Tundu Antipas Lissu special thread (CHADEMA CHAIRMAN)

Tundu Antipas Lissu special thread (CHADEMA CHAIRMAN)

IMG-20261101-WA0009.jpg
 
Taarifa za kusikitisha zimetufikia SasaLive zikithibitisha kifo cha Wakili Allute Lissu Mughwai, ambaye ni kaka wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa,Tundu Lissu, kilichotokea usiku wa kuamkia leo.

Habari za ndani za kuaminika zimeweka wazi kuwa msiba huo upo mkoani Arusha, ambapo taratibu za awali za msiba zinaendelea kuratibiwa na wanafamilia na ndugu wa karibu.

Hadi kufikia sasa, ratiba ya mazishi imepangwa kufanyika katika Kijiji cha Mahambe mkoani Singida, huku ikielezwa kuwa mazishi hayo yatasubiri kwanza kukamilika kwa hukumu ya kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu inayotarajia kusomwa tarehe 06 Novemba 2026.

SasaLiveinaendelea kufuatilia kwa karibu taarifa zaidi kutoka kwa viongozi wa familia na wanasheria ili kuwajuza wananchi na wadau kuhusu hatua nyingine zote za msiba huu mzito.

#AlluteLissu #TunduLissu #Chadema #Arusha #Singida SasaLive
1793517568074.jpg
 
Mdogo wake na Tundu Lissu, Ikota Lissu, amesema kuwa kumfikishia taarifa za msiba wa kaka yake Tundu Lissu ,marehemu Alute Lissu, ilikuwa kazi nzito kihisia kutokana na uhusiano wa karibu uliokuwapo kati yao kwa kuwa marehemu, alikuwa mlezi na mshauri wa Lissu katika masuala mbalimbali, yakiwamo sheria na siasa.

Akisimulia tukio hilo, Ikota amesema walifika Gereza la Ukonga asubuhi wakiwa watu wanne, wakiwamo yeye, Jenerali Ulimwengu, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na mpwa wa Lissu, lakini uongozi wa gereza uliwaruhusu ndugu wawili pekee kuingia kumfikishia taarifa hizo.

Amesema walipokutana na Lissu, hawakuhitaji kutoa maelezo marefu, kwani baada ya kusalimiana na kuulizana hali za nyumbani, mpwa wake alimtajia jina la Alute, jambo lililomfanya Lissu kuelewa mara moja kuwa kaka yake amefariki dunia.

Kwa mujibu wa Ikota, baada ya kupata taarifa hizo, jambo la kwanza Lissu alilosisitiza ni kuhakikisha marehemu anapata mazishi yanayostahili, huku akiahidi kutoa Sh.15 milioni kugharamia shughuli hizo.

Pia, Lissu aliwaelekeza ndugu zake kushirikiana na mapadri, askofu, viongozi wa Kanisa Katoliki mkoani Singida na marafiki wa marehemu katika kuratibu mazishi hayo, akisisitiza umuhimu wa kumpa heshima kaka yake.
1793671599219.jpg
 
Back
Top Bottom