BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakuanza leo, alianza akiwa shule na aliendelea hivyo hivyo kabla ya kuwa Mbunge, aliendelea hivyo hivyo baada ya kuwa Mbunge na anaendelea hivyo hivyo baada ya kuporwa ubunge kwa hila.
Hakuanza leo...alianza akiwa mzima wa afya, aliendelea hivyo akiuguza majeraha yaliyotokana na kumiminiwa risasi zaidi ya 30 na anaendelea hivyo hivyo pamoja na mwili kujaa makovu ya risasi.
Hakuanza leo...alianza akiwa kijana na aliendelea hivyo akiwa mwanasheria mdogo, aliendela hivyo hivyo akiwa Rais wa Wanasheria na leo anaendelea hivyo hivyo akigombea urais wa Tanzania!
Ndugu zangu Watanzania, tukimwacha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ni mgombea gani wa Urais aliyekuwa na historia kama ya Mh. Tundu Antiphas Lissu? Ni mgombea gani alipitia heka heka alizopitia Mh. Tundu Antiphas Lissu mikononi wa utawala kandamizi unaotumia vyombo ya dola kunyamazisha upinzani?
Ndugu zangu Watanzania, hebu tujikumbushe na kujiuliza:
Ndugu zangu Watanzania, majibu ya maswali hayo bila shaka yoyote mnayo kwani ni ya wazi kabisa na kwa miaka minne tumeshuhudia na kuvumilia mateso na manyanyaso yasiyo na kipimo. Hivyo mgombea mwenye sifa kama hizo hatufai.
Ni mgombea gani mwenye jeuri ya kusimama mbele ya wananchi na kuwaahidi uhuru na usalama wao kama katika utawala wake wananchi hao waliishi kwa hofu? Ni mgombea gani mwenye jeuri ya kusimama mbele ya wananchi na kuwaahidi haki na usawa kama wakati akiwa madarakani wananchi waliporwa hovyo mali zao? Ni mgombea gani mwenye jeuri ya kusimama mbele ya wananchi na kuwaahidi umoja na mshikamano kama wakati wake wananchi walibaguliwa kiitikadi, kikanda na kikabila?
Pamoja na hayo kumbukeni...
Mh. Tundu Antiphas Lissu hasimulii aliyosikia kuwakuta waliotumia uhuru wao wa kidemokrasia kuwakosoa walioko madarakani, hapana, anasimulia yaliyomkuta yeye katika harakati za kutetea uhuru, usawa, haki na utawala unaoheshimu sheria.
Mh. Tundu Antiphas Lissu hasimulii aliyosikia kuwakuta waliothubutu kupinga utawala huu jinsi walivyotekwa, kuteswa na kupotezwa, hapana, anasimulia yaliyomtokea yeye mikononi vyombo rasmi vya dola na visivyo rasmi vinavyodaiwa kutojulikana.
Huyo ndiye Mh. Tundu Antiphas Lissu yule yule wa siku zote...NI YEYE!
Kuna bwana mmoja baada tu ya kupata mamlaka fulani, moja ya vitu vya kwanza alivyofanya ni kumuita Bw. Reginald Mengi aende ofisini kwake.
Mengi aliitikia wito, ila kilichotokea ni kwamba mzee wa watu alikalishwa pale ‘holding room’ masaa mengi akimsubiri bwana yule.
Bwana yule alipotoka, akamwambia, “Nilitaka tu kukuonyesha kuwa ni nyakati zangu sasa inabidi ulitambue hilo”. Hii ni nukuhu isiyo rasmi ila ilikuwa inaendana na maudhui hayo.
True story.
Kuna bwana mmoja baada tu ya kupata mamlaka fulani, moja ya vitu vya kwanza alivyofanya ni kumuita Bw. Reginald Mengi aende ofisini kwake.
Mengi aliitikia wito, ila kilichotokea ni kwamba mzee wa watu alikalishwa pale ‘holding room’ masaa mengi akimsubiri bwana yule.
Bwana yule alipotoka, akamwambia, “Nilitaka tu kukuonyesha kuwa ni nyakati zangu sasa inabidi ulitambue hilo”. Hii ni nukuhu isiyo rasmi ila ilikuwa inaendana na maudhui hayo.
True story.
Ndugu zangu Watanzania, mwaka 2015 tulifanya makosa lakini kama wasemavyo wahenga, kosa si kosa bali kurudia kosa. Tukichagua tena hovyo, tusilalamike hovyo tutakapoanza kutendewa hovyo. Mwaka huu uwe mwaka wa kupiga moyo konde na kusema imetosha, hatukubali na hatutaruhusu...silaha yetu ni kura zetu!Lissu anatosha