PreGE2025 POTOSHI Tundu Lissu alisema 'No reforms, No election' sio msimamo sahihi, unaenda kuua chama

PreGE2025 POTOSHI Tundu Lissu alisema 'No reforms, No election' sio msimamo sahihi, unaenda kuua chama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
1751461181218.png
 
Tunachokijua
Tundu Lissu ni mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambaye anakabiliwa na makosa ya uhaini na uchochezi. Tarehe 09 Aprili, 2025 Lissu alikamatwa na jeshi la polisi mara baada ya mkutano wa hadhara alioufanya Jimbo la Mbinga mkoani Ruvuma na kusafirishwa hadi Dar es Salaam.

Katika muendelezo wa kesi, Julai 01, 2025 Kesi yake ya uhaini iliitwa tena na kusikilizwa na kuhairishwa tena hadi Julai 15, 2025.

Awali, Aprili 3, 2025, Lissu alifanya mkutano na viongozi wa chama hicho na watia nia wa nafasi za ubunge ambapo pamoja na mambo mengine alizungumzia kasoro walizozibaini katika chaguzi zilizopita (Mwaka 2024, 2020 na 2019) na kunyima haki kwa vyama vya upinzani.

Video iliyochapishwa TikTok ikimhusu Lissu.

Mtumiaji mmoja katika mtandao wa TikTok anayetumia jina la 'Mapinduzi 64' alichapisha kipande cha video ambacho ni sehemu ya hotuba ya Lissu kikimuonesha akisema 'No reforms, No election' ni msimamo usio sahihi, unaenda kuua chama.


Je, ni upi uhalisia wa kipande hicho cha video?

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google Reverse Image Search umebaini kuwa kipande hicho cha video kimepotoshwa uhalisia wake kutoka kwenye hotuba aliyoitoa Lissu Mwezi Aprili 03, 2025 katika mkutano na viongozi wa chama hicho na watia nia wa nafasi za ubunge.

Kipande hicho kilipotoshwa kwa kukata vipande vidogovidogo kutoka kwenye hotuba ya Lissu na kuviunganisha isivyostahili jambo lililosababisha kupotosha ujumbe halisi uliokusudiwa na Lissu. Katika hotuba hiyo sehemu iliyohusisha video hiyo Lissu alisema, (Rejea hapa, 1:09:27)

"Msimamo wa chama (kuhusu 'No Reforms, No Election') ulipitishwa na Kamati Kuu mimi (Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa) sikuwa Mwenyekiti wakati huo, ulipitishwa na Kamati Kuu chini ya Mwenyekiti Mbowe, wakati huo nilikuwa Makamu Mwenyekiti, msimamo wa chama ni 'No Reforms, No Election', na kwa Katiba hii (Anaonesha Katiba ya CHADEMA) mkutano mkuu ukisema twende hivi ni chombo gani kingine kinaweza kupinga?, na naomba mniambie wajumbe (watia nia wa Ubunge kwenye majimbo mbalimbali nchini kupitia CHADEMA), kwa haya yote mnayoyafahamu nani anaesema msimamo huu sio sahihi?, na mimi nataka nichaguliwe kwenye kacheo fulani nchi hii, wote tunataka kuchaguliwa lakini kwa hali ilivyo hilo haliwezekani bila reforms, hivyo 'No Reforms, No Election“

"Waheshimiwa Wajumbe, na mimi nataka nichaguliwe kwenye kacheo fulani nchi nii. Na nyie mnataka mchaguliwe kwenye kacheo fulani nchi hii, wote tunataka tuchaguliwe. Kwa hali ilivyo, hilo linawezekana? Kama haliwezekani tufanyeje? Wamesema kitu kimoja sahihi hapa, wanasema hivi, msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi hiyo ndiyo namna ya kupata mabadiliko,"



View: https://youtu.be/xX44JN7_9hk?si=I0wvqTBH5vgbxF6W&t=4167​
Tatizo la watu wengi hawajui kwamba Agenda ya "No reform no election" Siyo ya Chadema...ni ya Watanzania wenye kujielewa na haikuanza na Chadema Wala Lisu ipo kitambo Sana....huuu ni mwendelezo tu wa kudai mabadiliko ya Sheria, kanuni taratibu na mifumo yote ya kusimamia haki, usawa na demokeasia.
 
Back
Top Bottom