Uchaguzi 2020 Tundu Lissu achambua mifuko ya Jamii na fao la kujitoa, CCM jibuni hoja hizi

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu achambua mifuko ya Jamii na fao la kujitoa, CCM jibuni hoja hizi

Tatizo la wafanykazi wa Tanzania ni midabwada, watu hopeless and stupid ! Kuna wale ambao wana ka upenyo ka kupata bakishishi/marupurupu kazini, haya ya mifuko hayawahusu, "wanafidia" huku wanakochota. Kundi la walimu (siyo wote tafadhali, ila wengi wao wako hivyo) ni kundi la academic failures ambao walipata Div 4 na hivyo kujiona "afadhali" wanapata hata hicho kidogo!
Umesema ukweli mkuu. Yaani ukikaa ni hopeless kabisa. Halafu wana lile lichama linaitwa CWT. Upuuzi mtupu yaani. Wanapata hela lakini washenzi sana. Linapokuja suala la maslahi ya waalimu ni failures tu. Yaani wafanyakazi wa bongo bwana . . . Wajinga ni wengi sana kati yao
 
Mwezi wa tatu huu nahangaika na haya mamifuko kazi yenyewe mkataba uliisha 2018.
Tukajiongeza na kujiajiri ila mambo yamebadilika na mifuko pesa ndio hizo kila siku sheria inasema sheria ..halafu hawafatilii michango kwa waajiri sijui wanakula mlungula.
Pole sana mkuu. Mi ndugu yangu mwezi wa sita anaruka ruka tu hajapata kitu
 
Leteni uthibitisho kwanza wa madai yenu. Yaan chadema kila anachosema Lissu mnaamini tu bila hata kumuuliza yeye kajuaje.
Kasome ripoti ya CAG. Halafu hukumbuki kwamba wabunge waliwahi kutoa hoja kupitia kamati zao kwamba mifuko ya hifadhi ya jamii inabidi ifanyiwe tathmini kama itaweza kulipa mafao miaka ijayo maana hali yake kifedha sio nzuri
 
Nisikiapo hoja za Lissu kwenye mikutano yake ya kampeni na nisomapo hizi mnazoweka humu JF zinanikumbusha zile hoja alizokuwa akitoa alipokuwa Bungeni miaka hiyo. Lissu bado ni MWANAHARAKATI tu kama akina Nyepesi hivyo CCM haina muda wa kujibu hoja za kibunge kipindi hiki cha Uchaguzi. Hoja hizi za Mifuko ya Jamii na Mafao ya wahusika na nyingine kama hizo ni hoja za kibunge. CCMhawajibu masuala ya kibunge humu JF.
 
MKAPA alilipa watu wote FAO LA KUJITOA

KIKWETE ALILIPA WOTE FAO LA KUJITOA

Magufuli akaja Kuondoa FAO la kujitoa

Pesa za NSSF Magufuli umepeleka wapi?

Mtetezi wa wanyonge gani, unarpora Haki..

Mcha Mungu wa Aina gani Magufuli

Unatumia Pesa za Kampeni kutoka wapi na kukaza Mabango barabarani?
 
Magufuli hakuona tatizo la ajira? Labda Ni kipofu, Hana maono.

Halafu akafuta FAO la kujitoa

Magufuli na Ndugai...mmedhulumu haki za wanyonge
 
CCM baada ya kuifilisi mifuko ya hifadhi za Jamii wakaja na fao la kujitoa yaani Kama ulifanya kazi mfano una miaka 30 hakuna kupewa mafao yako ni Hadi ufike miaka 60 utadhani una mihadi na Mungu wakati unategemea pesa zako zikusaidie kuanza maisha baada ya mkataba wa ajira kukoma.

Pia kuna suala la kikokotoo kinachoanza tumika mwakani yaani mfanyakazi ukistaafu miaka 60 hakuna kupewa pesa zako zote unapewa kidogo kidogo tena kwa mafungu ili nyingi ziendelee kubaki kwao sababu Hawana uwezo wa kukulipa maana wamezitumia michango yako.

Tumeona waliofilisi mifuko wakipewa zawadi ya ubalozi badala ya kukaa ndani kwa uhujumu uchumi bali wakosoaji ndio wamebambikwa uhujumu. Maana Kama Ingekuwa ni kweli wanapambana na ufisadi tulitegemea majizi yote yaliyofilisi mifuko yawe ndani.

Fao la kujitoa na kikokotoo huu ni wizi na dhuluma kamili sawa na dhuluma zingine mfano kula rambirambi, kuzulumu wakulima pamba,korosho, mbaazi,kuporwa pesa za watu bureau de change kupitia operation feki, kuzulumu wafanyakazi haki yao ya kikatiba ya nyongeza za mishahara, nk.

