SoC03 Tunaweza kujilinda dhidi ya utamaduni wa Kimagharibi

SoC03 Tunaweza kujilinda dhidi ya utamaduni wa Kimagharibi

Stories of Change - 2023 Competition

Dubumweuisi

New Member
Joined
Jun 12, 2023
Posts
1
Reaction score
1
Kama ilivyo kwa kila nchi kuwa na sheria na kanuni zake ambazo ni ngumu kukuta kwa nchi nyingine basi hata jamii ina tamaduni zake ambazo zilikuwepo tangu hapo zamani enzi za mababu na mabibi zetu na hazikuwekwa tu bila sababu bali zilitokana ili kuilinda jamii na watu waliomo ndani take dhidi ya mambo mbalimbali ili kuepusha aibu, mikosi, laana na hata mmomonyoko wa maadili.

Kama ilivyo kwa jamii moja huweza kutofautiana na tamaduni za jamii nyingine basi hata bara moja pia hutofautiana tamaduni na bara nyingine mfano; Afrika na Ulaya ni mabara yanayotofautiana na tamaduni kwa kiasi kikubwa.

Turudi kwenye lengo la andiko hili ni kwa namna gani kama jamii tunaweza kujilinda na kuwalinda vizazi vyetu dhidi ya tamaduni za kimagharibi(Ulaya/wazungu) ambazo zimeonekana kuja kwa kasi kubwa na kuharibu vijana na hata watoto wetu wakike kwa wakiume kwa kiwango kikubwa na sio tu ni kinyume cha tamaduni baadhi ya watu wamekuwa wakisema ni kumhasi Mungu baadhi ya tamaduni zao wamekuwa wakizipigia chapuo kupotia mitandao ya kijamii, misaada mbalimbali wanayotoa kwa nchi za kiafrika kwa sharti la kutikiza takwa lao.

Tamaduni za kiafrika hasa jamii za kitanzania ni kuwa "jiwe kamwe halipondi jiwe bali chuma huponda jiwe" hiyo ikimaanisha mwanaume mwenza wake ni mwanamke na kamwe hawezi kuwa mwanaume mwenzie vivo hivyo kwa mwanamke lakini wamagharibi wanajaribu kuteka akili za kizazi chetu kuaminisha kuwa wanayo haki ya kupenda yeyote wanayemtaka hii sio sahihi hasa kwa tamaduni zetu na jamii yetu kwa ujumla kwani ni kupoteza kile walichotuachia mababu zetu na wao wangefanya hivyo sidhani kama hata kama mimi na wewe tungekuwepo duniani kwani kungekuwa hakuna namna wanaweza kuzaliana.

Tunawezaje kuilinda jamii, kuna namna au njia mbalimbali ambazo zinaweza kusaidia kuzuia hili lisitokee na kikakomaa kabisa na lisifanikiwe hata kuingia akilini mwa watoto wetu kwenye jamii zetu ili kulinda na kuenzi hizi tamaduni zetu za thamani;

Kwanza, kuwepo kwa hofu ya Mungu ikiwa jamii yetu kupitia viongozi wa dini zetu mapadri kwa mashekhe watafanya kazi yao kikamilifu kutoa neno la Mungu na kuwafunza watoto wetu ndani ya jamii basi watakuwa wakiwa na hofu ya mungu na kuogopa kufanya na kukubali tamaduni za magharibi huku wakijua ni kosa na dhambi kufanya hivyo hii itasaidia kwa kiasi chake.

Pill, kijana na mtoto wa kiume afundishwe thamani yake na nafasi yake kwenye jamii kuwa yeye ni mtu wa aina gani anatakiwa kuishi vipi baadae atakuja kuwa baba wa familia ikibidi aoneshwe mfano wa baba yake tumfanye mtoto wa kiume aone fahari kuzaliwa mwanaume atamani kuwa mwanaume kila Siku atamani kuwa baba sikumoja hii itasaidia kumlinda na hizi tamaduni mbaya kutoka magaharibi dhidi yake.

