Tundu A. M. Lissu & "Protocol Security" yake....

Tundu A. M. Lissu & "Protocol Security" yake....

Kuna wakati najiuliza kuwa adui mkubwa wa Tundu ni nani?
Jibu rahisi : Ni wanaCCM wachache wanaonufaika binafsi na utawala wa awamu hii.
Kila awamu tangu zamani ina wanufaika wakuu ndani ya CCM.

Hata awamu ya tano ina wanufaika wake wakuu.
Hawa ndio muda wote wanaangalia maslahi yao na nani ni tishio kwenye maslahi yao binafsi.
Hawa kwao vyeo ndio maslahi ya Taifa. Yani akishateuliwa basi anaimba wimbo wa uzalendo na kukatika viuno majukwaani muda wote meno yakiwa nje. Hapo Nchi inakua haina tena sheria ya kumuongoza isipokua kumfurahisha mteuzi wake na yeye kupata maslahi yake na familia yake..

Sina uhakika vizuri na nchi yetu lakini kuna baadhi ya nchi Duniani hasa Afrika ambapo teuzi zinajali zaidi Udini,Ukabila na ukanda wa anapotoka anayeteuliwa. Sijajua kwetu ikoje kwa sasa lakini angalau hatujafikia huku sana.
Lakini kama vigezo vinakua ni ukabila au udini basi kundi linalonufaika kikabila linakua na Roho Mbaya sana kwa mtu yeyote anayekua ni hatari kwa nafasi za ndugu yao wa damu au kabila.
Hapo mtu hamtetei mtu kama tu Kiongozi wa nchi Bali kama ndugu wa damu anayetaka kuporwa tonge mdomoni.
Hasira na chuki zinakua ni kubwa sana tena zinaambatana na vitisho vya wazi na hata kuua alimradi tu watu wanamtetea ndugu yao . Hapo sheria hua haizingatiwi tena bali hasira ya kuona ndugu yao anataka kukosa nafasi ambayo inawanufaisha wao kama familia au ndugu au kabila moja.

Ndio maana nchi zilizostarabika zinaweka sheria na katiba yenye ukali sana kwa watawala wanaovunja sheria kufikishwa mahakamani hii inawafanya hata ndugu kuepuka kutisha watu au kuua watu kwa lengo la kupigania ulaji wa kindugu. Hata ndugu wanakua ni sehemu ya kuhamasisha amani ,haki na usawa kwa hofu ya ndugu yao kutiwa gerezani.

Tanzania kutokana na uchumi wetu kukua sasa tunahitaji kiongozi anayeweza kulinda sheria nyingi tulizojiwekea kama jamii . Lakini pia mwenye uwezo wa kuwaita Watu wa nje na kubishana nao kisheria huku akitetea maslahi ya watanzania.

Tupinge hii roho chafu inayohamasisha watu kuua wenzao kama alivyofanya yule mwanaharakati aliyewataka wananchi wauawe kwa kumpokea kiongozi wa chama aliyenusurika kufa na kulazwa hospitalini kwa miaka.
Hii chuki sio ya kizalendo Bali ni maslahi watu waliojiwekea kuwa yatakuwepo kwa miaka kumi au ishirini au ya kudimu.
Maslahi ya nchi yanasimama kwenye sheria sio Mbwembwe wala nyimbo za majukwaani.
Uzalendo ni kulinda sheria zilizowekwa kikatiba . Hakuna Uzalendo unaowaza kupata tuu bila kupoteza kwa kutetea haki.
Kama atatokea MwanaCCM akasema kuwa tutasimamia uchaguzi uwe wa amani huru ,haki na usawa kwa wote hata kama tutashindwa kwa haki tutakubali kushindwa. Huo ndio uzalendo!!
 
Aisee CDM wawe makini sana.

Kuna watu wanaanza kutangulia mbele .

Kuna wengine wanafikiria hata kutengeneza muvi ya " T.Lissu" kasimamishwa


CDM wawe makini...
 
Aweke namba ya kuchangia tutajichanga aweze kupata ulinzi wa kweli kweli. Huyu sisi ndiye mnyonge mwenzetu.. sio wale wakinafki.
Hili ni muhimu sana mimi nitaunganisha na account yangu wawe wanakata humo humo kwa ajili ya Ulinzi wa Lissu kila mwezi
 
Kuna sehemu Tanzania limetokea tetemeko la ardhi vinywaji vimemwagija kwenye meza kwa mtikisiko.
 
Waziri Mkuu, Spika (V8s)au MTU yeyote mwenye gari Aina ya IST anaweza kutoka Dodoma Asubuhi na kufika Kagera same day(10-12hrs Trip). Safari hiyo itacover mikoa 8 ya Dom,Sngd,Tbr,Shinyanga,Simiyu,Mwanza,Geita na Kagera. Na kama unahitaji kufika kila Mkoa barabara (ambazo zote ni Lami tupu) ndiyo njia ya haraka, Sahihi na salama kutumia.
 
