JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,114
- 3,541
Salamu wanajamvi!
Kama kichwa cha habari kinavyo jieleza, sisi watanzania ni wanafiki tuna hangaika kuzunguka mbuyu wakati ukweli wote uko bayana. Hapo tuna fail.
Rais wa 42, wa Marekani Bill Clinton kwa kosa la kutembea na mwanamke Monica Lewinsky, mrembo wa miaka 21 ndani ya ikulu ya Marekani ilitosha kuwa impeached na Bunge la Makabwela. Kabla ya kupiga kura, mjadala ulikuwa mkali sana, na wabunge wengi walioneshwa kukerwa na tabia hiyo tena ndani ya Ikulu ya Marekani.
Baada ya mjadala kura zikapigwa, na wengi waliafiki kwamba Bill Clinton awe IMPEACHED. NA IKAWA HIVYO. Sasa, issue yake ikaenda bunge la Senate ili liinidhishe kwa mujibu wa kanuni zao. Huko nako shughuli ilikuwa pevu, akaponea chupu chupu.
Sasa turudi kwenye sakata la DP WORLD na bandari za TANGANYIKA. Kimsingi Rais Samia amevunja KATIBA ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Kwa kuuza sovernity ya Nchi yetu na kuikasimu wa Waarabu kwa kujua au kwa kuto kujua. Hilo halimfanyi asiwe na kosa.
Je, Bunge letu linaweza kumfanyia IMPEACHMENT na hatimaye kuondolewa ofisini kwa kosa lake hili?
Kwa KATIBA hii hii mbovu hilo linawezekana. Shida ni moja kubwa nayo ni udhaifu wa taasisi za kiserikali tulizo nazo. Siwezi kusema hazijitambui , lakini nafikiri huwa zina dhani Rais ni Mungu mtu.
Kwa kosa hili moja tu, Rais Samia alistahili kuwa IMPEACHED, Kwakuwa bado yupo ofisini najiuliza ni kosa gani Rais akifanya atakuwa impeached na kufunguliwa mashitaka?
Kuuza bandari zetu zote na kukabidhi sovernity ya Nchi yetu kwa Waarabu sisi bado tunazunguka mbuyu tu..............!