Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amepewa uhuru uliopitiliza

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amepewa uhuru uliopitiliza

Nimejaribu kufuatilia mwenendo wa Tundu Lissu tangu mchakato wa kampeni uanze. Kiwango cha Uhuru aliopewa na Serikali ni kikubwa sana.

Hata yeye mwenyewe nina uhakika wala hakutarajia. Yaani imekuwa kama surprise kwake. Haiwezekani ametua airport hajabughudhiwa. Amefanya kampeni kipindi cha kukusanya saini hajabughudhiwa. Ameenda kurudisha fomu tume ya uchaguzi hajabughudhiwa. Na kibaya zaidi kipindi hiki cha kampeni anatoa lugha ya matusi kwa Rais lakini hajabughudhiwa.

Sasa ni wakati wa kusema enough is enough. Upole huu wa serikali utatufikisha pabaya tusipokuwa makini kama nchi. Lazima huyu mtu awe held responsible kwa maneno na matendo yake
Taja matusi angalau matatu tuu...
 
Mleta mada alitaka Lissu akitua airport abughudhiwe!

Akienda kuchukua saini za wadhamini abughudhiwe!

Akifanya kampeni abaghudhiwe!

Mleta mada anashangaa imekuwaje kuwaje Lissu hajabughudhiwa?
Hivyo anaishauri serikali imbughudhi!

Hivi bughudha za risasi 16, kunyimwa matibabu na kunyimwa kiinua mgongo chake cha ubunge bughudha hizo hazikutoshi?
Kwa ujumla huu ni mfano wa baadhi ya watanzania walivyo na roho mbaya na ya kikatili, yaani hapa roho yake ingefurahi sana kama angesikia Lissu alivyotua airport kadakwa na kavunjwa mikono kama ilivyokuwa kwa akina Halima na Bulaya. Hajali kwamba sheria ina vunjwa wala nini, yeye angetamani hata kampeni Lissu apigwe mabomu au asweke lupango, hapo roho yake rahaaa, hata kama hapati chochote.
 
Back
Top Bottom