SoC02 Tunawezaje kupata utawala bora

SoC02 Tunawezaje kupata utawala bora

Stories of Change - 2022 Competition

Rebecca97

Member
Joined
Aug 30, 2022
Posts
6
Reaction score
4
TUNAWEZAJE KUPATA UTAWALA BORA?

Hakuna namna eneo lolote linaweza kujiendesha lenyewe bila uwepo wa utawala kuanzia ngazi za chini za kitongoji mpaka za kitaifa.Uwepo wa utawala ni wa muhimu sana ili kuhakikisha kuwa shughuli zote zinazofanyika katika eneo husika zinaenda sawa chini ya usimamizi wa mamlaka fulani.Lakini suala sio tu kupata utawala bali utawala bora ambao ndio unahitajika ili mambo yote yanayoendelea katika eneo husika kuwa katika hali salama.Sasa basi kabla hatujasonga mbele ni muhimu kujua nini maana ya utawala na huo utawala bora.

Utawala ni matumizi mamlaka fulani inaweza kuwa ya kisiasa ,kiuchumi au vyovyote vile katika kusimamia shughuli zinazoendelea katika nchi kwenye ngazi zotee au tunaweza kuutafsiri kama utaratibu wa kutumia madaraka ya umma katika kusimamia rasilimali za nchi ili kuinua hali za maisha za watu na utawala bora ni ule ambao unafuata kanuni na sheria zilizopo bila kuzivunja.

Tumeona nchi nyingi zikilia na kuomboleza kwa sababu tu ya ukosefu wa utawala bora,kuna mataifa leo yapo katika hali mbaya za kivita ,kiuchumi yote kwa sababu ya ukosefu wa utawala bora .Sasa swali la muhimu sana la kujiuliza na kulijua ni “Je tunawezaje kupata utawala bora kuanzia ngazi za chini mpaka za kitaifa?”

Uwepo wa uadilifu katika utendaji.Uadilifu ni hali ya kufanya kazi au jambo ulilopewa kulifanya kwa uaminifu mkubwa ,uadilifu ni kusema wengine kwanza mimi baadae yaan kutanguliza na kujali maslahi ya wengine .Niseme tu kwamba hakuna namna nchi yetu inaweza kupata utawala bora ikiwa tu watawala wenyewe wameshindwa kuwa waadilifu katika utendaji wao wa kazi.Ikiwa viongozi watajali kuendelea kujirimbikizia mali za serikali kwa manufaa yao binafsi ,kuchukua rushwa za pesa kutoka kwa wanachi na kuwagandamiza wananchi walio chini basi kauli ya utawala bora ni bora tuisahau katika akili zetu.Ni lazima viongozi wakubali kujikana wenyewe na kujitwika jukumu la kuhakikisha wanatumikia nafasi walizopewa kwa uaminifu mkubwa bila kujali hali zao kibinafsi (kiuchumi ) zikoje kwa wakati huo.

Kutanguliza demokrasia,neno hili linamaanisha uhuru .Namshukuru Mungu kuwa hapa kama taifa tumevuka kwa sehemu kwani tunao uhuru wa kuwapa wananchi kumchagua nani wanamtaka kupitia uchaguzi ,lakini nadhani hili linapaswa kufanyika kwa mapana zaidi kama tunatamani kuona nchi inapiga hatua hakika unahitaji uhuru kuachiliwa mikononi mwa wananchi ili waweze kuwa na uwezo wa kukosoa endapo wanapoona serikali haiendi sawa kwani hii itasaidia sana kama serikali kujua wapi imeshindwa kuwajibika ipasavyo na hatua gani ziongezwe kuhakikisha inafanya majukumu yake vyema lakini wananchi wapewe nafasi ya kushiriki katika kufanya maamuzi.

Pia uwazi wa mambo,suala la mipango,mikakati,matumizi yote yanapaswa kuwekwa wazi kwa wananchi ili kujua utawala ulioko juu yao umefikiwa wapi.Hii itasaidia sana wananchi kujitoa zaidi kushirikiana na serikali lakini kuwapa imani dhidi ya viongozi wao.Ni muhimu watawala (viongozi ) kuwa wa kweli na wa wazi katika suala zima linalohusu suala la fedha za wananchi kama vile zinazotumika katika ujenzi wa shule,vituo vya afya na vinginevyo lakini pia wananchi waweke bayana juu ya uwepo wa huduma zitolewazwo bure na zile zinazolipiwa.

