TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI
SEHEMU YA 11.
Waheshimiwa Majaji, mashahidi wote watatu hawa, without exception, wamesema haya maneno yanatengeneza kosa la uhaini.
Wametoa sababu zilezile kwamba maneno hayo ni uhaini kwa sababu ni mapolisi walewale.
Waheshimiwa Majaji, mashahidi wa utetezi wote wamesema maneno hayo siyo kosa kwa mujibu wa sheria za Tanzania.
Kwa DW1, ukurasa wa 596 na 623.
Kwa DW2, zipo ukurasa wa 671 to 672, 679, 681, 699–700, 703, and 726 to 728.
Kwa DW3, ushahidi wake upo ukurasa wa 747 to 750, 753 to 754, 787 na 797.
Kwa DW4, ushahidi wake upo kwenye kurasa za 805 hadi 806, 810 hadi 811, 814, 818 na 831.
Kwa DW5, ushahidi wake upo kwenye kurasa za 889 hadi 890, 930 na 932.
Waheshimiwa Majaji, mashahidi wote wa utetezi wamedai kwamba hayo maneno yanayodaiwa ni ya uhaini hayana kosa kwa sheria ya Tanzania.
Waheshimiwa Majaji, kwa sababu kuna pande mbili za ushahidi zinazopingana, je, upi ni msimamo wa sheria katika jambo hili?
Mahali pa kuanzia ni katika Ibara ya 28(4), na maneno ya Katiba yote katika Ibara hii ni muhimu.
Uhaini, kama unavyofafanuliwa na sheria, utakuwa ni kosa la juu kabisa.
Waheshimiwa Majaji, uhaini kwa nchi hii ni ule uliofafanuliwa na sheria, na nje ya sheria ni maneno matupu.
Sasa Waheshimiwa Majaji, kwa vile uhaini unatakiwa ufafanuliwe na sheria, ni sheria ipi inafafanua?
Ni Kifungu cha 39 ndiyo kinafafanua.
Kifungu cha 39 ni kifungu muhimu sana katika kesi hii.
Kama ninayotuhumiwa kuyafanya yapo katika kifungu hiki, hakuna uhaini hapo; ni maneno matupu.
Kifungu cha 39 kina vipengele vinne.
Kuna matendo 10 ambayo yametajwa kama uhaini.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.