James Martin
JF-Expert Member
- Apr 2, 2016
- 1,206
- 1,509
Nimejaribu kufuatilia mwenendo wa Tundu Lissu tangu mchakato wa kampeni uanze. Kiwango cha Uhuru aliopewa na serikali ni kikubwa sana.
Hata yeye mwenyewe nina uhakika wala hakutarajia. Yaani imekuwa kama surprise kwake. Haiwezekani ametua airport hajabughudhiwa. Amefanya kampeni kipindi cha kukusanya saini hajabughudhiwa. Ameenda kurudisha fomu tume ya uchaguzi hajabughudhiwa. Na kibaya zaidi kipindi hiki cha kampeni anatoa lugha ya matusi kwa Rais lakini hajabughudhiwa.
Sasa ni wakati wa kusema enough is enough. Upole huu wa serikali utatufikisha pabaya tusipokuwa makini kama nchi. Lazima huyu mtu awe held responsible kwa maneno na matendo yake
Hajapewa uhuru ila ANAUTUMIA uhuru wake ilimradi hajavunja sheria. Nafikiri wewe bado una mawazo ya ki CCM na ya kitwana mpaka umsubiri Magufuli akwambie ongea ndio unaongea.