Said, kwanza Asante kwa sahihisho. Ni kweli nina tatizo kwenye matumizi ya "h". Lakini vilevile jf inasomwa na kila mtu hivyo huwezi kusema Lipumba hayuko humu. Ni bora tu Prof. apokee ushauri itamsaidia ktk harakati zake za kisiasa.Mbussi,
Umesema kweli niliipenda CUF si kwa Uislam tu bali kwa kuwa haikuwa na uadui na Waislam.
Kuhusu hayo mengine siwezi kuyazungumza kwa kuwa yeye hapa hayupo.
Ni "ovyo" ndiyo Kiswahili safi si "hovyo."
Udini ni cancer inayoitafuna jamii. Nakushauri utoke huko, dini ibaki misikitini na makanisani na siyo kwenye vyama vya siasa na taasisi nyingine za umma. Hii ndiyo sababu nakumbuka umuhimu wa Nyerere aliyelikemea na kukataa udini kwa nguvu zote ktk serikali yake, japo wewe na wahafidhina wengine wa Uislam mnalikataa hilo. Vilevile Magufuli alikuwa akiandamana na viongozi wa dini na madhehebu yote bila kubagua. Nashangaa kuona haya mambo ya udini yamekuwa yakiibuka hasa inapotokea kiongozi wa juu ni Muislam. Tuliona kwenye utawala wa mzee Mwinyi na kwa kiasi fulani kwa Kikwete pia. Radio zenu hasa radio Iman, duuh vingine ni kunyamaza tu.
Kwenye uongozi wa Samia imekuwa ni agenda. Tumeona ilivyokuwa kwenye sakata la bandari, na hadi sasa wanaibuka akina Mwaipopo kuhubiri udini. Wewe pia kwenye post zako nyingi ni udini mtupu. Hapana, Katoliki na Ukristo havina ugomvi na Uislam japokuwa mnatuita Makafiri.