Anapita barabarani ana appreciate kazi iliyofanywa kuweka hizo lami.
 
Mkuu Kitatu, Mungu akubariki sana kwa bandiko hili! Mimi ni mwombaji, lakini pamoja na kushangilia sana ujio wa Lisu na kumtetea hapa ‘kijiweni’, sijamwombea! Naanza rasmi kumwombea, leo!
Nami namweka katika maombi yangu. Atakayetaka kumwondoa Tundu Lisu, ataondoka yeye na kumwacha Tundu Lusu katika utukufu.

Maombi yangu siku zote na wakati wote yamesimama. Kama ningekuwa kama wale wengine, ningekuwa na Kanisa tayari. Lakini kwa vile naamini Kanisa ni la Kristo, mwanadamu hawezi kuwa na Kanisa, nitaendelea kuwamo nyumbani mwa Bwana nikiusifu ukuu na uaminifu wake katika ahadi zake.

Uzi huu umenipa nafasi ya kutafakari makuu ya Mungu aliyowahi kunifanyia ikiwamo kuniepusha na kifo cha wazi cha bahati mbaya na vile vya kupangwa. Haikuwa kwa werevu wangu bali kwa vile alinitaka niishi.

Hakika Tundu Lisu hatakufa kamwe kwa hila za mwanadanu yeyote bali kwa mapenzi yake aliyemwumba. Mwenye kumgusa kwa dhamira chafu ataipokea hukumu aliyojiandalia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
LUKA 13

31 Saa ile ile Mafarisayo kadha wa kadha walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua.

32 Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha;Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika.

33 Pamoja na hayo imenipasa kushika njia yangu leo na kesho na kesho kutwa; kwa kuwa haimyakini nabii aangamie nje ya Yerusalemu.

Huo mstari wa 32, ni very interesting.....

Yesu Kristo anam - refer HERODE kama Mbweha....

Cheo cha "Herode" kwa leo ndicho kama alichonacho Magufuli wa CCM leo yaani "Rais wa nchi"....

Suppose leo Tundu Lissu amwite Bwana Rais wa Tanzania kama "Mbweha", kelele zitapigwa weeee kuwa kamtukana...

Mimi nadhani waanze na kumshutumu Mungu yaani Yesu Kristo kwa kauli yake hii kwa Herode....!!
 
Mkuu katika uzi wako kuna mapungufu so unataka mbinu zao za kumlinda mtu wao ziwe wazi ili iweje , mi nafikili ushauri hapa pamoja na mbinu zao walizo nazo ambazo hatuna haja ya kuzijua but ni jukum la vyombo vya usalama kuhakikisha yupo salama basi

Hujanisoma vizuri na kwa umakini/uangalifu. Sijasema hivyo...

Kwa manufaa yako, rudia tena kunisoma...

Bandiko langu hali - demand CHADEMA kuweka wazi mikakati yao ya ulinzi wa TAL....

Bandiko langu linashauri kuhusu hilo....
 
Nimefurahi kusoma taarifa nyingi humu kuhusu "convoy" ya Tundu Lissu inavyoendelea katika mikoa 10 kuzifuata saini za wadhamini ili wampe uhalali wa kuteuliwa kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA....

Safari ilianzia Dodoma mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kuomba uteuzi wa ugombea Urais wa JMT katika ofisi za NEC. Sikuwa huko, lakini niliona kuwa every thing was perfect....

Vivyo hivyo Singida hadi kule kijijini kwake, akapita Igunga na Nzega kando ya makao makuu ya mkoa wa Tabora, kisha Kahama - Shinyanga na leo tarehe 12/8/2020 kaingia Mwanza na inaonekana atafika mkoa wa Mara leo Leo....

Wote tunajua anatumia usafiri wa barabara (Magari) na kwa hakika hii ni safari ndefu sana kwa njia hii na ni "very risk" pia kiusalama....

Concern yangu ni hakikisho la usalama wake....

Wapinzani wake wa kisiasa (CCM na serikali wanayoingoza) wasingependa kumuona huyu mtu anashiriki uchaguzi huu dhidi ya mgombea wao Pombe Magufuli...

Kwa hakika, wako jikoni hawa usiku na mchana wakijaribu kila "option" isiyoacha "trace" zao ili kumtoa jamaa "out of the picture" haraka kwa kadiri inavyowezekana....

Tunafahamu pia Mungu muumba ndiye anayemlinda kila mtu mwema. Tundu Lissu kwa hakika hana kosa lolote hata astahili kufa. Huyu ni mtu mwema. Kosa lake ni moja tu. Kuchokonoa na kutaka huharibu maslahi ya watawala. Hill ndilo kosa lililotaka kudhulumu uhai wake 07/09/2017.....

