Chidu Mangalili
Senior Member
- Mar 24, 2017
- 144
- 96
Mgombea uraisi kwa tiketi ya Chadem ndg.Tundu A.Lisu anahitaji kuiachilia nafsi yake kwa kusamehe mabaya yaliyomkuta miaka mitatu iliyopita.Kuyaongelea kila mahali ampatapo wa kumsimulia,hasa majukwaa ya kisiasa,kutazidishia machungu kwake na wale wote wanaomhusu.
Niliwahi kumsikia mwenyekiti wake,Mh.Freeman Mbowe, akiongelea kutaka maridhiano ya kisiasa kati ya upande wa upinzani na chama tawala.
Huenda aliona umuhimu wa kuachilia au kutokuendelea kunyoosheana vidole kwa hisia zitokanazo na tofauti za kiitikadi.
Labda Mh.Tundu angepata wasaa wa kumuuliza mwenyekiti wake mantiki ya mrengo huo.
Inawapunguzia pia vyombo vya uchunguzi wa tukio la kushambuliwa kwake uzito wa kuwiwa kijamii na kiuwajibikaji umuhimu wa kulifanyia uchunguzi wa aliyehusika.Kwani litabeba taswira ya "ushabiki au kupuuzia kuwa ni wanasiasa ktk hoja zao za kutafuta kura".
Aliachilie kwa ajili ya nafsi yake na itamuongezea umaarufu zaidi wa kisiasa kwani binadamu wengi hasa wastaarabu wanapenda kusikia neno msamaha kuliko kulipiza au kuendelea kulaani na kushutumu.Ipo mifano mingi,tena ya matukio ya mtendwa na mtendewa kujulikana wazi na jamii.
Pia kuendelea kumhisi mtu kuwa ndie mtekelezaji wa shambulio sio vyema.
Inaleta mpasuku zaidi kiasi kuwa hata kuachia na kusamehe inakuwa ngumu baadae kwani nae yule unampiga risasi za nafsi,huku ukiwa hauna uhakika wa yeye kuhusika atakuwa na majeraha ya nafsi ambayo huwa ni magumu kuachilia bila rehema ya Mungu nae kumwingia.
Hata kama ni mbinu za kutafuta kura basi isiwe kibinafsi kiasi hicho.
Iko siku mtakutana mtataniana kuwa mlichuana bali walio mashabiki wenu mnakuwa mmekwisha watenganisha kwa kujijengea uadui wa nafsi kwa jinsi ya upande waliopo.
Tunajijua Watanzania ni watu wa kukanyagwa bila hata kuuliza kwanini umenikanyaga na kuanzisha vita huwa tunamwambia aliyekukanyaga " samahani",kama umemjua,nae atakuomba samahani pia hata kama alifanya makusudi.
Mungu aliyekuponya ni Mungu wa msamaha,ni Mungu asiyependa kisasi wala kinyongo.
Kuachilia ni ushujaa kwani kunaiweka nafsi huru.Huenda ni mpango wa Mungu hata juu ya sintofahamu ya kipi kinaendelea kiuchunguzi ili kutoa mwanya wa kuyasamehe na maisha yaendelee kwani yeye ameshakuponya dhidi ya adui,tena usiemfahamu bado,naomba kusisitiza kuwa haumfahamu bado.
Usijikite kwenye kumnyooshea kidole mwingine kwani mara zote kiubinadamu huwa tunapenda kumlaumu kwa kila jambo baya litufikalo yule tunaevutana nae juu ya maslahi au Imani zetu.
Una wito wa kufanya siasa,umerudi ulingoni kaza daluga fanikisha uliyoyakusudia.
UTAKUWA UMEPONA MWILI NA NAFSI.