Lisu katika harakati za kusaka wadhamini akiwa mjini Tanga na Muheza amesifia kazi za awamu ya tano kuwa wanajenga reli mpya bwawa kubwa la umeme na miradi mingi mikubwa. Kafananisha kazi hizo na zile zilizofanywa na watawala wa kizungu na mwalimu nyerere, akasema wajerumani walijenga reli ya Tanga arusha na Dar Kigoma, huku waingereza wakiunganisha Tanga Dar na Tabora Mwanza.
Kasema amekaa ulaya miaka mitatu nao wana miundo mbinu kama ya kwetu na bado wanajenga mingine, hili ni jambo jema sana. Ila nimkumbushe wazungu walitawala miaka 75 na nyerere miaka 25 jumla yao ni miaka 100, JPM atafanya hayo ndani ya miaka kumi tu hongera JPM.
Kasema wajerumani walijenga shule moja tu ya Tanga school, yaani kwa miaka 35 waliyokaa hii nchi walijenga shule moja tu, leo hii tuna shule zaidi ya elfu 20 nchi nzima tena zenye walimu madawati na vitabu watoto hawabebi makwanja wala kuchangishwa fedha ya lebo na madawati.
Kasema nayeye akichaguliwa ataendeleza pale JPM atakuwa kafikia basi kama ni kweli ni jambo jema kabisa, ila basi atuonyeshe angalau ajenge ofisi ya makamu mwenyekiti CHADMA pale Dodoma tuamini hayo anayotuambia, alivyokuwa arusha kakuta ofisi ya chama imechomwa moto achilia kutohamasisha ukarabati wa ofisi hata kutoa mia ya pole hamna, hajazungumzia chochote afya ya mlinzi wala hajaenda kumpa pole. Nasikia ile nyumba niyakupanga sasa chama kitaikarabati au mwenye nyumba shauri yake?