Hapo sawa.
Nilitaka kukushangaa sana, Nyerere ni habari nyingine.
Hii elimu bure hadi kidato cha nne kwa Nyerere ilikuwa kuanzia darasa la awali, shule ya msingi, sekondari hadi chuo kikuu.
Tena yeye alienda mbali sana kwa kutoa huduma ya chakula bure cha mchana na kifungua kinywa(uji saa nne asubuhi) shule za msingi, sekondari huko usiseme, vyuo vikuu kulikuwa na mabomba ya maziwa, mikate, matunda, vyakula vya kutosha na likizo watu walilipiwa nauli hadi za ndege na serikali.
Yule mzee hakuwa mtu wa kawaida kama waliomfuatia.
Hii inayo itwa mikopo ya elimu ya juu ilikuwa bure kabisa tena 100%.
Kitu cha kushangaza watu waliofaidika kupitia huduma hii ndiyo walikuja kupiga kura bungeni kupitisha sheria ya bodi ya mikopo na wengine kuandaa kanuni wizarani watu walipe hii fedha kama mikopo.
Wakapanga walipe waliofaidika kuanzia miaka ya 1990 na kitu wakajitoa wao wa miaka ya 80's kurudi nyuma wasilipe huduma hizo walizopewa bure na Nyerere.
Hapo kati nchi ilioza sana kwa ubinafsi na ufujaji mali ya umma, hao wazee kama haitoshi wakabadili muda wa kustaafu wakajiongezea muda ili waendelee kula wao na kuajiri ndugu zao.
Wenzetu wanashusha umri wa kustaafu ili kutoa fursa kwa vijana nao waajiriwe wapate mitaji sisi tunafanya kinyume chake!!!