Tatu, mtoto wa kike au binti aijue thamani yake kama mwanamke hii itamfanya kujiona watahamani mbele ya mwanaume tumfanye binti huyu atamani kuitwa mama siku za usoni, afundishwe shughuli au kazi za nyumbani zinazomuhusu mwanamke apewe mafunzo ya kike atakapofikia umri wa balehe kama baadhi ya makabila yanavyofanya hili litaweza kuilinda jamii yetu ipasavyo dhidi ya tamaduni zinazotaka kuiharibu jamii.

Nne, wazazi wazungumze na watoto wao kama mzazi unawajibu mkubwa kumlinda mtoto wako haijalishi hauna muda wa kutosha kukaa na familia jitahidi unapopata zungumza na watoto wako kuhusu maisha kuwa rafiki kwa watoto wako watakuambia yanayowasumbua mapema na utaweza kuzuia haraka zaidi waambie watoto wako ukweli usiwafiche kuwa dunia sasa imebadilika hivyo wanapaswa kuwa makini kwa kila wanachokifanya wawapo sehemu yeyote na wasimuamini mtu yeyote kirahisi kwani tuanashuhudia watu wa karibu ndio wanaharibu vijana na watoto kwa kuwalawiti watoto wa kiume na kuwabaka inafika hatua mzazi unakuja kugundua hatua za mwisho mtoto hawezi kupona tena kwa kufanya hivyo litasaidia sana kudhibiti tamaduni hizi za kimagharibi.

Tano, matumizi mazuri ya utandawazi hasa kwenye hii mitandao ya kijamii vijana wengi hutamani na huvutiwa kwa vitu mbalimbali wanavyoviona huko na wengine hujaribu kutaka kufanya kwani kama nilivyosema hapo awali hutumia njia za utandawazi kupenyeza tamaduni zao hivyo kama hutakuwa makini unaweza kuingi mtegoni kirahisi basi kama wazazi na familia tuwalinde vijana na watoto wetu kutumia utandawazi kwa natumizi chanya kama kutafuta maarifa na mengineyo yanayofaa kwani hata hizi Cartoon(vibonzo) baadhi yake vimekuwa vikishinikiza tamaduni hizo za kimagharibi kuhusu ushoga na usagaji ambazo ni kinyume na tamaduni, mila na desturi zetu.

Sita, yote kwa yote kama jamii kwa kushirikiana na serikali inabidi itolewe elimu ya kutosha kila uchao bila kusita kuhusu jamabo hili itasaidia kuwa na uelewa mpan kwa watoto wetu wakikuwa huku wanaelewa madhara ya hizo tamaduni za kimagharibi kuwa ni mbaya na hazifai kwa jamii yetu.

Baada ya kusema hayo hili janga ni letu sote kama taifa na jamii kwani linazidi kuja kwa kasi ulimwenguni na hakuna wakututoa humo isipokuwa sisi wenyewe tunahitaji kusimama imara tena zaidi ya imara ili kupinga hili kila mmoja alichukulie kwa uzito endapo litaikumba familia yake au litamkuta mtoto wako wa kiume pekee uliyetamani siku akuletee mjukuu uitwe babu au bibi inaumiza sana.

Tunapaswa kuweka nguvu ya ziada elimu izidi kutolewa kuhusu tamaduni zetu zikoje vizazi vyetu vijivunie tamaduni zao na kuzilinda na hili tutaweza endapo tutaelezana ukweli kama taifa na jamii na kuwaeleza ukweli hao wamagharibi kuhusu msimamo wetu licha ya kuwa wataweka vikwazo lakini sikuzote umoja hushinda.

Tulinde jamii yetu, tulinde vizazi vyetu, tulinde tamaduni zetu, kwa pamoja tunaweza kufanikisha hili. Mimi, wewe, yule kwa pamoja sote tunaweza kuwalinda vijana wetu wakiume na wakike na kufanya yale yanayompendeza Mungu na kuenzi tamaduni zetu
 
Upvote 1
Back
Top Bottom