Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amekutana na Waandishi wa habari kuelezea mwenendo wa kampeni. Asema Jaribio la kuvuruga Uchaguzi litasababisha watu wapelekwe 'The Hague'

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amekutana na Waandishi wa habari kuelezea mwenendo wa kampeni. Asema Jaribio la kuvuruga Uchaguzi litasababisha watu wapelekwe 'The Hague'

Mbona juzi kati hapa kapigwa pini na USA na amenywea. Boya Kama Boya Wengine. Ukiona Mtu yeyote kutoka Nchi Maskini Kama Afrika anapewa Position kubwa Kama hiyo, basi ujue, lengo ni atumike dhidi ya Waafrika wenzake. Huyu Bibi na the late Kofi Anan ni mifano hai!

Hata taasisi za kimamlaka hapa nchini zinatumika na ccm kunyima haki.
 
Huyu jamaa na the hague yake bana.. Ndo sawa na wale watoto anakishajua hana haki ya kupata anachokitaka anaanza kujiliza ili mkubwa uliepo umuonee huruma usimamie apewe anachokitaka.. Lissu mbona vitisho vimekuwa vingi sana! Tulia upigwe spana dadek, utajuta kilichokuingiza kwenye huu mchakato
Screenshot_20201024-111116_1.jpg
 
Mgombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo amekutana na Waandishi wa habari kuzungumzia hali ya ya kampeni zake ilivyo mpaka sasa na kile kinachoendelea kuelekea Uchaguzi Mkuu mnamo tarehe 28/10/ 2020. katika Mkutano huo ambao waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali walihudhuria, Tundu Lissu ametolea ufafanuzi wa masuala mbalimbali.

Aidha, akianza kutoa tathmni ya kile kinachoendelea katika kampeni zao Tundu Lissu alisema "Kwa ujumla tumefanya kazi kubwa sana na nyie ambao mpo kwenye msafara huu mmeona na Watanzania wameona. Tumefanya mikutano mingi kuliko mikutano yote aliyofanya mpinzani wetu Mkuu Rais Magufuli pamoja, Makamu wake pamoja na Waziri Mkuu kwa combined. Yaani mikutano ambayo tumeifanya sisi ni mingi kuliko ambayo wameifanya wao kwa ujumla wao.

Mikutano yetu imekuwa na mafanikio makubwa sana kuliko ambavyo sisi wenyewe tulitegemea mwanzoni, hakuna mkutano ambao imebidi tusafirishe mtu yeyote. Mikutano yetu imehudhuriwa na maelfu kwa maelfu ya Watanzania ambao wametembea wao kwa miguu yao, wamekuja kwa vyombo vyao wamekuja kwa namna mbalimbali za usafiri kwa kujitegemea. Mikutano yote ya Chama cha Mapinduzi watu wanakwenda kwa kulazimishwa, wanapeleka watoto wa shule baada ya kuwalazimisha kwa kufunga shule, kutisha waalimu, wanafunga Maofisi ya serikali na kulazimisha wafanyakazi kwenda kumsikiliza Magufuli.

Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amesema jaribio lolote lenye nia ya kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 na kutumia mabavu litapelekea watu kufikishwa Mahakama ya Kimataifa 'The Hague'

Amesema, "Kuna uchunguzi unaendelea, wa matukio yote ambayo yanafanyika na yameshafanyika. Kuna list (orodha) ya watu wanaoangaliwa"

Ameongeza kuwa, yeyote atakayetumia mbinu za kiharamia kuvuruga Uchaguzi na kusababisha maafa kwa Watanzania anajiingiza mwenyewe katika orodha hiyo.

Katika orodha hiyo Lissu ni nambari wani
 
Aache ujinga kila saa wazungu wazungu yaani domoni mwake kumejaa wazungu tu ohhh madini tutayaweka rehani kwa wazungu ohhh Amsterdam ohhh the Hague ohhh Mimi najua kingereza

Lisu lazima tumupnyesha kuwa Tanzania ni ya waswahili sio wazungu tarehe 28 October hatumpi kura
Sio kwa kura, hilo daftari la wapiga kura mmelichezea ili mpate ushindi wa wizi mmechemsha. Halafu Zec bila aibu wanasema eti watu hawajaenda kuhakiki taarifa!
 
Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amesema jaribio lolote lenye nia ya kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 na kutumia mabavu litapelekea watu kufikishwa Mahakama ya Kimataifa 'The Hague'

Amesema, "Kuna uchunguzi unaendelea, wa matukio yote ambayo yanafanyika na yameshafanyika. Kuna list (orodha) ya watu wanaoangaliwa"

Ameongeza kuwa, yeyote atakayetumia mbinu za kiharamia kuvuruga Uchaguzi na kusababisha maafa kwa Watanzania anajiingiza mwenyewe katika orodha hiyo.
Hi ni muhimu Sana ili wananchi na wapiga kura kwa ujumla wasipandwe kichwani na NECcm, policcm, nk
 
Dalili za mvua kwa yanayoendelea Mafeni amegoma kurudi kwao anataka kwenda the Hague nasi hatuna Cha kupingana na maamuzi yake maana asiyefunzwa na mama dunia bado haijawahi acha kufunza
 
Wewe kwa akili yako, Magufuli anaweza kusimama The Hague akajitetea kama akitakiwa hivyo mana kuongea point tu kwa kiswahili hawezi sembuse kule.

Kinuke tu!
Wewe ukipelekwa huko unaweza kujitetea? Very stupid..why should Magufuli be sent to The Hague and Not Lissu ? Stupid...Do you think by pointing out that Tanzanians will waver..? We are tired of this nonsense
 
Hakuna kipindi chama chakavu kimekamatika Kama this time tuliwaambia wekezeni kwenye mioyo ya watz mkatudharau mkawekeza kwenye dola badala ya watu. Tumieni hata paundi na euro kabisa lkn hamuwezi tena kuokolewa nazo. Haijawahi tokea mgombea wa ccm kuacha kwenda kusini kuomba kura ndo mjue kusini hawana chao.
Gharama za kuiba kura ni kubwa mno kuliko Kama mngewekeza kwenye kuboresha maisha ya watz. Mlisomesha watz namba why hamtaki kuzisoma kura zao?
 
True huu mwaka hatuna mchezo na uchaguzi
Mbinu zote tegemezi za wizi zimebuma,vituo hewa majina hewa zimebuma mapolisi wamehaha kusaka center za kudakia matokeo halisi ya upinzani wamebuma mara wamkamate mdee, mara Heche, mara lema, mara matiko hovyo kabisa, yameambulia patupu.
Eti yamelimit sms wakati njia za mawasiliano zipo zaidi ya mia Hawa ni zero kabisa na mbinu zao za stone age
 
Sirro at ajiuzulu kabla ya matokeo ya uchaguzi kutoka
Huyu jamaa na the hague yake bana.. Ndo sawa na wale watoto anakishajua hana haki ya kupata anachokitaka anaanza kujiliza ili mkubwa uliepo umuonee huruma usimamie apewe anachokitaka.. Lissu mbona vitisho vimekuwa vingi sana! Tulia upigwe spana dadek, utajuta kilichokuingiza kwenye huu mchakatoView attachment 1610392
Mbona Magufuli Kawa Rais na amedhihirisha kama urais tu hata binti wa chekechea anaweza kuwa Rais na mambo yakaenda
 
Lissu nae pumbavu tuu kila siku the Hague, ICC, Amsterdam! Hili jitu tumwa la mawazo linawaza kitumwa tumwa kila siku. Lunaabudu wazungu badala ya kuwaza utanzania na nchi yetu linawaza ulaya tuu.
Na hiyo Dec 18 aliyosema anaenda ubelgiji ifike aende zake haraka pumbafff.
 
Mgombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo amekutana na Waandishi wa habari kuzungumzia hali ya ya kampeni zake ilivyo mpaka sasa na kile kinachoendelea kuelekea Uchaguzi Mkuu mnamo tarehe 28/10/ 2020. katika Mkutano huo ambao waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali walihudhuria, Tundu Lissu ametolea ufafanuzi wa masuala mbalimbali.

Aidha, akianza kutoa tathmni ya kile kinachoendelea katika kampeni zao Tundu Lissu alisema "Kwa ujumla tumefanya kazi kubwa sana na nyie ambao mpo kwenye msafara huu mmeona na Watanzania wameona. Tumefanya mikutano mingi kuliko mikutano yote aliyofanya mpinzani wetu Mkuu Rais Magufuli pamoja, Makamu wake pamoja na Waziri Mkuu kwa combined. Yaani mikutano ambayo tumeifanya sisi ni mingi kuliko ambayo wameifanya wao kwa ujumla wao.

Mikutano yetu imekuwa na mafanikio makubwa sana kuliko ambavyo sisi wenyewe tulitegemea mwanzoni, hakuna mkutano ambao imebidi tusafirishe mtu yeyote. Mikutano yetu imehudhuriwa na maelfu kwa maelfu ya Watanzania ambao wametembea wao kwa miguu yao, wamekuja kwa vyombo vyao wamekuja kwa namna mbalimbali za usafiri kwa kujitegemea. Mikutano yote ya Chama cha Mapinduzi watu wanakwenda kwa kulazimishwa, wanapeleka watoto wa shule baada ya kuwalazimisha kwa kufunga shule, kutisha waalimu, wanafunga Maofisi ya serikali na kulazimisha wafanyakazi kwenda kumsikiliza Magufuli.

Wataalamu wetu wa mahesabu na watu ambao wanafuatilia wanafanya survey za muelekeo wa Upigaji kura wanatuambia kwamba kwa jinsi ambavyo mikutano yetu imekwenda ya kampeni, kwa jinsi ambavyo tumefanya mikutano yaetu tunashinda uchaguzi huu kwa asilimika kati ya 65 hadi 75 huo ni mtazamo wa watua ambao tumewaopa kazi wa kufanya survey ya Wapiga kura nchi nzima.

Hali yetu ni nzuri sana. Kwahiyo, Magufuli nje ya Tume ya Uchaguzi, nje ya wasimamizi wa Uchaguzi aliowateua. Makada wa CCM ndio Wakurugenzi na Wasimamizi wa Uchaguzi, nje ya kufanya vurugu, nje ya kuiba kura hawezi akashinda uchaguzi huu kwa sababu hana kibali cha Watanzania tena. Kwahiyo kwa sababu hana kibali cha Watanzania na kampeni yake inadoda kila mahali tunaona sasa vitendo ambavyo tulivitabiri mwanzoni. Tulisema kwamba hawa watu hawawezi wakashinda Uchaguzi ulio huru na haki na tayari tunaanza kuona dalili hizi aidha kuharibu uchaguzi, au kufanya wizi mkubwa wakitumaini kwamba labda pengine atabaki madarakani.

Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amesema jaribio lolote lenye nia ya kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 na kutumia mabavu litapelekea watu kufikishwa Mahakama ya Kimataifa 'The Hague'

Amesema, "Kuna uchunguzi unaendelea, wa matukio yote ambayo yanafanyika na yameshafanyika. Kuna list (orodha) ya watu wanaoangaliwa"

Ameongeza kuwa, yeyote atakayetumia mbinu za kiharamia kuvuruga Uchaguzi na kusababisha maafa kwa Watanzania anajiingiza mwenyewe katika orodha hiyo.

Utoto huo, au siyo riziki?
Uchaguzi utashindwa vibaya, ukileta fujo unachapwa na machizi wenzako
Tanzania ukipata Uhuru 1961!
 
Hakuna maafa yeyote yatatokea hapa nchini kwenye huu uchaguzi!

Lisu atapigwa mbela na nyuma kisha anarudi zake ubelgiji
 
Back
Top Bottom