GE2025 Tundu Lissu afikishwa Mahakama Kuu kwa mara ya kwanza leo Septemba 8, 2025 kujibu kesi ya uhaini

GE2025 Tundu Lissu afikishwa Mahakama Kuu kwa mara ya kwanza leo Septemba 8, 2025 kujibu kesi ya uhaini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
524
Reaction score
829
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, leo Septemba 8, 2025 anafikishwa katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam, kwa ajili ya kesi ya uhaini inayomkabili, kwa ajili ya usikilizwaji wa awali (preliminary hearing - PH).

1761114241569.webp

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa katika hatua hiyo na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Iringa, Dunstan Ndunguru.

Pamoja na mambo mengine Lissu atajibu shitaka hilo kwa mara ya kwanza kabla ya kuendelea na hatua inayofuata kutegemeana na jinsi atakavyolijibu shitaka

Lema ndani ya ukumbi wa Mahakama

---
Update: Lissu akifikishwa mahakamani
Mwanasheria Dkt. Nshala akielezea kilichoendelea kwenye Kesi ya Lissu


View: https://youtu.be/vbQdSEDAmM8?si=yYLd5c5bn8J7CJyy

Maelezo ya Mwanachadema MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila kuhusu kilichoendelea Mahakamani, Kesi yaahirishwa mpaka kesho September 9, 2025
----------

Leo kesi ya uhaini, Jamhuri Vs. Tundu A.M Lissu ilikuwa Mahakama Kuu, Masjala ndogo Dar es Salaam kwa ajili ya kusiliza hoja za awali (preliminary hearing – PH).

Mahakama ilipokea notice of motion kwa mujibu wa kifungu cha 294(1) na 295 cha (CPA) ambayo imesaini na TAL na kupitishwa na Mkuu wa gereza la Ukonga.

Notice of Motion ya TAL ilikuwa na mamombi mawili (1) Pingamizi katika hati ya mashtaka (2) TAL anahoji mamlaka ya Mahakama Kuu ya TZ (jurisdiction).

Huo ndiyo msingi wa Mahakama Kuu kupanga Jopo la Majaji watatu kusikiliza notisi ambayo Tundu Lissu alikuwa amewasilisha katika mfumo wa Mahakama.

Vinginevyo, notice of motion ilitakiwa kwenda Mahakama ya Rufani, huko linaketi jopo na majaji watatu na kuendelea, ili kusikiliza na kuamua kesi husika..

Kwanini ingekwenda Mahakama ya Rufani? Hiyo ni mahakama ya juu ya Mahakama Kuu, anayoilalamikia kwamba haina mamlaka na uhalali wa kusikiliza kesi.

Hoja yake siyo Mahakama Kuu ni ndogo na kwamba haiwezi kusikiliza shauri lake, Hapana. Msingi wa malalamiko mchakato wa committal court una dosari

Kwamba mchakato una irregularities na kwa utaratibu wa kisheria kwa aina ya kosa analoshtakiwa, alitakiwa kushtakiwa katika Mahakama alipokamatiwa, Mbinga.

Halafu committal proceedings ingefanyika Mahakama za chini eneo hilo kabla ya kuanza kusikiliza hoja za awali (preliminary hearing - PH) katika Mahakama Kuu.

Jopo la Mawakili wa Serikali kupitia kiongozi wao, Nassoro Katuga likasisitiza Mahakama isiendelee la PH hadi suala la jurisdiction litolewe uamuzi wake..

Nafikiri hawakujua nini kinakwenda kutokea muda mfupi baadae.., TAL alikuwa tayari kwa jambo lolote ambalo Mahakama ingeamua. PH au notice of motion….

Kabla ya Mahakama kuanza kusikiliza notisi hiyo ya TAL ambayo ndani yake ilikuwa na maombi mawili ikiwepo uhalali wa Mahakam hiyo kusikiliza kesi hiyo…

Tundu Lissu alipewa nakala yake ya committal bundle gerezani. Leo alipofika Mahakamani, akalinganisha na nakala ambayo walikuwa nayo Mawakili wa Serikali.

Nakala hizo mbili zikawa tofauti katika maudhui. Tundu Lissu akaomba kujenga msingi wa hoja yake kwa kuhoji utofauti wa maudhui katika nyaraka hizo mbili…

Ndipo zilipoibuka hoja za nyaraka za Mahakama kuchezewa. ikaonekana tofauti kati ya nyaraka ambayo TAL alipewa gerezani na aliyoikuta Mahakamani.

Jaji akaingia katika kumbukumbu za Mahakama, akaona nyaraka iliyopo imekamilika tofauti na hiyo ambayo Tundu Lissu anayo anasema mambo mengi hayapo…

Kwa hatua za awali TAL alibaini kwamba tarehe za kuanza kuhairisha kesi yake Kisutu ni 18.08.2025 wakati ukweli ni kwamba kesi imeanza kuhairishwa 10.04.2025

Jaji akaamuru Tundu Lissu apewe nyaraka ya Mahakama, Mahakama ikahairishwa kwa dakika 60. TAL akapelekewa nyaraka hiyo, akapitia kwa dakika 12..

Tundu Lissu akagundua tofauti nyingine; muundo wa maandishi (font). Idadi ya kurasa zinatofautina. Tofauti ya maudhui. TAL alasema, nyaraka zimechezewa..

Hapo ikabidi TAL aombe Mahakama itoe amri ya kuhairisha kesi hiyo hadi kesho asubuhi, ili akapitie nyaraka hizo na kuendelea kubaini makosa mengine..

Kumbuka, hapo bado Mahakama haijaanza kusikiliza notisi ambayo Tundu Lissu ameiwasilisha Mahakamani akihoji uhalali wa Mahakama hiyo kusikiliza kesi..

Kesho tena, tutakutana Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar ea Salaam kuendelea kupata shule ya bure ya sheria kutoka kwa SC Tundu A.M Lissu.

Nafikiri nimefafanua kidogo kilichotokea leo Mahakama Kuu ya Tanzania leo. Sisi wengine tunajivunia sana kumuona Tundu A.M Lissu akiwa HAI.

Fuatilia mwenendo wa Kesi na Utetezi

Septemba 9
Septemba 10
Septemba 11
Septemba 15
Septemba 16
Septemba 18
Oktoba 20
 
Wamuachie tu huyo mjuba kwani hana tishio la kuvuruga uchaguzi wao na si tishio la amani ya nchi, wamuachie tu tuone kama atatia timu uwanjani au ataendelea na msimamo wa No reform no election
 
Vikaragosi wapo kwenye kampeni wamepewa magari mapya makali na ya bei mbaya plus ulinzi wa nguvu haijawahi kutokea wagombea kupewa ulinzi wa kufa mtu kiasi hicho. Lissu wamuachie tu pengine mambo ya ajabu yataachwa kuibuliwa kila uchao kuelekea uchaguzi mkuu uliosusiwa na wengi
 
Back
Top Bottom