Nani asiyejua huyo mgombea wenu alivyo na mdomo mchafu?
Taja hayo matusi ili tujiridhishe ni kweli au ni hoja zake mnazoshindwa kuzijibu kwa mnataka vyombo vya ulinzi na usalama,NEC na Msajili wawasaidie.
Kikwete aliwaambie msitegemee hivyo vitu mtakuja anguka. Lissu sasa hivi anawaambie polisi hamjaongezewa mshahara miaka mitano, kuna kikokotoo kipya kipo pending kupisha uchaguzi,kinarudi 2021. Wakiwaamrisha mtupige mabomu msikubali maana mtamsaidie mtu ambae hajali maslahi yenu wala ya ndugu zenu. Ujumbe huo huo ameeafikishia watumishi wengine wa umma. Au haya ndiyo unayoyaita matusi?
Magufuli alikuwa anatuswaga kama hakutokuwa na uchaguzi,sasa hivi anajifanya kukenua meno na kurukaruka mziki wa akina Zuchu,hatudanganyiki tunajua jiwe hawezi kubadilika na tutamkataa ili aibe kura aongoze kwa mabavu bila ridhaa yetu wananchi.
Yaani kila sehemu unayogusa moto wa maisha magumu umewaka kuanzia utumishi wa umma mpaka sekta binafsi,tena husijaribu kujiajiri utakoma,kwenye kilimo moto mazoao ya biashara yote yameporoka bei,kuanzia korosho,ufuta,mbaazi,pamba,tumbaku,katani mpaka kahawa.