Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,476
Mambo vp JamiiForums
Sasa tunalo kombe la mapinduzi kwa vilabu kutoka Tanganyika na Zanzibar, kwanini tushindwe kuwa na kombe la muungano (April 26) mechi moja tu kwa timu za taifa za bara (Tanganyika) na visiwani (Zanzibar) kwa wachezaji wa ligi za ndani tu? Lilianza mwaka 1982 na kufa mwaka 2003.
Timu ya taifa ya Zanzibar
=====
Ninasema ni kombe la muungano kwa wachwzaji wa ligi za ndani nikiwa na maana mchezaji wa Zanzibar anayecheza ligi ya Tanganyika hatoitwa katika kikosi cha timu yake ya taifa na vivyo hivyo kwa mchezaji wa Tanganyika anayecheza ligi kuu ya Zanzibar.
Tunataka kuona viwango combination ya vijana wa Malindi, Mlandege, K.M.K.M, Kipanga na Jang'ombe Boys wakiwa wanacheza kwa pamoja. Ni wachezaji wa vilabu vya ndani tu, akina Samatta hatutawaita katika muktadha huu
HISTORIA NDOGO YA KOMBE LA MUUNGANO
==========
Ligi ya Muungano ilianza rasmi mwaka 1982 lengo ni kudumisha Muungano wetu na kutoa usawa wa kiuwakilishi katika michuano ya kimataifa ya vilabu, hii ni kutokana na Tanzania bara kuwa na ligi yake na Zanzibar kuwa na ligi yake.
Upande wa pili (Zanzibar) ukiwa sio mwanachama wa shirikisho la soka barani Africa caf, hivyo kukosa sifa ya timu zake kushiriki michuano ya vilabu bingwa africa na kombe la washindi (ilijulikana hivyo miaka hiyo).
Kwa kuwepo kwa ligi ya Muungano ambayo ilikuwa inajumlisha timu 3 zilizomaliza nafasi juu kwenye ligi husika basi timu kutoka Zanzibar nazo zilipata nafasi ya kuiwakilisha Jamhuri ya Muungano kwenye michuano ya CAF.
Moja ya timu iliyofanya vizuri sana kimataifa katika uhai wa miaka 21 ya michuano hiyo kwa upande wa Zanzibar ni timu ya Malindi.
Leo hii ni miaka 18 sasa tangu michuano ya ligi ya Muungano ife, michuano ambayo ilifanyika kwa miaka 21 mfululizo. Lakini kama wasemavyo wahenga "Tumbo la shari huzaa kheri" kwa namna moja iliwafungua macho Zanzibar kuomba uanachama CAF ili vilabu vyake vishiriki michuano ya kimataifa.
Sababu michuano hii ilikuwa inafanyika December nimeona sio vibaya tukakumbushana kidogo. Pale ambako unaona rekodi hazipo sawasawa unaweza kuwasiliana nami.
==========
SWALI: Tunaweza kuwa na kombe la muungano (April 26) kwa timu za taifa za wanaume bara (Tanganyika) na visiwani (Zanzibar) kwa wachezaji wa ligi za ndani tu?
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.