Uchaguzi 2020 Tundu Lissu abadili upepo, aanza kumsifu Rais Magufuli

Huyo Jiwe sifa kwake ni Kama Dose ya usingizi.

Yaani anatafuta sifa kwa nguvu na na kwa gharama kubwa mnoooooo.
 
Haya ni madhara ya kuaminishwa kua upinzani umekufa Mara ghafka Mambo yanakua kinyume lazima mdate tu.
 
Nyerere aliyafanya yote hayo kwa muda gani?
 
Ila nimkumbushe wazungu walitawala miaka 75 na nyerere miaka 25 jumla yao ni miaka 100, JPM atafanya hayo ndani ya miaka kumi tu hongera JPM.
Tumtetee na kumpigia chapuo Magufuli sababu anastahili hivyo lakini tuwe rational tunapotaka kumlinganisha na watangulizi wake.
Wakoloni na Nyerere walikuta hakuna watanzania wasomi au wataalamu kwenye nyanja mbalimbali kama sasa.

Ndiyo maana Nyerere alikuja na mipango mingi sana ya kuboresha elimu nchi kama Universal Primary Education(UPE), mambo ya elimu ya watu wazima n.k.
Juhudi zake zilionekana na kutambulika duniani kote kiasi cha nchi yetu kufikia viwango vya juu sana kiasilimia ya watu wanaojua kusoma na kuandika au waliopata angalau elimu ya msingi.
 
Halafu hakujenga hata barabara ya lami kwao katika miaka 25 ya utawala wake. Aliona vijiji vyote vya Tanzania ni vyake, siyo Butiama tu. Barabara ya lami ya Kyabakari hadi Butiama imejengwa Nyerere akiwa ametoka madarakani muda mrefu. Halafu kuna watu eti wanamlinganisha Magufuli na Nyerere! Washamba sana binadamu.
 
Nyerere aliyafanya yote hayo kwa muda gani?
Miaka 25 lakini kumbuka Nyerere hakukuta nchi yenye miundombinu kama aliyokuta Magufuli, hakukuta vyuo vikuu wala wasomi kama aliowakuta Magufuli, hakukuta chuo kikuu hata kimoja, hakukuwa na wahandisi wala madaktari wazalendo kama aliowakuta Magufuli.
Huko jeshini hakukuta askari wazalendo (weusi) kwenye vyeo vya juu au wenye taaluma flani au ueledi kwenye uhandisi wa kuwatumia kama hawa aliowakuta Magufuli na kuwatumia kwenye miradi inayojengwa na jeshi.
Hakukuta muuguzi hata mmoja mwenye shahada ya uuguzi (Nursing bachelor degree)
Hakukuta TBA wala taasisi kama TRA.

Nyie vijana kasomeni,someni, someni kabla hamjamfananisha Magufuli na Nyerere. Niambie Magufuli ameanzisha viwanda vingapi vinavyomilikiwa na serikali katika miaka mitano yake ya kwanza na Nyerere alianzisha vingapi kwa miaka 25 kisha hivyo vya Nyerere gawanya kwa tano tujue wastani kwa miaka mitano alijenga viwanda vingapi?

Magufuli kakuta tayari kuna viwanja vya ndege vingi na na reli mbili kuu, Je Nyerere alikuta reli ngapi na viwanja vingapi?
Magufuli analipia watu elimu kuanzia elimu ya awali hadi chuo kikuu?
Magufuli analipia huduma za faya bure?
Magufuli anagawa chakula na madaftari shuleni?
Nyerere alifanya yote hayo. Na aliweza pia kuasaidia mataifa mengine kujikomboa.
 
Mwalimu alikaa ikulu miaka 29 Magufuli amekaa miaka 5 linganisha kama Mwalimu ndani ya miaka 5 alifanya yaliyofanywa sasa..fikiri kabla ya kuandika kijana.
 
unayosema ni kweli, tatizo kuu la nyerere lilikuwa uungwana, hakutaka mtu aambiwe ukweli, ukiiba hapa anakupeleka pale anaionea huruma familia yako, viongozi wa juwata walikuwa na nguvu kuliko GM wakampuni, uwajibikaji ukawa hafifu, ndio hayo anayohubiri leo Lissu, kumwambia mtu akalime asitegemee chakula cha msaada eti kwake kosa, wakati Lissu anatwambia tuna njaa Sumri alikuwa akilalamika kukosa soko la Mahindi yake kule sumbawanga,

