kwamba vyma vya Upinzani ili viweze kushinda mikoani ni vizuri (as a suggestion) kama wakiachiana wilaya ambazo mgombea wa chama fulani kashika nafasi ya pili chini ya CCM.. Naposema chini ya CCM nina maana zile sehemu ambazo Upinzani walishindwa na CCM..

Sikusema hivyo kwa sababu labda nimefikiria tu out of blue.. no mkuu wangu nilipitia matokeo ya mwaka 2005, nikaona viti 60 ambavyo Upinzani wangeweza kabisa kushinda kama wangeweka mtu mmoja tu nikichukulia ushindi wa CCM ulikuwa chini ya asilimia 60...I did my homework mkuu wangu...

Sasa inapobakia wagombea wawili tu mara nyingi kunakuwepo na swing vote hivyo ukijumuisha kampeni za vyama vyote vya Upinzani wakiwa pamoja wangeweza kabisa kushinda majimbo hayo..
Kisha ukisha weza kujenga majimbo 60 ya uhakika kupata ushindi ni rahisi kwa majimbo yaliyokuwa jirani ku swing pia kwa sababu nimeona pia matokeo mengi yamekuwa aidha dhaifu au kimbunga ktk mkoa mzima labda wilaya moja tu ndio imetofautiana sana na wilaya nyinginezo...
Huko Zanzibar hatuna wasiwasi kabisa CUF watachukua majimbo mengi hivyo kuna advantage kubwa kuwa na wabunge wengi...

Haya swala la mim ikuwauliza viongozi wa CUF, nadhani mkuu wangu utakumbuka kwamba uchaguzi wa tarime nilimpiga madongo, Mrema, Mtikila na Lipumba ambao hawapo hapa kijiweni..laa sivyo ningewauliza wao kuhusiana na huu muafaka wa vyama vya upinzani una malengo gani..

Na mwisho, ni swala la Itikadi.. Mkuu wangu tusijidanganye hapa hata kidogo.. Nimekwisha sema Tanzania na nchii zote za Kiafrika tumevamia Demokrasia kama vile vazi la suti..

Hakuna chama ambacho kina mrengo wa kushoto ama kulia na wanachama wake kweli ni waumini wa mrengo huo..Ndani ya CCM kuna kila rangi iwe Conservative, Liberal au Progressive..Chadema, CUF na vyama vingine vyote bado kabisa hatujaweza kujenga itikadi hizo ktk vichwa vya watu kwa sababu ni itikadi ambazo hazijawekwa ktk matendo..Muda wake bado kabisa itachukua miaka 20 mingine wananchi kuweza kutenganisha tofauti kati ya itikadi mbili ndani ya Ubepari..

Inakuwa kama imani ya Dini tu..tumezipokea kwa kuamini lakini ndani ya waislaam na wakristu kuna watu wasioweza kabisa kufuata maadili ya dini hizo..Zaidi ya hapo kwa maslahi ya wananchi wote sioni sababu ya Waislaam kukataa kuungana na wakristu kama jamii moja kuokoa Taifa linalozama ati kwa sababu tunaamini vitu viwili tofauti..Hivi kweli wewe huwezi kuungana na Muislaam kumwokoa mtu anayekufa maji?.. ati kwa sababu unataka mtu huyo afahamu kuwa wewe ndiye mwokozi!.. damn!..peke yako huwezi kumtoa mtu huyo ktk dimbwi na unafahamu hilo, why even try!..shika miguu mwenzako atashika kichwa swala ni kuokoa Taifa, pia kumbuka swala sio nani ashike kichwa..

This is politics, inayokwenda ndani ya vyama vya Upinzani mkuu wangu tunafahamu hata kama sisi tupo nje... Tazama Kenya, waliungana pamoja na kwamba itikadi zao zilikuwa tofauti lakini baada ya kumwondoa Moi na KANU ndipo wakaanza ugonvi wao wa ndani.. Yes, ugonvi wa Kenya ni funzo jingine kwetu kuangalia kwamba mtu yeyote atakaye chaguliwa nafasi ya rais ni lazima awe religion/tribe free - hasimamii jamii fulani na hasa kabila na dini zetu iwe kinga ya kwanza..Mdini na Mkabila ni rahisi kumchambua toka ktk kundi la viongozi tuliokuwa nao..
 
Mbona mnataka kutoa impression kuwa CHADEMA is a popular party wakati mnajua CHADEMA inasadiwa na vyombo vya habari tena kupitia kelele za akina Mbowe, Slaa, Mnyika na Kabwe. Ukiwaondoa hao anaebakia ni babu Ndesamburo. Hiyo ndiyo CHADEMA. Basi. Sasa linganisha na CCM. Umewahi kumsikia JK akifanya kazi ya Publicity Secretary? Au akipayuka payuka? Why CCM is a popular party whose support and foundation is the masses. Nguvu ya CCM iko ndani ya Chama chenyewe. Ukimwondoa JK, Makamba, Chiligati na wengine CCM ina uhai. It is a system whose engine and power is inherent in itself. CCM haitakufa kwa sababu maumbile yake yana uwezo wa kujiongezea pumzi ya uhai. Someni historia ya Chama hicho. Hakitegemei individuals. Individuals wakienda kinyume nacho hao individuals wanatoswa na chenyewe kinaendelea kudumu. Kwa hiyo jamani msitudangaye hapa kana vile CHADEMA ni chama cha umma. Hakuna kitu.
 
Mkandara,
Dhana yako ya kuachiwa aliyeshika nafasi ya pili nyuma ya CCM 2005 ni potofu. Upepo umegeuka sana kisiasa hasa baada ya kikao cha bajeti 2007. Waulize watu wa CCM watakupa ukweli.
 
Mkuu Mkandara,

Naona unawapigia mbuzi gitaa, unajisumbua bure. Umekomelea kweli msumari hasa kwenye suala la itikadi; vyama vya Tanzania vina itikadi gani? Mwangalie JK ana itikadi gani pale? Vyama vyetu vinaunganisha magenge ya opportunists ambao hubadilika kama kinyonga kufuata kura. Itikadi iliondoka na akina JKN.

Kwenye hizi chaguzi ndogo ndio ulikuwa muda mzuri kwa upinzani kushinda na kujiimarisha. Uchaguzi mkuu zoezi hubadilika kwasababu kunakuwa hakuna resources ya kutosha kuweza ku cover nchi nzima. Kila mtu huenda kupigana vita vyake kwao na hapo CCM kwasababu wao wana resources za kutosha ni rahisi kushinda.

Huu ndio ulikuwa muda muafaka kwa upinzani kuungana ili mwaka 2010 wawakilishwe na mgombea mmoja kwenye kila jimbo. Binafsi ningependa kuwaona akina Mrema, Lipumba, Mbowe, Mbatia na wengine wanachukua forms za kugombea ubunge ili kuimarisha nguvu ya upinzani bungeni. Ebu angalia hawa wakuu wote wangelikuweko kule bungeni kuongezea nguvu za akina Dr. Slaa, Zitto na wengine, huko bungeni kweli kungekalika?

Tatizo kila mmoja wao anataka uraisi ambao watu wengine wote wanajua hawawezi kuupata.
 
Mtanzania,
Hao kina Mrema wangekuwa bungeni leo kitu pekee ambacho kingebadilika ni bei yao!
 
Uchu na uroho wa madaraka.
Kama unaona uko weak mahara furani then kubalianeni nani yuko strong maeneo hayo mumpe kura.Kuliko kufight independently wote mnaishia kushindwa.
 
Back
Top Bottom