Ishu za wafanyakazi zinagusa Makundi yote kwenye Jamii ibomoee ccm kwa kuzungumzia fao la kujitoa na kikokotoo hapa piga spana za hatari maana hapa hawana uwezo wa kujibu hoja yeyeto kutetea fao la kujitoa na kikokotoo.

Huu ni wizi mtupu kuibia wafanyakazi, iweje michango yao wawekewe muda wa kuchukua Hadi miaka 60?
 
Molemo hili swala la kikokotoo na fao la kujitoa ni mambo muhimu na yanayogusa wengi,hivyo mwambieni Lissu alipe mkazo kwenye kampeni zake katiba Siku zilizobaki.

Kingine,mwambieni Lissu atoe ahadi ya kurudisha Bunge live kwani hili jambo litagusa na pia litapokelewa vizuri na watu wengi.
 
Fedha Ni za wafanyakazi, wanyonge

Pesa sio za CCM Wala Magufuli

Ni wizi kufuta FAO la kujitoa

Watu mikataba ikiisha wanaishi Kama watumwa...watu wanaofukuzwa kazi hawana Tumaini Tena la kujiajiri.
 
FAO la kujitoa Ni Haki ya wafanyakazi

Wabunge wanalipwa mafao yote baada ya miaka 5.

Kwa Nini wanyonge waporwe Haki

Wabunge wa CCM wakaondoa FAO la kujitoa kwa kura ndiooo
 
Wabunge wa CCM na Ndugai wakapitisha Sheria Kuondoa FAO la kujitoa...kupora haki
 
Huyu TL anahatari Sana wasiokuwa makini na huyu jamaa ccm chalk,maana kawafanya wapizani wasiwe nauoga
 
Leteni uthibitisho kwanza wa madai yenu. Yaan chadema kila anachosema Lissu mnaamini tu bila hata kumuuliza yeye kajuaje.
Mkuu tukiachana na hizi stori za lissu kwa hela zimetuwaje!
Je wewe utaratibu huu wa mafao ya Wastaafu uliopo unaona uko fair? Fao la kujitoa je? Fao la kukosa ajira kwa sababu za kukoma kwa mikataba?

Yaan hata hii unataka ushahidi?
 
Fao la kujitoa lirudishwe hali ni mbaya! Serikali hii sheria yenu hii ni mbaya sana haifai inaumiza na kudumaza uchumi wa raia.
 
Molemo hili swala la kikokotoo na fao la kujitoa ni mambo muhimu na yanayogusa wengi,hivyo mwambieni Lissu alipe mkazo kwenye kampeni zake katiba Siku zilizobaki.

Kingine,mwambieni Lissu atoe ahadi ya kurudisha Bunge live kwani hili jambo litagusa na pia litapokelewa vizuri na watu wengi.
Mkuu,.

Mchakato wa fao la kujitoa uwe endelevu. Pazeni sauti kila siku tunaumiza uchumi wa mtu mmoja mmoja ni hatari sana.
 
CCM wapo wenyewe Bungeni 99%

Kazi Ni kwao, ajira million 8 kwa Vijana zinatakiwa

Kurudisha FAO la kujitoa

Ajira za Waalimu

Kuajiri Madaktari

Watu wengi wanafariki Dunia bila kulipwa Mafao, NSSF NA PSSSF wanabaki na Mabilioni..

Hizo Pesa wanapeleka wapi?

Kwa niniifuko haikaguliwi na Wafanyakazi wanapewa ripoti?

Pesa za hii mifuko zinaliwa na Vigogo gani? Iko siku Mungu atatupa ufunuo
 
Mkuu,.

Mchakato wa fao la kujitoa uwe endelevu. Pazeni sauti kila siku tunaumiza uchumi wa mtu mmoja mmoja ni hatari sana.

Watu kukosa FAO la kujitoa inaathiri uchumi na TRA itakosa makusanyo ya Kodi.

Wafanyakazi wapewe FAO LA KUJITOA ili wakajiajiri na kuongeza wigo wa walipa Kodi.

Bunge Sasa Ni 100 % CCM

Wananchi wanataka kuona maendeleo na kutendewa Haki.

Sera ya Kikokotoo haileweki... Waziri wa Kazi na ajira atoe ufafanuzi.
 
MUULIZE DUNIANI KOTE KAZI KUU NNE ZA MIFUKO YA HIFADHI ZA JAMII NI. NINI? WASIPOWEKEZA HIZO PESA ZA KUWALIPA WAHUSIKA "WITH INTEREST" ZITATOKA WAPI?

Queen Esther
 
Back
Top Bottom