Tunawezaje kuwalinda watoto wetu dhidi ya maudhui yasiyofaa kwenye TV?

Tunawezaje kuwalinda watoto wetu dhidi ya maudhui yasiyofaa kwenye TV?

Shanily

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2024
Posts
856
Reaction score
1,662
Kama mjuavyo teknolojia ilivyotaradadi Kila Kona ya Duniani. Utazamaji wa Television (TV) umekuwa haukwepeki.

Shida katika maudhui yanayorushwa kuna maudhui yasiyofaa kuangalia na vijana wetu ambao Bado hawajajua kuchanganua mambo.

Kuna muda unataka uangalie zako tamthilia nawao hao wapo hapo hapo wanakodoa.

Hata hizi katuni ambazo tunawawekea napo Kuna maudhui yasiyofaa, ukisema ufungie Yako, kwa jirani zipo zinafungiuliwa na huwezi wafungia ndani.

Hivi tunawalindaje vijana wetu hawa?
 
Sikuhizi waafrica wamekuwa wapumbavu sana, Takataka za hovyo tulizo zoea kuzisikia kwa wazungu na waarabu, sasa waafrica wanaiga na kuonyeshana kwenye tv
Yaani ni tafrani hasa hzi tamthilia hzii😢
 
Nunua Tv yako weka chumban, hiyo ya seblen set channels zinavyoangalika tu, kama channels za michezo, wanyama na katuni za kulingana na umri wao basi, wakataze watoto wake kwenda kwa majirani dunia sio nzuri hii, weekends pendelea kuwapeleka sehemu za mazoezi na michezo ili wawe active na wasipate muda wa kuangalia Tv sana.
Kwisha kazi
 
Ondoa CCM madarakani, kila kitu kinawezekana
Kwani CCM ndo wameleta maudhui yaliyopo ndani ya hzo TV!?.

Alaumiwe alotutoa analogy kutuleta digital, analogy kulikuwaga hakuna vimbwanga vingi kwenye Tv kma sasa
 
Sio lazima pia kuwa na TV, habari zote unazipata kwa simu yako. Hela ya TV unaweza nunua kinanda, guitar, vitabu, computer za watoto n.k.
Wewe unaweza usinunue, jirani yako nae utamzuia!?. Maana watoto wanacheza kwingi huwezi mzuia ndani tu.
 
Nunua Tv yako weka chumban, hiyo ya seblen set channels zinavyoangalika tu, kama channels za michezo, wanyama na katuni za kulingana na umri wao basi, wakataze watoto wake kwenda kwa majirani dunia sio nzuri hii, weekends pendelea kuwapeleka sehemu za mazoezi na michezo ili wawe active na wasipate muda wa kuangalia Tv sana.
Kwisha kazi
Hv kweli Marine hz watoto wanatoka wanaenda kwa majirani serious serious serious kufanya nn dah tunatofautiana mm naishi useaz bt akitoka shule ndan week end kama hakuna kaz maalum ndan hao wako wakubwa na wadogo hawana rafiki mnawezaje kutoa watoto out of your control
 
Wewe unaweza usinunue, jirani yako nae utamzuia!?. Maana watoto wanacheza kwingi huwezi mzuia ndani tu.
Unaweza kumzuia, akitoka shule ni homework, kucheza mpira anarudi nyumbani. Na mtoto kizazi hiki unamruhusu aende kwa jirani kweli!!!
 
Hali ni ya hatari na mbaya sana siku hizi tunalipia fees wazazi kwa Furaha kabisa kila mwezi watoto wetu wajifunze uhuni. Kwa jina la king'amuzic Subscription
Shida wanayabeba kma yalivyo na kwenda kufanya majaribio kwa wayayoyaona
 
Hv kweli Marine hz watoto wanatoka wanaenda kwa majirani serious serious serious kufanya nn dah tunatofautiana mm naishi useaz bt akitoka shule ndan week end kama hakuna kaz maalum ndan hao wako wakubwa na wadogo hawana rafiki mnawezaje kutoa watoto out of your control
Hapo unaminya mwanao kukua kiakili, kuchanganyika na wenzie Kuna faida kiakili kwa mtoto , anakuwa mchangamfu
 
Ni vizuri kustuka namna hii. Siku hizi hata kuangalia movie kunapungua unaona bora utandike documentaries tu
 
Ni vizuri kustuka namna hii. Siku hizi hata kuangalia movie kunapungua unaona bora utandike documentaries tu
Kabsa kwa hali ilivyo sio poa kbsaa, tutaishia kuangalia Tanzania Safari channel basi
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Mm natumia Netflix pekee nyumbani, hivyo kuna account za watoto tu, na za Dad.
Nimarufuku nimkute mtoto ameingia kwenye account yangu a Dad. Fullstop......
Ila Netflix ni wachafu kwenye account za Dad, yaani Movies zao kila kipande lazima washikane
 
Back
Top Bottom