POTOSHI Tundu Lissu alisema 'Chama chetu tunafuata maelekezo na agenda kutoka ulaya'

POTOSHI Tundu Lissu alisema 'Chama chetu tunafuata maelekezo na agenda kutoka ulaya'

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Wakuu,

Tupeni uhakiki hapa, naamini Mwenyekiti Kamanda Tundu Lissu hawezi kuruhusu huu ukoloni

1759823722099.png
 
Tunachokijua
Tundu Lissu ni mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambaye ameshikilia nafasi hiyo kuanzia Januari 2025 baada ya kumshinda mwenyekiti aliyekuwa anamaliza muda wake Freeman Mbowe.

Kipo kipande cha video kinachosambazwa mtandaoni kikimuonesha Lissu akizungumza na waaandishi wa habari kikiwa na kichwa cha habari "Chama chetu tunafuata maelekezo na agenda kutoka Ulaya"


Je, ni kweli Lissu alitoa kauli hiyo?


Kupitia marejeo ya video imebainika kichwa hicho cha habari kinapotosha uhalisia kwani Lissu hakutoa kauli hiyo. Kutokana na majibu ya Google Reverse image search, yanaonesha sehemu ya video hiyo na kueleza ilikuwa Januari 06, Tundu Lissu alipokuwa makamu mwenyekiti wa CHADEMA akiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere baada ya kuwasili baada ya kuwepo Brussels, Ubelgiji, katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka 2024 na mwanzo wa 2025.

Aidha alipoulizwa kuhusu safari zake za mara kwa mara za ughaibuni Lissu alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa chama chake na jumuiya ya kimataifa na kwamba alikuwa akifanya majukumu ya chama nje ya nchi kadri alivyohitajika.

"Kwa shughuli zote za chama ambazo nahitajika kuzifanya, nazifanya zote. Kazi ya chama, kazi ya siasa kwa nchi kama ya kwetu hii vilevile ni kazi ya kimataifa, lazima uweze kuzungumza na jumuiya ya kimataifa, wakikwambia njoo tuzungumze inabidi uende na ukazungumze lugha wanayoijua, sasa mimi nafanya kazi ya chama, napohitajika kufanya kazi ya chama nje ya nchi vilevile nafanya. Nimefanya hivi nikiwa mgonjwa, miaka mitano nikiwa ubelgiji nafanya kazi ya uenezi wa chama kwenye ulingo wa kimataifa, huwezi ukashinda hii vita bila kujenga urafiki na jumuiya ya kimataifa"
​
Back
Top Bottom