Tunayopenda Tusahau

Mbussi,
Umesema kweli niliipenda CUF si kwa Uislam tu bali kwa kuwa haikuwa na uadui na Waislam.

Kuhusu hayo mengine siwezi kuyazungumza kwa kuwa yeye hapa hayupo.

Ni "ovyo" ndiyo Kiswahili safi si "hovyo."
Said, kwanza Asante kwa sahihisho. Ni kweli nina tatizo kwenye matumizi ya "h". Lakini vilevile jf inasomwa na kila mtu hivyo huwezi kusema Lipumba hayuko humu. Ni bora tu Prof. apokee ushauri itamsaidia ktk harakati zake za kisiasa.

Udini ni cancer inayoitafuna jamii. Nakushauri utoke huko, dini ibaki misikitini na makanisani na siyo kwenye vyama vya siasa na taasisi nyingine za umma. Hii ndiyo sababu nakumbuka umuhimu wa Nyerere aliyelikemea na kukataa udini kwa nguvu zote ktk serikali yake, japo wewe na wahafidhina wengine wa Uislam mnalikataa hilo. Vilevile Magufuli alikuwa akiandamana na viongozi wa dini na madhehebu yote bila kubagua. Nashangaa kuona haya mambo ya udini yamekuwa yakiibuka hasa inapotokea kiongozi wa juu ni Muislam. Tuliona kwenye utawala wa mzee Mwinyi na kwa kiasi fulani kwa Kikwete pia. Radio zenu hasa radio Iman, duuh vingine ni kunyamaza tu.

Kwenye uongozi wa Samia imekuwa ni agenda. Tumeona ilivyokuwa kwenye sakata la bandari, na hadi sasa wanaibuka akina Mwaipopo kuhubiri udini. Wewe pia kwenye post zako nyingi ni udini mtupu. Hapana, Katoliki na Ukristo havina ugomvi na Uislam japokuwa mnatuita Makafiri.
 
Mbussi,
Umesoma kitabu cha Abdul Sykes?

Kuhusu Prof. Lipumba mimi siwezi kumjadili na yeyote kwani lililopita halidhuru.
 
Mbussi,
Umesoma kitabu cha Abdul Sykes?

Kuhusu Prof. Lipumba mimi siwezi kumjadili na yeyote kwani lililopita halidhuru.
Said, sijakisoma hicho kitabu na sidhani kama nina huo mpango wa kukisoma. Historia uandikwa na watu kukuhusu wewe, na wewe mwenyewe huwezi kujiandikia historia inayokuhusu wewe hiyo itakuwa ni CV. Hichi kitabu inavyoelekea kimeandika mambo yanayowahusu Waislam, kwangu mimi ukishabagua tu kwa msingi wowote wa kidini siyo mvumilivu wa hayo mambo.

Kama Sykes ameandika kwa msingi ya utaifa naweza shawishika kusoma, lakini kama ameandika kwa malalamiko ya Waislam kubaguliwa na utawala wa Nyerere kwasababu ya ukristo wake, utaniwia radhi.

Kuna andiko mzee Said ulilokuwa ukilalamikia serikali ya Nyerere kuwanyima ruhusa mashirika ya Kiislam ikiwemo OIC kujenga vyuo vikuu, kama kweli ilikuwa hivyo. Ninaelewa sasa ni kwanini Nyerere aliona mbali na kufanya hivyo. Na ndiyo maana hata Shule na Hospital zizokuwa zikimilikiwa na kuendeshwa na madhehebu ya kikristo alizitaifisha.
 
Mbussi,
Hapana tatizo kama umeamua hutaki kukisoma.

Kitabu hiki kipo katika kundi la vitabu vinavyoitwa, "Corrective," yaani kitabu kinachoandikwa kusahihisha yale yaliyoandikwa lakini yana makosa.

Huku ndiko kulikofanya kitabu hiki kiingizwe katika Cambridge Journal of African History.

