Tukuza hospitality
JF-Expert Member
- Jul 30, 2022
- 321
- 691
Kwa miongo mingi nchi nyingi zinazoendelea, ikiwemo Tanzania, ambazo kilimo ni nguzo kuu ya uchumi, zimekuwa zikitegemea kwa kiasi kikubwa mvua katika kufanya kilimo. Kilimo cha aina hii kilifanikiwa kwa kiasi chake miaka ya nyuma (tuseme miaka ya 1980 na kurudi nyuma), wakati hali ya hewa ikiwa nzuri na misimu ya mvua ikitabirika.
Ukuaji wa viwanda na matumizi makubwa ya rasilimali asili duniani, imepelekea uzalishaji mkubwa wa hewa ya ukaa, ambayo inasababisha mabadiliko ya tabianchi. Kwa mujibu wa jarida la HakiArdhi la Machi 11, 2021, mabadiliko ya tabianchi ni mabadiliko ya hali ya hewa ya muda mrefu katika eneo fulani (mkoa, nchi au bara) tofauti na ilivyozoeleka. Jarida linaendelea kufafanua kwamba, mabadiliko hayo huleta athari katika nyanja za kiuchumi, kimazingira na kijamii, na kwamba ni tatizo linalioikabili dunia katika karne ya ishirini na moja kutokana na athari zake katika nyanja mbalimbali zinazogusa maisha ya binadamu wa kawaida kila siku ikiwa ni pamoja na kilimo na ufugaji.
Kupungua kwa rutuba na mvua katika maeneo mbalimbali nchini, kumesababisha makundi ya wakulima na wafugaji kuhamahama kwa ajili ya kupata malisho, maji na ardhi yenye rutuba; na kupanda kwa gharama za vyakula. Hali hii ya kuhamahama (hasa kwa wafugaji), mbali na kuharibu mazingira, imesababisha migogoro mingi katika maeneo mengi nchini, kutokana na kugombea maji, malisho ya mifugo na ardhi yenye rutuba.
Hali ya Uzalishaji wa Chakula Tanzania
Kwa mujibu wa Jarida la “Vatican News” (Julai 20, 2019), katika mazungumzo na waandishi wa habari tarehe 18 Julai 2019, Waziri wa Kilimo (wa wakati huo), Mheshimiwa Japhet Hasunga (Mb), kuhusu taarifa ya hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula kwa msimu wa 2018/2019 na upatikanaji wake kwa mwaka 2019/2020, alisema hali ya uzalishaji na upatikanaji wa mazao ya chakula nchini Tanzania imeendelea kuwa nzuri katika kipindi cha miaka mitano mfululizo kufuatia uzalishaji wa ziada wa mazao ya chakula kuanzia msimu wa kilimo wa 2013/2014 hadi 2017/2018 ambapo kwa msimu wa 2018/2019 nchi imejitosheleza ikilinganishwa na mahitaji.
Pamoja na mafanikio hayo, Waziri aliendelea kusema, tathmini imebainisha uwepo wa maeneo yenye dalili za upungufu wa chakula kwenye halmashauri 46 katika mikoa 13.
Waziri alisema, katika maeneo yanayopata mvua misimu miwili, mvua za vuli katika maeneo mengi hazikufanya vizuri. Aidha, mvua za masika zilichelewa sana kuanza na hivyo kuathiri shughuli za kilimo katika maeneo hayo. Pili, alisema, kuchelewa kuanza kunyesha kwa mvua na mtawanyiko usioridhisha kwenye baadhi ya maeneo ya nchi yanayopata mvua msimu mmoja.
Kwanini nasema umefika wakati wa kulima kipindi cha kiangazi?
Kwa mujibu wa malezo ya hapo juu, ni ukweli usiopingika kwamba kilimo cha kutegemea mvua hakiwezi kutuvusha katika safari yetu ya maendeleo ya kiuchumi. Simaanishi kwamba mvua sii muhimu, la hasha! Ni muhimu sana, kwani bila mvua vyanzo vingi vya maji (mabwawa, mito, maziwa nk.) vitakauka na hivyo kutatiza maisha ya viumbe karibu vyote; kwani “Maji ni Uhai”. Kutokana na mabadiliko ya tabianchi, mvua zinanyesha kwa kiasi kidogo na kwa wakati usiotabirika, jambo ambalo linasababisha mazao kupungua kwa kiasi kikubwa katika maeneo mengi nchini. Ninachopenda kusisitiza hapa, ni matumizi ya maji yaliyopo chini ya ardhi na vyanzo vingine kufanya kilimo cha umwagiliaji, mara baada ya msimu wa mvua. Kilimo hiki kinaweza kufanywa na wakulima wakubwa na wadogo.