Nani alikwambia Nyerere alisomesha bure? ulikuwa ukihitimu lazima ufanyekazi serikalini sio chini ya miaka mitatu, alikuwa na chuo kikuu kimoja chenye wanafunzi wasiozidi miambili, leo hii tuna wanafunzi elfu 90 vyuo vikuu zaidi ya 45, haiwezekani wakasoma bure, wakati wanyerere tulienda kusoma Old Moshi ilboru Galanosi nchi nzima, hebu fikiria kutoka Kayanga ukasome Ashira all the way binti hajatongozwa tu njiani? wale ma TT walijisevia watoto wa shule kama wake zao, leo hii kwetu kila kijiji kina sekondari na kuna sheria kali ukisalimia mwanafunzi tu unalipa faini ya ngombe na fimbo juu. kwenye utiaji nia mwaka huu Graduates pekee walikuwa 67 na kati yao 28 wanafanyakazi ulaya na tisa ni wahadhiri wa vyuo vikuu.
 
Nyerere hajaongoza miaka 25. Halafu usiwe unakuja humu ukiwa umelewa, video clip ya Tanga tunayo.
 
Unadhani kuhudumia idadi ya watu iliyokuwepo wakati wa Mwalimu kwa maana ya kutoa elimu, matibabu, maji mishahara ya wafanyakazi nk ni sawa na idadi ya watu iliyopo sasa?
 
Hapo kwenye ulazima wa kwenda kuajiriwa serikalini miaka mitatu unazidi kumpaisha akili kubwa Nyerere.
Unaelewa umuhimu wa hilo jambo na kwanini sasa tunapaswa tuige?

Hapo aliondoa tatizo la ajira la sasa kwa maana hawakufanya kazi bure.
Pili aliwapa fursa vijana ya kupata uzoefu kazini ambapo baada ya hapo waliweza kukidhi kigezo cha uzoefu wa angalau miaka mitatu kazini au kazi kama hiyo.
Aliwapa uzoefu ambao ilikuwa rahisi kwa sekta binafsi kuwaajiri, angalia sasa vijana na masters zao hawajui kazi wapo mtaani bila ajira na hawawezi kuajirika wala kujiajiri.

Hiyo idadi ndogo ya shule na vyuo ndiyo changamoto aliyoikuta akapambana nayo, kwanza hata angejenga shule nyingi angepata wapi waalimu na wanafunzi wa kutosha? Au umesahau ilikuwa rahisi kwenye familia nyingi kukuta mtu angalau mmoja hajasoma kabisa shule?
 
Unadhani kuhudumia idadi ya watu iliyokuwepo wakati wa Mwalimu kwa maana ya kutoa elimu, matibabu, maji mishahara ya wafanyakazi nk ni sawa na idadi ya watu iliyopo sasa?
Hata miundombinu na wataalamu wa wakati huo tofauti na sasa.
Hivyo usichukulie kuwa ilikuwa kazi rahisi, Nyerere aliweza sababu kuu mbili.
Kwanza aliwekeza sana kwenye kilimo na viwanda hivyo tuliuza bidhaa nyingi za kilimo na mifugo nje ya nchi kuliko sasa.
Pili Nyerere alikuwa bingwa wa diplomasia hivyo alipata sana misaada ya maendeleo huko miaka nyuma kabla ya vurugu kubwa za vita baridi.
 
Jamani mabadiliko ni lazima na ukweli lazima usemwe hata kama ni mchungu. Naomba niongelee jambo moja japo hapa sio mahala pake lakini nachomekea tu. Kule bungeni mbunge mmoja alizungumzia kuhusu kuajiriwa Air hostess wenye viwango na mvuto kwenye ndege zetu za Air Tanzania. Mbunge huyo aliandamwa mpaka akaomba radhi lakini ukweli haukusemwa. Siku moja nilipanda Air Tanzania flight ya Kilimanjaro hadi Zanzibar ndege aina ya Bombandier.