Mabingwa wa African History: John Iliffe, Jonathon Glassman na James Brennan wakaandika mapitio na kuchapwa katika jarida hilo.

Hawa ndiyo wakakifanya kitabu hiki kisomwe vyuo vyote kama kitabu cha rejea katika Political History ya Tanzania na katika maisha ya Julius Nyerere.

Kitabu kikawa maarufu na mwandishi akawa pia maarufu.

Hapa nyumbani Prof. Haroub Othman akazungumza na Mwalimu akamwambia kitabu cha Abdul Sykes kimebadili historia ya uhuru wa Tanganyika na kimebadili historia yake na "legacy," yake pia.

Haya yanatosha.

Ila nasikitika kuwa kwa hali yako ilivyo itakuwa mimi napoteza muda kujadiliana na wewe kwa kuwa huna unachokijua katika historia ya uhuru wa Tanganyika na hauko tayari kujifunza.

Prof. Haroub ni mwalimu wangu Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam lakini katika historia hii ya wazee wangu alikubali kuwa mwanafunzi wangu na akajifunza yale ambayo hakuwa anayajua.

Alichokifanya ili Tanzania iwe na historia ya kweli ya uhuru wake alimuomba Mwalimu akubali utafiti mwingine ufanywe kuhusu maisha yake.

Mwalimu alikubali.

Mimi nilihojiwa na Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Yahya Othman na Dr. Ng'wanza Kamata wakati wa utafiti wa kitabu cha maisha ya Julius Kambarage Nyerere.

Katika kitabu hiki ndani wameandika kuwa Maktaba yangu ni kati ya maktaba tatu zilizosheheni taarifa za Mwalimu Nyerere wakianza na maktaba ya Dr. Salim Ahmed Salim, Mohamed Said na Brig. Hashim Mbita.


Kitabu cha Mwalimu Nyerere nilichotunukiwa kwa mchango wangu katika uandishi wake.

Nikihojiwa nyumbani kwangu na Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Yahya Othman na Dr. Ng'anza Kamata

Kitabu cha maisha ya Abdulwahid Kleist Sykes (1924 - 1968) na kitabu cha maisha ya Julius Kambarage (1922 - 1977) vikiwa katika Maktaba


 
Mzee Said, sijakuelewa. Unasema mwal. Nyerere alikubali ili utafiti ufanyike kuhusu historia ya maisha yake yeye mwenyewe au maisha ya mtu mwingine!! Mbona kichekesho. Kwamba yeye Nyerere hakujua jinsi alivyozaliwa, makuzi yake, shule, harakati za Uhuru hadi maisha yake kama Rais mpaka alipostaafu?

Hapa ndipo nakuona bias. Sykes akiandika kitu kuhusu maisha yake binafsi unataka watu tuamini, lakini kwa Nyerere mliitaji utafiti tena wakati bado akiwa hai, si mungemuuliza tu yeye mwenyewe, au alikuwa haaminiki?
 
Mbussi,
Nimekuambia kuwa hapana haja ya mimi na wewe kuendelea na mjadala huu.

Nimekueleza yaliyotokea na ikiwa huniamini hakuna tatizo.
Hujaridhika umerejea kwangu na maswali.

Naam Mwalimu Nyerere alikubali historia yake iandikwe na alimuagiza Prof. Haroub Othman aunde kamati na yeye ataieleza hiyo kamati maisha yake.

Kitabu cha Mwalimu Nyerere kisingeweza kuandikwa kama yeye asingeridhia.

Katika kamati Ile mjumbe mmoja alikuwa Prof. Ahmed Muhidin ambae mimi nilizungumzanae nyumbani kwake Kikambala, Mombasa na akanieleza yote jinsi Mwalimu alivyomuomba ashiriki katika utafiti na uandishi wa maisha yake.

Bahati mbaya kamati hii haikupata kukutana kwa kuwa Mwalimu alikuwa mgonjwa akafariki na Prof. Haroub nae pia akafariki.

