- Source #1
- View Source #1
Habari za weekend wakuu
Uhalisia wa taarifa hii kuhusu Lissu umekaaje wakuu maana napata utata nimepita katika page za JamiiForms sijaiona kabisa
Uhalisia wa taarifa hii kuhusu Lissu umekaaje wakuu maana napata utata nimepita katika page za JamiiForms sijaiona kabisa
- Tunachokijua
- Tundu Lissu ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA tangu mwaka 2019 alipochaguliwa kutumikia nafasi hiyo, pia alikuwa mbunge wa jimbo la Singida mashariki kuanzia mwaka 2010 mpaka mwaka 2020 ambapo wagombea wengi wa upinzani hawakufanikiwa kushinda nafasi mbalimbali wakati wa uchaguzi huo.
Lissu ni mwanasiasa anayesifika kwa kuwa muwazi na msema kweli kutokana na haiba yake ya kukosoa na kutokufumbia macho ukiukwaji wa haki za binadamu, demokrasia na masuala mbalimbali yenye maslahi kwa umma.
Mnamo tarehe 12 na 13 Novemba 2024 Lissu alizungumza na waandishi wa habari akiwa mkoani Singida, pamoja na mambo mengine alikosoa ukiukwaji wa taratibu za kidemokrasia katika michakato mbalimbali kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo pia alitumia nafasi hiyo kukemea rushwa ndani na nje ya chama chake.
Unaweza kurejea mikutano hiyo ya Lissu na waandishi wa habari hapa na hapa.
Kumekuwapo na chapisho linalosambaa mitandaoni linalomuhusisha Lissu kuwa ametaka hoja zake zijibiwe na CHADEMA, huku ikiambatanishwa barua ya taarifa kwa umma inayobainisha hoja hizo kuwa ni rushwa na uwepo wa pesa chafu katika michakato ya ndani ya chama, pia ukosefu wa wagombea katika baadhi ya maeneo katika Chapisho linalodaiwa kuwa limetolewa na JamiiForums.
Je ni upi uhalisia wa Chapisho hilo?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini chapisho hilo si la kweli na halijatolewa na JamiiForums, huku ikibaini kuwa barua ya taarifa kwa umma iliyoambatanishwa katika chapisho hilo haijatolewa na Tundu Lissu wala CHADEMA.
Tarehe 15 Novemba 2024 JamiiForums haikuchapisha chapisho hilo katika mitandao yake rasmi ya kijamii tofauti na chapisho hilo linaloonesha tarehe hiyo na kudai kuwa lilitolewa na JamiiForums.
Aidha Chapisho hilo lisilo la kweli limebainika kuwa na mapungufu kadhaa ukilinganisha na machapisho rasmi ambayo hutolewa na JamiiForums katika kurasa zake za mitandao ya kijamii, sehemu ya mapungufu hayo ni kutofautiana kwa rangi, ambapo rangi iliyotumika haitumiwi na JamiiForums katika maudhui ya kisiasa, pia kutofautiana kwa mwandiko (fonts) wa maandishi yaliyotumika kuandika kichwa cha habari (title), si ule unaotumiwa na JamiiForums.
Vilevile chapisho hilo linaonesha alama ya taarifa zaidi kuelekea upande wa kulia lakini lina ukurasa mmoja tu ambapo hakuna taarifa zaidi ya ukurasa huo (hakuana slides)
Aidha katika mapungufu yaliyobainika katika barua hiyo ya taarifa kwa umma ambayo inadaiwa kutolewa na Tundu Lissu mwandiko uliotumika katika kichwa cha habari ni tofauti na unaoutmiwa na barua rasmi za CHADEMA, kadhalika kutokea kwa jina la mhusika anayedaiwa kuandika barua katika kichwa hicho. Kadhalika matumizi ya Wingi na umoja kwenye malalamiko hayo, ambapo maudhui haioneshi malalamiko ya Lissu badala yake inaonesha naye ni sehemu ya watu wanaotakiwa kujibu hoja hizo.
Hata hivyo barua hiyo haijachapishwa katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya CHADEMA wa makamu mwenyekiti wa chama hicho ambapo mpaka leo Novemba 16, 2024 mara ya mwisho ukurasa wake wa mtandao wa X unaonesha alichapisha mnamo Oktoba 17, 2024.
Chapisho hilo limehifadhiwa hapa.