Ndege hii kimuundo ni nyembamba kwa hiyo mle ndani sehemu ya kupita ni nyembamba lakini cha ajabu alikuwepo Air hostess mmoja mnene na mpana hata yeye mwenyewe alikuwa anapita kwa shida kweli. Ninavyojua mimi cabin crew huwa anatakiwa asizidi kilo 62 na hata Rwandair, Kenya airways, Ethiopian, KLM, SAA, Egyptyair, n.k. na hata Precision air ( nimezitaja zile nilizowahi kupanda karibuni)bado wanafuata vigezo hivi vya kimataifa vile vile wanatakiwa wawe na mvuto, lugha nzuri, smile na sura nzuri.

Nakumbuka msichana mmoja wakati wa EAA alijifungua akawa anakula hovyo (junk food) matokeo yake aliporudi kazini akawa ni over weight alitolewa kwenye flying akahamishiwa department ya cargo. Yoyote yule muhusika Air Tanzania vigezo vya kimataifa vifuatwe hiyo mizinga yenu itoeni kwenye ndege na ikitokea emergency hata kuinama tu itakuwa shida itabidi aokolewe yeye badala ya kuokoa passengers. Samahani kwa yoyote niliyemkwaza kwa hili mie naropoka tu.
 
Nyerere hakuchimba madini na wala hakukuwa na wawekezaji wa kigeni kwa maana ya FDI ilikuwa kama haipo na ndio alifanya hayo.

Mimi nimesoma shule ya msingi kwenye hiyo miaka ya sabini tulipewa madaftari shuleni bure na wanafunzi wa sekondari wakipewa warrant za kusafiria hadi wafungwa waliomaliza vifungo vyao walipewa warrant za kusafiria.

Where were you?? Population ikiwa ndogo mostly na productivity pia hua ndogo na ikiwa kubwa pia productivity inapashwa iwe kubwa vile vile.
 
Mwalimu alikaa ikulu miaka 29 Magufuli amekaa miaka 5 linganisha kama Mwalimu ndani ya miaka 5 alifanya yaliyofanywa sasa..fikiri kabla ya kuandika kijana.
Wewe usijitoe ufahamu nenda kafanye utafiti vitu alivyofanya Nyerere kipindi hicho na kwa rasilmali alizokuwa nazo, plus alisaidia hadi ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika kwa fedha zetu na watu wetu.

Tafuta yote ya Nyerere gawanya kwa tano kisha linganisha na ya Magufuli ya miaka mitano, hata hizo reli na umeme wa Stieglers vyenyewe bado hajamalizia ndiyo kwanza ameanza havijaisha.

Acheni ushabiki wa kitoto Magufuli bado sana kwa Nyerere ila akijitahidi zaidi atamkaribia au atamkuta na kumpita, ila kwa sasa tukitafuta wastani bado sana kuwafananisha kundi moja.
 
Mwalimu alikaa ikulu miaka 29 Magufuli amekaa miaka 5 linganisha kama Mwalimu ndani ya miaka 5 alifanya yaliyofanywa sasa..fikiri kabla ya kuandika kijana.
Nyerere alikabidhiwa Ikulu 1962 alikuta hazina ya taifa ina pound 75m hadi kufikia 1967 alikuwa kafanya nini? Maafisa wa Ikulu aliowakuta Nyerere kina Kasela Bantu na Edwin Mtei waliamua kutimka zao baada ya kuona mambo hayaendi sawa. Ni Amil Jamal raia wa Canada mwenye asili ya India ndio aliyekuja kuokoa jahazi, viwanda mnavyo visifia ni juhudi binafsi za Amil Jamal. Halafu leo mpuuzi mmoja anakuja kumbeza JPM.
 
Mkuu waambie hawa wanojitoa ufahamu.
Kwanza wakae wakijua hadi Mwinyi alitoa madaftari shuleni.
 
Muon Muongo Wewe !!!!
 
Hakuna anaye mbeza Magufuli, infact mimi namkubali sana sana.
Nauona mwanga mbele yetu kupitia uongozi wake mzuri.

Ila kuja kusema amefanya bora kuliko Nyerere acheni mizaha, nendeni mkamuulize mwenyewe aseme kila siku anapokaa peke yake au na wasaidizi wake anajipima viatu vya Nyerere alivyoviacha kama vinamkaa angalu nusu tu?

Nyerere was from another planet in that sense. He was extraordinary!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…