Shalom,
Mkuu unazungumzia Ushabiki hapa na sioni kama unatutakia mema sisi wananchi wote.. Kama ni swala la Uanachama wa Chadema basi mimi mkuu wangu kwa taarifa yako mimi CHADEMA tena naweza kusema ni mtu pekee ambaye hana wadhifa wala nafasi ndani ya Chadema na kajitoa wazi hapa JF ukumbini..wengine wote wanajificha chini ya kivuli wanaona sijui aibu!.. au unataka nikwambie kadi yangu namba ngapi! - Mkuu huwa sina kitu cha kuficha na nikiamua kukipaka nakipaka hata kwa ndugu zangu acha Chama..
Sasa turudi kwenye mada, kwanza nilisema kwamba vyma vya Upinzani ili viweze kushinda mikoani ni vizuri (as a suggestion) kama wakiachiana wilaya ambazo mgombea wa chama fulani kashika nafasi ya pili chini ya CCM.. Naposema chini ya CCM nina maana zile sehemu ambazo Upinzani walishindwa na CCM..
Sikusema hivyo kwa sababu labda nimefikiria tu out of blue.. no mkuu wangu nilipitia matokeo ya mwaka 2005, nikaona viti 60 ambavyo Upinzani wangeweza kabisa kushinda kama wangeweka mtu mmoja tu nikichukulia ushindi wa CCM ulikuwa chini ya asilimia 60...I did my homework mkuu wangu...
Sasa inapobakia wagombea wawili tu mara nyingi kunakuwepo na swing vote hivyo ukijumuisha kampeni za vyama vyote vya Upinzani wakiwa pamoja wangeweza kabisa kushinda majimbo hayo..
Kisha ukisha weza kujenga majimbo 60 ya uhakika kupata ushindi ni rahisi kwa majimbo yaliyokuwa jirani ku swing pia kwa sababu nimeona pia matokeo mengi yamekuwa aidha dhaifu au kimbunga ktk mkoa mzima labda wilaya moja tu ndio imetofautiana sana na wilaya nyinginezo...
Huko Zanzibar hatuna wasiwasi kabisa CUF watachukua majimbo mengi hivyo kuna advantage kubwa kuwa na wabunge wengi...
Haya swala la mim ikuwauliza viongozi wa CUF, nadhani mkuu wangu utakumbuka kwamba uchaguzi wa tarime nilimpiga madongo, Mrema, Mtikila na Lipumba ambao hawapo hapa kijiweni..laa sivyo ningewauliza wao kuhusiana na huu muafaka wa vyama vya upinzani una malengo gani..
Na mwisho, ni swala la Itikadi.. Mkuu wangu tusijidanganye hapa hata kidogo.. Nimekwisha sema Tanzania na nchii zote za Kiafrika tumevamia Demokrasia kama vile vazi la suti..
Hakuna chama ambacho kina mrengo wa kushoto ama kulia na wanachama wake kweli ni waumini wa mrengo huo..Ndani ya CCM kuna kila rangi iwe Conservative, Liberal au Progressive..Chadema, CUF na vyama vingine vyote bado kabisa hatujaweza kujenga itikadi hizo ktk vichwa vya watu kwa sababu ni itikadi ambazo hazijawekwa ktk matendo..Muda wake bado kabisa itachukua miaka 20 mingine wananchi kuweza kutenganisha tofauti kati ya itikadi mbili ndani ya Ubepari..
Inakuwa kama imani ya Dini tu..tumezipokea kwa kuamini lakini ndani ya waislaam na wakristu kuna watu wasioweza kabisa kufuata maadili ya dini hizo..Zaidi ya hapo kwa maslahi ya wananchi wote sioni sababu ya Waislaam kukataa kuungana na wakristu kama jamii moja kuokoa Taifa linalozama ati kwa sababu tunaamini vitu viwili tofauti..Hivi kweli wewe huwezi kuungana na Muislaam kumwokoa mtu anayekufa maji?.. ati kwa sababu unataka mtu huyo afahamu kuwa wewe ndiye mwokozi!.. damn!..peke yako huwezi kumtoa mtu huyo ktk dimbwi na unafahamu hilo, why even try!..shika miguu mwenzako atashika kichwa swala ni kuokoa Taifa, pia kumbuka swala sio nani ashike kichwa..
This is politics, inayokwenda ndani ya vyama vya Upinzani mkuu wangu tunafahamu hata kama sisi tupo nje... Tazama Kenya, waliungana pamoja na kwamba itikadi zao zilikuwa tofauti lakini baada ya kumwondoa Moi na KANU ndipo wakaanza ugonvi wao wa ndani.. Yes, ugonvi wa Kenya ni funzo jingine kwetu kuangalia kwamba mtu yeyote atakaye chaguliwa nafasi ya rais ni lazima awe religion/tribe free - hasimamii jamii fulani na hasa kabila na dini zetu iwe kinga ya kwanza..Mdini na Mkabila ni rahisi kumchambua toka ktk kundi la viongozi tuliokuwa nao..