Nataka nikueleze kitu kimoja ukielewe.

Aliyeandika maisha yake ni Kleist Sykes (1894 - 1949) baba yake Abdul Sykes na aliandika kabla hajafariki mwaka wa 1949.

Unaweza kupata kwanza paper aliyoandika Aisha ''Dasy'' Sykes Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, East African kutokana na mswada wa babu yake: ''The Life of Kleist Sykes'' Ref. No. JAN/HIST/143/15 (1968).

Baadae hii paper ikiwa sura katika kitabu alichohariri John Iliffe, ''Modern Tanzanians,'' (1973) ''Kleist Sykes: The Townsman.''

Mimi ndiye nikaja kuandika kitabu: ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,'' Minerva Press, London 1998.

Mimi siye niliyeshauri kitabu cha Mwalimu kiandikwe na Prof. Haroub Othman yeye ndiye aliyetoa wazo hilo kwa Nyerere akamwambia kuwa kitabu changu kimebadili historia ya uhuru wa Tanganyika na historia yake.

Nyerere alikuwa amesoma kitabu changu tayari wakati anazungumza na Prof. Haroub kwa hiyo alikuwa anajua kiwango cha masahihisho niliyofanya kuhusu mchango wake katika kuunda chama cha TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika:


Tanganyika Standard 20 October 1968


Na Prof. Ahmed Muhidin nyumbani kwake Kikambala, Mombasa​

Mbussi,
Soma machache niliyoandika baada ya kuonana na Prof. Muhidin:

''Prof. Muhidin ni mwingi sana kupita kiasi.

Yeye ndiye aliyenigusia kuhusu uhusiano wa Mwalimu na Prof. Mazrui na kunieleza kuwa Mwalimu alikuwa na chumba chake pale nyumbani kwake Msasani ambacho funguo zake akikaa nazo mwenyewe kibindoni na chumba hiki haingii mtu mwingine ila wale wandani wake, yaani wale anaowapenda kama Prof. Muhidin.

Prof. Muhidin akaninong'oneza kuwa baada ya kutoka Ikulu Mwalimu alimuomba amsaidie kuandika historia ya maisha yake.

In Shaa Allah hiki ni kisa cha kujitegemea ikipatikana fursa tutakizungumza.''
(2020)
 
Mauaji ya mwembe chai yalikuwa 1998, ya 2001 ilikuwa ni Pemba baada ya uchaguzi wa 2000
 
Mauaji ya mwembe chai yalikuwa 1998, ya 2001 ilikuwa ni Pemba baada ya uchaguzi wa 2000
Sawa, ni muda mrefu umepita nilichanganya. Mkapa aliingia madarakani 2000, Mwembechai alikuwa Mwinyi.
 
Ok Said, nimekuelewa kwamba historia ya Nyerere "Rais wa nchi" kuandikwa iliitaji kuundiwa kamati wakati wa uhai wake, lakini paper moja tu kutoka kwa mwanafamili Aisha "Dasy" Sykes ilitosha kuandaa vitabu kadhaa vya maisha ya familia ya Sykes ambao tayari walikuwa marehemu na uhusika wao kama Waislam ktk kupigania Uhuru.
 
Mbussi,
Hapana.
Paper ya Daisy ni maisha ya babu yake Kleist Sykes (1894 - 1949) na haikusababisha kuandikwa kwa vitabu kadhaa.

Kitabu changu kinamweleza Kleist Sykes na Abdul, Ally na Abbas Sykes kuanzia 1942 Abdul na Ally walipojiunga na KAR na kinatokana na Nyaraka za Sykes.

Nyaraka hizi zina taarifa nyingi pamoja na taarifa za Julius Nyerere na ndizo nilizotumia kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Wakati naanza utafiti 1980s Nyerere alikuwa hai halikadhalika Ally na Abbas Sykes na wazalendo wengine ambao niliwahoji.

Nyerere kakisoma kitabu pamoja na watu wengi ndani ya serikali na CCM.