Lakini kwa ujinga huu, ubinafsi na hofu ya watawala ndiyo inasukuma tendo hili lililobebwa na "roho ya uuaji" ndani ya nafsi za watawaka kutaka kufanyika tens....

Wanamuona huyu jamaa anatishia maslahi yao. Wanadhani jibu pekee ni kumuua tu ili wawe Salama. Huu ni ujinga wa kishetani...!!

Mungu ndiye mlinzi wetu sisi sote. Huyu Mungu Yehova aliyemuumba Tundu Lissu, kiuhalisia ndiye anayemlinda na atamlinda siku zote hadi anaingia ofisi kuu ya nchi hii - Ikulu. Lakini Mungu hutoa maarifa ya usalama kupitia watu wake...

Aidha najua kuwa protokali za kiusalama huwa za mtu mwenyewe na walio karibu naye. Si rahisi wakaweka mipango yao ya kiusalama. Nami sisemi waweke hayo wazi hapa au popote...

Hata hivyo, sisi wengine ni wa kusema tu katika namna ya kutahadharisha na kukumbushana...

Na kwamba, kutumia njia ya barabara kwa safari ndefu kama hii anayoifanya Tundu Lissu kuzungukia mikoa 10 Tanzania nzima ni very risk kiusalama na kwa vyovyote lazima timu inayoshughulikia usalama wa mtu huyu iwe very well equipped na mbinu, mikakati na vifaa vya kisasa vya kuhakikisha usalama wa mtu huyu muhimu sana kwa wakati huu ambapo Tanzania na Watanzania wanamhitaji mno kwa sababu amebeba AMANI, FURAHA na MATUMAINI yao....

Hatutavumilia kabisa kumpoteza mtu huyu kwa wakati huu...

NAMTAKIA KILA LA KHERI TUNDU A. M. LISSU NA MUNGU YEHOVA AMBARIKI SANA....!!
Hebu acha kujitekenya na kucheka mwenyewe...mtawala gani Kama angetaka TL kuuawa angebakia hai! TL alishapuuzwa hata kabla ya kushambuliwa na kambi yake mwenyewe🤔! Serikali ninahakika haikuhusika na Wala haitahusika na mapichapicha yao! Kwa hiyo yy ajilinde na kambi yake mwenyewe🤔! Serikali Haina haha ya kuanza ya wagonjwa wa akili...vinginevyo isingewekeza C1 bugando, milembe nk🤣😂🤣!
 
Mkuu Kitatu, Mungu akubariki sana kwa bandiko hili! Mimi ni mwombaji, lakini pamoja na kushangilia sana ujio wa Lisu na kumtetea hapa ‘kijiweni’, sijamwombea! Naanza rasmi kumwombea, leo!

Good of you, anza sasa mtumishi wa Mungu...

Vita aliyonayo huyu ndugu ni kubwa mithiri ya ile ya Yesu Kristo miaka takribani 2000 iliyopita katika safari yake kuukomboa ulimwengu toka kwenye mikono ya Shetani, Ibilisi....

Alikuwa anapambana na watawala wa dunia hii wenye nguvu na mamlaka ya kidunia....

Hawakujua kuwa, yeye ndiye MFALME wa WAFALME, muumbaji na mmiliki wa vyote mbinguni na duniani...

Mwisho wa siku, Yesu Kristo alishinda zaidi ya kushinda...

Tundu Lissu pamoja na sisi sote, Mimi na wewe na yule, tutashinda kwa msaada wa Mungu wetu aliyehai katika Jina la Yesu Kristo....!

Omba, omba, omba mtumishi. Usichoke kumwomba Mungu muumba watu.... Amen
 
Tundu Lissu hatafanywa kitu. Ikitokea akapata accident na kufariki itakuwa too much of a coincidence. Huyu sijui kama watajaribu kumchapa tena. Efforts zote zitapelekwa kwenye wizi wa kura ili ionekane ameshindwa kihalali. Baada ya hapo watajaribu kumfix kwenye kesi alizonazo.

Kwa sasa Chama kingejaribu kumuweka sawa na kumwambia aepuke kurusha allegations nzito na ambazo anajua akiambiwa atoe evidence atakuwa hana na wanaweza kumbana kwa sheria zilizopo.

Tukuelimishe kidogo. Kwenye platformvya siasa, allegations hazihitaji proof mahakamani.

Ukishutumiwa unajibu hoja. And that's it. Hakimu hapo huwa mwananchi kwenye sanduku la kura.

Kwa hiyo punguzeni kujitisha wenyewe kwa mambo ya kufikirika.

CCM ndiyo wana hofu halisi. Wanajua umma uko nyuma ya TL hata kama wanajifanya hawaoni.

Kawapanikisha mpaka wanatamani wajaribu kumuua tena, lakini mtu huwa hafi mara mbili.

Mwaka huu wanalo...
 
Back
Top Bottom