å Ni majibu ya kauli ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dr. Wilson Mahera Charles aliyoitoa jana alipokuwa anazungumza na vyombo vya habari.
å Kwamba, baadhi ya wagombea katika mikutano yao ya kampeni wanakiuka kanuni na maadili ya uchaguzi mkuu wa 2020.
å Na kwamba, tume inaweza kuwachukulia hatua za kinidhamu ikiwemo kuwazuia kuendelea na kampeni zao.
å Tundu Lissu akiwa Mbozi leo tarehe 16/9/2020 akichanja mbuga kuendelea na mikutano yake ya kampeni, kabla ya kuwahutubia wananchi alitumia dakika 12 kuijibu NEC juu ya kauli yake hii kupitia kwa mtendaji wake mkuu, Mkurugenzi wa Uchaguzi Dr Wilson Mahera Charles.
å Katika kujibu, Tundu Lissu akaikaripia vikali NEC kuwa ndiyo mkiukaji mkubwa wa KANUNI na MAADILI hayo ya Uchaguzi mkuu 2020.
å Akataja makosa matano (5) ya ukiukaji KANUNI na MAADILI yanayofanywa na mgombea Urais wa CCM, ndg John Pombe Magufuli huku NEC wakiwa kimyaaa.
Mbona Jiwe anatoa amri kwa watendaji na kuahidi kutoa pesa kutatua matatizo wakati wa uchaguzi lakini kada Mahera yuko kimya?
Mbona Jiwe anakusanya wanafunzi wakati wa masomo na Mahera yuko kimya?
Hii nchi ina maajabu sana..
Lissu ni saiz yake,makavu ndiyo anayaelewa-shida Lumumba hawajawahi kufikiria siku moja mtu atatokea na kuwafungua macho wananchi kwa style ya lissu ya kuhutubia;Lissu ana skills ya kufikisha taarifa ngumu kwa mtu wa chini kwa jinsi rahisi ambayo ataielewa.
Mpaka uchaguzi uishe Mzee mkubwa credibility yake itakuwa imepungua mno kwa jinsi Lissu anavyo yafumbua mambo yake yake ya kificho hadharani sababu wananchi walikuwa wanamvumilia wakiamini hana scandal ila mambo ni tofauti