Kilimo cha aina hii kimefanikiwa sana nchini India, na ndio maana pamoja na changamoto zake nyingine, inajitosheleza kwa chakula, na inapata ziada ya kuuza nje ya nchi kila mwaka.
Makingamaji na Shughuli za Maendeleo. Chanzo: “Wikipedia on Watershed Project in India”
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani – FAO (2018), miaka ya 1960, India ilikumbwa na ukame mkali sana, ambao ulipelekea maeneo mengi kukumbwa na baa la njaa. Ndipo serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, pamoja na mambo mengine, ikawezesha wakulima kukarabati makingamaji (“Watersheds”), pamoja na kuhifadhi vyanzo mbalimbali vya maji, kwa ajili ya kilimo.
Mwaka 2012, nilitembelea maeneo mbalimbali ya mashambani nchini India, ambapo nilishuhudia wakulima wadogowadogo wakishiriki katika kilimo cha mazao mbalimbali, ambapo kila mmoja humiliki wastani wa ekari tatu. Wakulima hawa hutumia visima vifupi na virefu, na/au mabwawa kumwagilia mashamba yao kwa kutumia pampu za kawaida. Pia, kupitia vyama vya ushirika, wakulima wengi hutumia trekta kulima na kupalilia; na “combine harvester” kuvuna mazao. Hali hii ndio imeleta mapinduzi ya kijani nchini India, ambapo ina chakula cha kutosha wananchi wake, na cha ziada kinachouzwa nje ya nchi kila mwaka.
Makingamaji husaidia ardhi kufyonza kwa kiasi kikubwa maji ya mvua, badala ya kwenda mbali huku ikisababisha mmomonyoko wa ardhi na kupoteza rutuba ya ardhi.
Makingamaji katika baadhi mashamba nchini India. Chanzo: www.jamkhed.org
Ukilingalisha na India, maeneo mengi ya Tanzania yana vyanzo vingi vya maji; hivyo kilimo cha umwagiliaji kinaweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Serikali iimarishe vyama vya wakulima na kuviwezesha kupata zana za kilimo zikiwa ni pamoja na pampu za kumwagilia maji, trekta nk, ili wakulima wengi wafanye kilimo cha kisasa kisichotegemea mvua.
Serikali na wadau wengine ihimize wakulima kufanya kilimo cha kiangazi, kwa kuwabadili fikra, kwani wengi wanaamini zaidi katika kilimo cha misimu ya mvua tu.
Hitimisho
Kilimo cha kiangazi kitaleta Mapinduzi ya Kijani nchini Tanzania.
Rejea
Erin Gray and Arjuna Srinidhi (Disemba 19, 2013), “Watershed Development in India
(Economic Valuation and Adaptation Considerations)”
HakiArdhi (Machi 11, 2021), Uchambuzi wa athari za mabadiliko ya tabianchi na haki za ardhi kwa wazalishaji wadogo
Jarida la “Vatican News” (Julai 20, 2019), Hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula 2018/2019 na Upatikanaji wake nchini Tanzania.
Ridham Kakar (Septemba 01, 2020), Jarida la “Down to Earth”, “Micro-irrigation: The way ahead for sustainable agriculture”.
Taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani – FAO (2018), “The state of food security and nutrition in the world”.
“Wikipedia on Watershed Project in India”
www.jamkhed.org

Mapendekezo
Serikali iunde timu ya wataalam itakayotembelea nchi zilizofanikiwa katika kilimo cha umwagiliaji wa gharama nafuu, kama India na nchi nyingine za Asia kujifunza na kupendekeza utekelezaji wake nchini.Serikali iimarishe vyama vya wakulima na kuviwezesha kupata zana za kilimo zikiwa ni pamoja na pampu za kumwagilia maji, trekta nk, ili wakulima wengi wafanye kilimo cha kisasa kisichotegemea mvua.

Upvote
13