Adam sio mtu wa kwanza kuumbwa bali yeye alikuwa mtu wa kwanza kuongea na Mungu au alikuwa mtu wa kwanza kupokea ufunuo wa miongozo kutoka kwa Mungu.
Katika Dini ya Uisilamu Adam anacho cheo cha unabii na utume, mtu hawi mtume hadi kuwepo na watu ambamo kwao huyo mtume ametumwa kamwe mtume hawezi tumwa bila ya kuwepo kwanza kuwepo watu, sasa inaposemwa Adam ni mtu wa kwanza maana yake ndiyo hiyo kwamba ni mtu wa kwanza kupokea ufunuo, kuongea na Mungu na kuwa civilized na akawa wa kwanza kuwafundisha watu wake mafundisho ya Mungu.
Kuja kuijaza dunia hiyo ni kanuni ya maumbile ya wanadamu na wanyama pia, wanyama pia nao huijaza dunia katika njia ileile ambayo binadamu huijaza dunia sasa wao wameambiwa wapi waje kuijaza dunia???, kwa maana hiyo maneno "kuijaza dunia" ni maneno yenye maana fulani ya kiroho.
Sasa kwa lengo la mjadala tufanye Adam ndiye mtu wa kwanza kuumbwa na baadaye Hawa akatokea "ubavuni" kwa Adamu na kisha wakazaa watoto wawili Kaini na Habili, hadi hapo walikuwepo Watu 4 (wanne) yaani; Adam, Hawa, Kaini na Habili. Kama utakumbuka imeandikwa ndani ya Biblia kwamba Kaini alimuua Habili kisha akatorokea nchi ya NOD na alipofika huko AKAOA, swali linakuja alioa kitu gani wakati alipomuua nduguye walikuwa wamebaki watu 3 watatu tu??!!, Maana yake ni hii Huko NCHI YA NOD walikuwepo watu wengine wakiishi na ndiyo maana ikaitwa "nchi" ya Nod, sote tunajua eneo likiitwa nchi maana yake watu wanaishi hapo. Huo ni ushahidi kutoka ndani ya Biblia kwamba Adam hakuwa mtu wa kwanza kuumbwa bali walikuwepo watu kabla yake naye Adamu alizaliwa kama watu wengine.
Ukisoma History ni kwamba Adam aliishi maeneo ya Babylon katika makutano ya mito miwili ya Tigris na Yufrata (Tigris and Euphrates) katika Iraq ya leo, aliishi yeye na watu wake "qawm" takriban miaka 6,000 (elfu 6) iliyopita hadi leo, bado historia inasema fuvu la mtu wa kale lilifukuliwa huko Oldivai Gorge lenye umri unaokadiriwa miaka 1000,000 isitoshe bado mafuvu na masalia ya watu wa kale yaliyokuwepo kwa maelgu ya miaka yanazidi kufukuliwa katika sehemu mbalimbali duniani, kulingana na historia kamwe huwezi kusema Adam alikuwa ni mtu wa kwanza kuumbwa bali yeye alikuwa ni mtu wa kwanza kupokea ufunuo, kuongea na Mungu, kuwa civilized au kwa neno zima yeye alikuwa mtu wa kwanza "kuumbwa kiroho"( kuumbwa kiroho maana yake alikuwa mtu wa kwanza kuwa karibu sana na Mungu).
Basi swali linaibuka je Mtu wa kwanza kuumbwa ni nani ??!!--- hilo swali ni gumu kweli kwani utakapolijibu hapohapo yataibuka maswali mengine; Kuku wa kwanza kuumbwa ni yupi?? Mbuzi wa kwanza, Bata wa kwanza, mchungwa wa kwanza, Sisimizi, Fisi, Simba, Ng' ombe nk, wa kwanza kuumbwa ni wepi?!!😒.
Lakini ni lazima kulikuwepo na watu, wanyama, mimea na hata wadudu nk, vya kwanza kuumbwa.
Dunia hii ilivyokuwa leo sio sawa na jinsi ilivyokuwepo billions ya miaka iliyopita, muundo (feature) wa dunia katika miaka hiyo kabla ya UHAI (the origion of life/ genesis) dunia yote ilifunikwa na maji ya uhai (Biotic soup) na nuru ya jua ilikuwa ikishuka mojakwamoja katika uso wa dunia, Biotic soup n8 supu iliyokuwa na mchanganyiko wa elements zilizoweza kuzalisha viumbe hai pale ambapo nuru ya jua iliposhuka moja kwa moja kama "Catalyst" kwenye hiyo supu kuchochea reaction ya kikemikali, kumbuka hiyo nuru ya jua (ultra violet rays) hivi sasa imepunguzwa nguvu yake na "ozone layer" ambapo hapo zama za "biotic soup" hakukuwa na hiyo layer na nuru ilikuja moja kwa moja katika uso wa dunia---- jinsi ambavyo viumbe wametoke duniani ni "Complex mechanism" kifupi ni kwamba hiyo ndiyo njia ya awali ya kisayansi jinsi viumbe hai walivyotokea, kwanza walianza kuumbwa Viumbe wa Baharini katika Biotic soup iliyofunika uso wa dunia, hiyo supu ilipojitenga kufanya Bahari na nchi kavu ndipo viumbe wengine wa nchi kavu wakatokea kama vile mimea na Donasours nk, baadaye sana ndipo Mtu naye akatokea hapo hali ya uso wa dunia tayari ilikuwa imebadilika vya kutosha kuweza kukidhi uhai wa mtu (Watu wa kale kina Zinjanthropus boisei), hapo tayari Ozone layer ilikuwa imeshajitokeza nk, baada ya viumbe kuwepo katika uso wa dunia viumbe hao wakaendelea kuijaza dunia kwa njia ya kujamiiana na watu wa zama hizo walikuwa "primitive sana" hawakumjua Mungu kabisa na miaka ikaenda watu wakiwepo taratibu wakipata ustaarabu hadi zama za Adam ndipo Mungu akaona inafaa kumpa ufunuo huyo Adamu ili awape watu wake ujumbe kutoka kwake Mungu ndipo Adamu akawa mtu wa kwanza kupewa ujumbe kutoka kwa Mungu.
Mungu anazo njia 3 za uumbaji, Uumbaji wa kwanza ni kuumba kutoka katika utupu (creation of something from nothing), uumbaji kutoka katika sehemu ya kitu, na uumbaji wa kuzaliana. Njia ya Uumbaji wa viumbehai wa Mwanzo niliyoieleza ni hiyo njia ya pili.
Njia hiyo ya pili leo bado inatokea duniani; kuna baadhi ya watu wakifungwa POP (hogo) kwa muda fulani litakapoenda kuondolewa utashangaa kukuta ndani kuna chawa wengi, swali hao chawa wametoka wapi???---- ni muunganiko wa chemikali kutoka kwenye POP, ngozi ya mhusika iliyokufa, jasho linalotoka katika mahali ilipofungwa POP, joto la mwilini, hewa ya carbon kutoka katika mwili sehemu ilipofungwa hiyo POP, kutaja kwa uchache tu hizo ni kama "Biotic soup" inaweza kuzalisha chawa ndani ya POP.
Juu ya yote Adam hakuwa mtu wa kwanza KUUMBWA.