Kitabu kiliwasisimua.

Hilo swali la historia ya Nyerere kuundiwa kamati mimi halinihusu.

Umesoma kitabu cha Julius Nyerere?
 
Mzee Said,
Tuachane na hii mada. Labda tuambie, je, maandamano yenu na Sheikh Ponda Issa Ponda kuhusu ya kichoendelea kwa Waparestina yalifanikiwa?
 
Mzee Said,
Tuachane na hii mada. Labda tuambie, je, maandamano yenu na Sheikh Ponda Issa Ponda kuhusu ya kichoendelea kwa Waparestina yalifanikiwa?
Mbussi,
Kitu gani kimekufanya wewe useme maandamano ya Palestina yananihusu mimi na Sheikh Ponda?

Nakushauri endapo unapenda kujua habari za Palestine na Tanzania fungua uzi mpya In Shaa Allah nitakuja.

Nimeandika mengi kuhusu Palestine.
Niko tayari kutoa darsa sote tunufaike.

Hapa si mahali pake.



Wanafunzi wa State University of Zanzibar (SUZA) wakifuatilia mada yangu kuhusu Palestine 2017​
 
Mzee said,
Kama mliomba ridhaa kutoka kwake ili muandike historia yake ilikuwaje baba yake Abdul aandike historia hiyo?
Ni kwamba mzee kleist sykes alipata ruhusa?

TUtamini vipi stori hii haina bias yoyote wakati mwalimu aliumwa na kufariki?
 
Mzee said,
Kama mliomba ridhaa kutoka kwake ili muandike historia yake ilikuwaje baba yake Abdul aandike historia hiyo?
Ni kwamba mzee kleist sykes alipata ruhusa?

TUtamini vipi stori hii haina bias yoyote wakati mwalimu aliumwa na kufariki?
Passion...
Mimi sikuhusika na utafiti na uandishi wa kitabu cha Julius Nyerere kwa hiyo usinijumuishe, ''mliomba ridhaa...''

Kwangu walikuja niwaeleze historia ya Nyerere toka alipofika Dar es Salaam na kupokelewa na wenyeji wa Dar es Salaam.

Walinihoji mara mbili na niliwapa baadhi ya Nyaraka za Sykes na picha kutoka Maktaba ya Picha ya Sykes.

Aliyeomba ridhaa ya Nyerere ni Prof. Haroub Othman.
Kleist Sykes yeye aliandika maisha yake kabla hajafa 1949.

Mswada huu ukaja kuwekwa wazi na mwanae Abdul Sykes mwaka wa 1968
alipomkabidhi bint yake Daisy ili akamilishe assignment aliyopewa na John Iliffe mwalimu wake wa historia University of East Africa.

Kuhusu ''bias'' kitabu hiki cha Mwalimu Nyerere kimempamba Mwalimu akapambika hakuna baya lililosemwa kuhusu yeye.

Waandishi wa kitabu hiki waliongozwa na Prof. Shivji.


Nyarala ya Sykes

Kulia Lawi Sijaona, Abdul Sykes, Julius Nyerere na Dossa Aziz
Ukumbi wa Arnautoglo dhifa ya kumuaga Nyerere safari ya pili UNO 1956


 
2001 ni mauaji ya waandamanaji kupinga wizi wa kura Katika uchaguzi wa 2000 kule Zanzibar.Kilikuwa kipindi Cha Mkapa sema Mkapa alikuwa amelazwa Ulaya,hakuwepo nchini.
 
Historia ni taaluma ,historia ni sayansi.Historia siyo masimulizi lazima ufanye utafiti ili uandike historia.
 
Mzee wetu, Mohamed Said, kuna platform yeyote ilipo historia uliyoandika (documents, audio or visual) inayohusu Palestine na mzozo wake Middle East?

Mimi natamani kujifunza, kama naweza kupata darasa lako nitashukuru,

NB: Mimi ni mwanafunzi wako kwenye jukwaa hili,Asante!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…