TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI
SEHEMU YA 6.
Maelezo haya yapo ukurasa wa 497 na 498. Anasema hivi:
“Hayo maneno hayapo kwenye Kielelezo D16. Ni kweli kwamba nilikuwepo katika mkutano.”
Anasema viongozi hawakukosea kuzungumzia changamoto wanazokutana nazo wakati wa uchaguzi.
Na huyu ni shahidi wao. Angekuwa wa kwangu, wangesema, “Unategemea nini?”
Waheshimiwa Majaji, Kifungu cha 67(1) cha Sheria ya Ushahidi kinazungumzia ushahidi wa moja kwa moja.
Hiki kifungu huwa kinaitwa “The best evidence.”
Kama ni ushahidi wa kuona, ni shahidi wa kuona.
Kama ni wa kusikia, ni shahidi aliyesikia.
PW17 ni “the best witness.”
Wameniweka gerezani mwaka mmoja na nusu, wakijua sina hatia, kwa maneno ya shahidi wao.
Nisipozungumza haya kwa ukali, Waheshimiwa Majaji, mawe yatazungumza.
Waheshimiwa Majaji, PW17 alikuwa shahidi wa mafichoni, na mimi nina shida sana na hilo kwa sababu ninaamini sana katika Open Justice.
Lakini Waheshimiwa Majaji, in all fairness, huyu ni shahidi bora aliyetoa ushahidi wake mafichoni.
Huyu hakukamatwa na Polisi kama wale wengine ambao walikamatwa, wakashtakiwa na baadaye wakafutiwa kesi ili waje kutoa ushahidi dhidi ya Tundu Lissu.
Muhimu zaidi kuhusu shahidi huyu, ushahidi wake unaunga mkono ushahidi wote wa utetezi.
On all major questions, Waheshimiwa Majaji, PW17 amepingana na ushahidi wa Prosecution.
Waheshimiwa Majaji, kwa hilo, mashahidi wanne wa mashtaka wametofautiana fundamentally.
Maana yake ni kwamba kuna ndimi mbili, na effect ya hizi ndimi mbili.
Na hili nilisema jana, Waheshimiwa Majaji, ni suala la kufa na kupona.
Without proof, kesi inakufa.
Waheshimiwa Majaji, ninachotaka kusema hapa ni kwamba kesi yote ya mashtaka imejengwa kwenye hisi.
Ukizuia uchaguzi uliowekwa kisheria, maana yake umeitishia Serikali.
Waheshimiwa Majaji, je, ni kweli kwamba Serikali ndiyo chombo pekee kinachosimamia sheria nchini?
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.