The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Jamaa mara baada ya kuwachanachana CCM, saa saba za mchana siku hiyo ya tarehe 7/9/2017 akapigwa risasi mchana kweupe. Mungu Mwenyezi alimnusuru na kifo yu hai leo, bila shaka huyu ndiye Rais ajaye wa Tanganyika.
Pamoja na jaribio la serikali ya CCM chini ya Rais Magufuli kutaka kumuua mkosoaji wake mkuu, hata hivyo hiyo haikufuta ukweli kwamba, kilichokuwa kinafanywa na mwendazake John P. Magufuli yalikuwa na maigizo yasiyotumia maarifa na kukosa weledi ndani yake.
Ushahidi ni kuwa, mpaka leo zile Trilioni 197 tulizoambiwa ziliibiwa na kwamba tungelipwa kama nchi ili kila mwananchi mkubwa kwa mdogo anunue Noah yake, zimeyeyukia hewani na pengine zimemfuata mwenyewe "Hayati" huko huko aliko Chato!