Vile vile ni kuhakikisha uwajibikaji wa viongozi,kiongozi yoyote natamani ajue kuwa uongozi sio kuhusu kutumikiwa bali ni kutumika kwa ajili ya wengine.Kwahiyo kiongozi anapopewa mamlaka fulani ya kutawala inamaanisha kuwa amekubali kuwa mtumwa wa watu walio chini yake,lazima watawala (viongozi) wakubali kubeba majukumu yao ipasavyo kama tunahitaji kuona nchi yetu ikiwa katika hali ya utawala bora.Uongozi sio wa masaa kadhaa bali ni wa muda wote yaan asubuhi ,mchana mpaka usiku ,kiongozi yoyote anayedhani anatumika kwa masaa fulani tu awapo ofisini basi hawezi kutufikisha kwenye utawala bora tunaouhitaji .Ni lazima kiongozi awe tayari kupatikana na kuwatumikia wananchi wake hata kama hajisikii kufanya hivyo kwa wakati huo ,ni lazima akubali kuweka ubinafsi wake pembeni na kutazama mambo yanayohusu majukumu yake kwanza.Kama viongozi wote wakilijua na kulifanyia kazi hili basi hakika tutaishi katika taifa lenye utawala bora kwa asilimia mia moja.

Lakini pia tunahitaji usawa wa kuheshimu sheria,kuna kauli fulani ambayo watu hupenda kuisema sana .Kauli isemayo “hakuna aliye juu ya sheria,wote tupo chini ya sheria” .Ni msemo ambao huenda watu wengi hawautilii maanani lakini una maana kubwa sana kama tunatamani kuona tunakuwa chini ya utawala bora.Ni lazima watawala waelewe kuwa hata wao wako chini ya sheria hivyo ni jukumu lao kuheshimu sheria zilizowekwa kulingana na majukumu yao(sheria za nchi) ,hii itasaidia pia kupunguza suala la rushwa za ngono,unyanyasaji wa wanachi,upigaji wa wananchi na ugandamizaji dhidi yao.

Nimalize kwa kusema kwamba hatuwezi kuupata itawala bora ikiwa kama taifa viongozi /watawala wamekosa vigezo hivyo hapo juu ,ni lazima wahakikishe wanatimiza hayo na mengine mengi ili kutufanya wananchi kuwa chini ya utawala tutakaoufurahia na kunufaika nao.Suala la utawala bora hakuna ambae asiyetamani kuona unafanya kazi kwenye jamiii yetu kwani kupitia huo ndipo tunapata maendeleo kama taifa na ngazi zote kwa ujumla (kwa mfano viongozi wote wakawa waadilifu bila kuiba mali za umma hakika pesa zote zitatumika kufanya mambo ya kimaendeleo) na kupungunza umaskini.Pia utawala bora unasaidia kuleta amani na utulivu kwenye maeneo husika kwasababu kutakuwa hakuna uvunjaji wa sheria ,unyanyasi wa sheria na maovu mengi kwahiyo watu wote tutaishi kwa amani.Utawala bora ndio utakaofanya heshima iwepo juu ya haki za binadamu kwani kila mtu atatambua kuwa hayuko juu ya sheria bali chini yake.

Nashauri sana watanzani wenzangu wote hasa viongozi ni vyema kuwa na maono makubwa yanayohusu utawala wao ,muelekeo thabiti wa kutamani kuona nchi (eneo wanalotawala) linafika mbali tayari kujenga mawasiliano mazuri na watu mnaowatawala ,kuwahamasisha watu kujitoa kwenye shughuli za kijamii kama mikutano na kuwapa matumaini hasa katika nyakati ngumu.
 
Upvote 13
Kama ukiguswa na ujumbe wangu tafadhali usipitie bila kunipa kura yako kwa kubonyezqma kidude chenye alama hii [^] chenye rangi ya kijani chenye ya makala yangu…
 
Unastahili update kipindi kwenye television ya taifa ili Jambo hili ulivyolielezea kwa upana liwafikie na wengine kwa njia ya tv (THANK YOU)
 
Back
Top Bottom